Maafande wa jeshi la
kujenga taifa, Ruvu Shooting ya mkoani Pwani wametamba kuwamaliza Azam Fc,
Lambalamba katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara unaotarajiwa kupigwa uwanja
wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani jumamosi ya wiki hii.
Ruvu Shooting wenye pointi 29 ,nafasi ya saba ya msimamo watashuka katika dimba lao la nyumbani kusaka ushindi ili kumaliza msimu huu wa ligi wakiwa nafasi nne za juu.
Ruvu Shooting wenye pointi 29 ,nafasi ya saba ya msimamo watashuka katika dimba lao la nyumbani kusaka ushindi ili kumaliza msimu huu wa ligi wakiwa nafasi nne za juu.
Akizungumza na mtandao huu, Afisa habari wa Ruvu shooting, Masau Bwire, amesema kuwa maandalizi ya mchezo huo yanakwenda barabara huku kocha mkuu wa klabu hiyo Charles Boniface Mkwasa “Master” akirekebisha makosa yaliyojitokeza mechi iliyopita ambayo walifungwa 1-0 na vinara wa ligi hiyo, klabu ya Yanga.
Masau alisema Azam fc
jana walishinda 3-0 dhidi ya wapiga kwata wenzao wa Tanzania Prisons hali
ambayo imewapa nguvu kubwa ya kuwania ubingwa, lakini mchezo wao wa Jumamosi
wasitarajie urahisi hata kidogo.
“Wapinzani wetu
wamefanya vizuri kombe la shirikisho kwa kuwafunga Barrack Young Controller II
mabo 2-1 ugenini, jana wamepata matokeo mazuri mbele ya Prisons na wanazidi
kuamsha mizimu ya kuusaka ubingwa, sisi tunahitaji nafasi ya kushiriki hata
Tusker cup mwaka huu, hatukubali kufungwa”. Masau alitamba.
Afisa habari huyo
ameongeza kuwa mchezo uliopita dhidi ya Yanga ambao walipoteza, walistahili
kushinda kutokana na kiwango cha vijana wao, lakini walikosa nafasi nzuri za
kufunga na wapinzani wao walipata nafasi moja waliyoitumia kupata ushindi.
Masau alisema Mkwasa
anaendelea kunoa makali ya washambuliaji wake wakiwemo Hassan Dilunga, Said
Dilunga, Ernest Ernest, Ayubu kitala ili kuibuka wababe katika mchezo huo wa
kukata na shoka.
“Watanzania wanawajua
vizuri Ruvu shooting, moto tunaowasha si mchezo, tutawapiga Azam fc na baada ya
hapo tutaanza hesabu za kuwavaa Polisi Morogoro wiki ijayo”. Masu aliongeza.
Akizungumzia malengo
yao kwa sasa, msemaje huyo amesema wapo nafasi ya saba na ponti 27 huku wakiwa
na michezo saba kibindoni, hali hii inawapa matumaini ya kufanya vizuri na
kushika hata nafasi ya nne ili kucheza kwa mara ya kwanza michuano ya kimataifa
yaani kombe la Tusker linaloshirikisha klabu za afrika mashariki.
Kwa upande wa Azam fc
kupitia kwa afisa habari wao Jaffar Idd Maganga wamesema kuwa mchezo huo utakuwa mgumu sana kwao na wanauchukulia
kwa umakini mkubwa sana ili kupata pointi tatu na kuendeleza harakati zao za
kuwania ubingwa.
Pia alisema mchezo
huo wataumia kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano wa kombe la
shirikisho dhidi ya Waliberia, Barrack Fc machi 9 mwaka huu dimba la taifa
jijini Dar es salaam.
“Sisi kila mchezo
kwetu ni fainali, katu hatudharau timu yoyote ya ligi kuu, tuna safari ndefu na
tunakabiliwa na michuano ya kimataifa, lakini tunafanya jitihada kubwa
kujiandaa kwa ajili ya mashindano yote, na jumamosi tutashinda kama jana”. Idd
alisema.
