SIMBA CHALI ANGOLA, JAMHURI YATIA AIBU, AZAM FC YAIKOA TANZANIA KWA USHINDI MZITO SUDAN - SASA KUKUTANA NA BARRACK Y.C.II YA LIBERIA
Ushindi wa 5-0 dhidi ya Al Nasri Juba ya Sudan Kusini, umeipa Azam FC
nafasi ya kuingia hatua ya pili ya mashindano ya Kombe la Shirikisho
Afrika kwa kuitoa timu hiyo kwa jumla ya magoli 8-1.
Azam FC
inashiriki kwa mara ya kwanza mashindano hayo yanayoandaliwa na
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imefanikiwa kuvuka hatua ya awali na
kuingia hatua ya pili ambapo zimesalia timu 36.
Azam FC imefikisha idadi hiyo ya magoli baada ya kupata ushindi wa 3-1
katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam wiki mbili zilizopita na leo wakacheza mechi ya pili kwenye
Uwanja wa Juba nchini Sudan Kusini na kupata ushindi mnono wa 5-0 wakiwa
ugenini na kufikisha jumla ya magoli 8-1.
Kwa timu za
Tanzania zinazoshiriki mashindano ya CAF, ni Azam FC pekee iliyosalia
baada ya timu za Simba SC kutolewa na Recreativo Libolo ya Angola kwa
jumla ya magoli 5-0, na Jamhuri ya Pemba nayo ikatolewa na St. George ya
Ethiopia kwa kipigo cha jumla cha 8-0 zote zilikuwa zinacheza Klabu
Bingwa Afrika.
Azam FC wanabaki kuwa wawakilishi pekee wa
Tanzania katika mashindano ya CAF, watakutana na mshindi kati ya Barrack
Y. C. II ya Liberia na Johansens ya Sierra Leone.
Katika
mchezo wa leo ambao Azam FC walipata ushindi wa 5-0, magoli yalifungwa
na Khamis Mcha magoli matatu ‘Hat Trick’, John Bocco na Salum Abubakar
wamefunga goli moja moja.
Azam Fc katika mchezo wake wa kwanza
ilipata ushindi wa 3-1 magoli ya Azam FC yakifungwa na Abdi Kassim na
Kipre Tchetche aliyefunga magoli mawili.
Kikosi kamili cha
Azam Fc kitarejea nchini kesho kwa maandalizi ya mchezo wao mwingine wa
Kombe la Shirikisho utakaochezwa kati ya Machi 15-17 mwaka huu.
HONGERENI AZAM FC. KWA SIMBA TULITABIRI ZAMANI HATIMAYE HATA WACHEZAJI SASA WANAULAUMU UONGOZI KWA KUENDESHA TIMU KISIASA! MAJUTO NI MJUKUU SIMBA TUCHUKUE MAAMUZI MAGUMU MAPEMA ILI KUINUSURU TIMU. NA WITO KWA VIONGOZI NI KUWA UNAPOELEMEWA NA MAJUKUMU NI VZR KUSTEP DOWN KIUSTAARABU! CYO HADI USUBIRI VURUGU! NA NINAWAOMBA WANA SIMBA WAWE WATULIVU WAKATI HUU NA KULETA MABADILIKO KWA UTULIVU NA KWA KUFUATA UTARATIBU KWA MUJIBU WA KATIBA YA SIMBA. NAOMBA KUWASILISHA. NURU SPORTS MSM.
ReplyDeletesasa mbona habari za simba ujaziandika sawasawa we acha unazi pamoja inauma na kuwachoma kwa kipigo.we andika jinsi kipigo kilivyokuwa.na sisi watani zako tuzisome.
ReplyDeletehongera Azam. Hilo liwe ni somo kwa Simba na Jamhuri
ReplyDelete