MSHAMBULIAJI wa Yanga, Hamis Kiiza amesema bao alilofunga dhidi ya Ruvu Shooting ni zawadi kwa beki Ladislaus Mbogo.
Mlinzi
huyo amelazwa kwenye hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam,
baada ya kufanyiwa upasuaji Machi 12, mwaka huu kuondoa uvimbe kwenye
shavu lake la kushoto.
Kiiza alisema; "Nilipania kufunga tangu mwanzo kwa lengo la kuiweka timu yangu karibu na ubingwa wa ligi msimu huu."
"Nafikiri hilo nimetimia na kuzidi kuweka matumaini yetu hai kutwaa taji la ligi kwa msimu huu."
Alifafanua kuwa kwa sasa wanahitaji pointi 12 tu kuwa mabingwa wapya wa ligi.
"Tunatakiwa kushinda mechi nne kufikisha pointi hizo na kuwa mabingwa."
Kiiza
alisema anaamini ushindi huo umemgusa kila mwenye kuitakia mema Yanga,
Lakini kubwa ambalo angependa kulisema ni ushindi huu kuupeleka kwa
mchezaji mwenzao Mbogo aliyelazwa katika hospitali ya
Mwananyamala.
"Goli nililofunga nimelitoa kama zawadi kwa mwenzetu Mbogo (Ladislaus) ambaye amefanyiwa upasuaji hivi karibu." alisisitiza.
Nafurahi kuona wachezaji wetu wanaupendo miongoni mwao ....They are kipin real Yanga Daima Mbele
ReplyDelete