MWANARIADHA wa Tanzania Sara Makela,amewatoa kimasomaso
Watanzania baada ya kushika nafasi ya kwanza katika mbio za Half
Marathon kwa Wanawake,huku Wakenya wakiendelea kutamba katika mbio hizo zilizofanyika jana kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini hapa. Kwa matokeo hayo Sara,amejizolea Sh milioni 3. Sara aliwashinda wenzake baada ya kutumia saa 1:13.05,huku akifuatiwa na Victoty Chepkemoni (Kenya), 1:14.34,Failuna
Malanga
(Tanzania) 1:15.35,Joyce Kiplimoo (Kenya) , Paulina Muchiri (Kenya),
Catherine Tuku (Tanzania), Nancy Kotich (Kenya),Jacinta Mboani
(Kenya),Florence Cheruiyot (Kenya) na Phylas Jelagat (Kenya). Kwa upande wa Half Marathon Wanaume, Sila Limo (Kenya),aliibuka mshindikwa kutumia saa 1:03.46,hukumshindi wa pili akiwa Benard
Kiprotich (Kenya), akitumia 1:04.00, wakatimshindi watatu ni Charles
Ogahri (Kenya),akitumia 1:04.25, Dickson Marwa(Tanzania), saa 1:04.30,
Peter Kosgei (Kenya), akitumia saa 1:04.42, Evans Taiget (Kenya),
akitumia saa 1:04.46, Stephano Huche (Tanzania), akitumia saa
1:04.52, Patric Wambugu (Kenya),alitumia saa 1:04.56,Said Makula
(Tanzania), akitumia saa1:05.03 na nafasi ya kumi ilishikwa na Peter
Jule (Tanzania), aliyetumia saa 1:05.09.
Kwa upande wa Full
Marathon kwa Wanaume, mshindi wa kwanza ni Kipsang Kipkemoi (Kenya),
aliyetumia saa 2:14.56 na kujinyakulia Sh milioni 3, huku mshindi wa
pili akiwa Julius Kilimo (Kenya), akitumia saa 2:15.44 na
kujinyakulia Sh 1.5, huku mshindi wa tatu akiwa Dominic Kangor (Kenya),
akitumia saa 2:16.25 na kujinyakulia Sh laki nane na nusu, nafasi ya
nne ilikwenda kwa Onesmo Maitinya (Kenya), akitumia saa 2:16.36 na
kujipatia Sh laki sita na nusu, huku nafasi ya tano ilikwenda kwa
Lioshiye
Moikan (Tanzania), akitumia saa 2:17.50 na kujipatia Sh laki tano, huku nafasi ya sita ikienda kwa Abraham Kipkosgei (Kenya), aliyetumia
saa 2:18.7 na kujinyakulia Sh laki 3 na nusu, nafasi ya saba ilishikwa
na Alex Bartilol (Kenya), aliyetumia saa 2:18.14 na kujipatia Sh mbili
na nusu, wakati Justus Mebur (Kenya) alishika nafasi ya nane
alitumia saa 2:18.16 na kujipatia sh laki mbili, wakati nafasi ya tisa
ilishikwa na Eric Christopher (Kenya), aliyejipatia Sh laki moja na nusu huku nafasi ya kumi ikienda kwa Antony Mugo (Kenya),aliyetumia saa 2:18.29. Kwa
upande wa Full Marathon Wanaume, mshindi alikua Edna Joseph (Kenya),
aliyetumia saa 2:39.5, huku mshindi wa pili akiwa Eunice Muchiri,
aliyetumia saa 2:41.00, wakati nafasi ya tatu ilishikwa na Fridah
Too (Kenya), aliyetumia saa 2:44.04, huku nafasi ya nne ilishikwa na
Rosnline Daud (Kenya), aliyetumia saa 2:45.01, huku nafasi ya tano
ikienda kwa Jane Kangora (Kenya), aliyetumia
saa 2:46.06, huku nafasi ya sita ikienda kwa Gladus Otero (Kenya),
aliyetumia saa2:47.54, huku nafasi ya saba ikichukuliwa na Lilian
Cheplimo (Kenya), aliyetumia saa 2:49.09, wakati nafasi ya nane
ilikwenda kwa Rosina Kibona (Kenya), aliyetumia saa 2:49.25, huku
Seoflesina Sumawe (Tanzania0, akishika nafasi ya tisa kwa kutumia saa
2:50.11 na Eunice Korir (Kenya), akishika nafsi ya kumi kwa kutumia saa
2:52.21. Hata hivyo wanariadha hao, watapatiwa zawadi zao baada ya
kupimwa, mkojo ili kujirithisha kama hawajatumia dawa za kuongeza nguvu. Akizungumza
katika tukio hilo, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk.
Fenela Mukangara, alisema riadha ni mojawapo ya michezo inayoheshimika sana duniani. "Niwakumbushe
kuwa, mataifa ya Kiafrika ndiyo yamekuwa kinara wa kuzalisha wanariadha
mashuhuri, nawaasa viongozi wa riadha Tanzania, kuandaa mikakati shirikishi ya kukuza riadha na kuitekeleza ili nchi yetu iendelee kung’ara
katika anga za kimataifa, kwa upande wa wanariadha, nawasihi
muendelee kujituma kwa kuwasikiliza makocha na viongozi wenu ili muweze
kufanikiwa kuwa na viwango vitakavyowawezesha kuwa na ushindani wa Kimataifa," alisema. Mbio hizo zinaratibiwa na Executive Solutions na kudhaminiwa na Kilimanjaro PremiumLager, huku wadhamini wengine wa tukio hilo
ni
pamoja na Vodacom Tanzania (5km Fun Run), GAPCO (Nusu Marathon
Walemavu), Tanga Cement, CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, New Arusha Hoteli, Kilimanjaro Water, FastJet na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA). |
No comments:
Post a Comment