Azam fc wapo nafasi
ya pili katika msimamo wa ligi kuu wakiwa na pointi 40 huku Yanga wakiwa
kileleni na pointi 48. Mabingwa watetezi simba wanabakia nafasi ya tatu na
pointi 34 baada ya kupoteza 1-0 mchezo
wa jana dhidi ya Kagera sugar.
Ligi kuu kwa sasa
imejigawa katika makundi matatu, kundi la kwanza ni timu zinazowania ubingwa wa
ligi kuu kwa maana ya Yanga, Simba na Azam fc, kundi la pili ni zle zinazowania
nafasi mojawapo za juu, Mtibwa Sugar, Coastal union, kagera sugar, JKT Oljoro,
Ruvu shooting na kundi la mwisho ni zile zinazowania kukwepa mkasi wa kushuka
daraja, JKT Ruvu, Tanzania Prisons, Toto Africans, African Lyon.
RATIBA: Jumamosi Machi 30
JKT OLJORO v JKT RUVU [SH. AMRI ABEID,
ARUSHA]
RUVU SHOOTINGS v AZAM FC [MABATINI, PWANI]
AFRICAN LYON FC v COASTAL UNION [AZAM
COMPLEX, KAGERA]
POLISI MOROGORO v YOUNG AFRICANS [JAMHURI,
MOROGORO]
KAGERA SUGAR v MTIBWA SUGAR FC [KAITABA,
KAGERA]
TOTO AFRICANS v SIMBA SC [CCM KIRUMBA,
MWANZA]
MSIMAMO:
NA
|
TIMU
|
P
|
W
|
D
|
L
|
GD
|
PTS
|
1
|
YANGA
|
20
|
15
|
3
|
2
|
25
|
48
|
2
|
AZAM FC
|
20
|
12
|
4
|
4
|
19
|
40
|
3
|
SIMBA
|
20
|
9
|
7
|
4
|
11
|
34
|
4
|
KAGERA
|
21
|
9
|
7
|
5
|
5
|
34
|
5
|
COASTAL
|
21
|
8
|
8
|
5
|
4
|
32
|
6
|
MTIBWA
|
21
|
8
|
8
|
5
|
4
|
32
|
7
|
RUVU SHOOTING
|
19
|
8
|
5
|
6
|
3
|
29
|
8
|
JKT OLJORO
|
21
|
6
|
7
|
8
|
-3
|
25
|
9
|
MGAMBO
|
21
|
7
|
3
|
11
|
-6
|
24
|
10
|
PRISONS
|
21
|
4
|
8
|
9
|
-9
|
20
|
11
|
JKT RUVU
|
18
|
5
|
4
|
9
|
-12
|
19
|
12
|
POLISI
|
21
|
3
|
8
|
10
|
-10
|
17
|
13
|
TOTO
|
21
|
3
|
8
|
10
|
-12
|
17
|
14
|
LYON
|
21
|
4
|
4
|
13
|
-18
|
16
|
Kwa namana msimamo huu ulivyo nina maoni yafuatayo;
ReplyDelete1.Yanga ina wastani wa kupata pointi 2.40 kwa kila mechi moja inayocheza,Azam pointi2.00 na Simba pointi 1.70
2.Kwa misimu mitatu mfululizo iliyopita Yanga haikuwahi kuvuka pointi 50 lakini kwa hali ilvyo msimu huu watavuka mapema pointi hizo
3.Kuanzia timu ya 7-14 goal difference yao ni hasi au minus hali inayoonyesha tofauti kubwa ya kiuwezo kati ya timu 7 za juu na timu 7 za chini.
3.Yanga ina wastani wa kushinda mechi 3 katika kila mechi 4 inazocheza.Azam ina wastani wa kushinda mechi 3 katika kila mechi 5 wanazocheza.Simba ina wastani wa kushinda mechi 2 katika kila mechi 4 inazocheza.
4.Hivi sasa timu hizi tatu zimebakiza mechi sita kila moja.Yanga ikishinda mechi zote "point ceiling" yake ni pointi 66,Azam 58 na Simba 52.Kumbukan katika mechi zilizobaki Yanga ina mechi moja na Simba na pia Azam ina mechi moja na Simba na hivyo matokeo ya mechi hizi yanaweza kubabadili "point ceiling" baina ya timu hizi tatu.