Search This Blog

Friday, March 29, 2013

HAZARD, DEMBELE, FELLAINI, KOMPANY, NA MASTAA WENGINE WATAISHANGAZA DUNIA WAKIFUZU KWENDA BRAZIL 2014


Kuna miezi 14 imebaki mpaka kuanza kwa kombe la dunia nchini Brazil na kutoka kwenye matokeo ya michezo ya kufuzu mpaka sasa, tunaweza kutabiri timu mbili za juu kutoka kwenye kila kundi la brani ulaya. 
Katika kila msimu wa kombe la dunia, kumekuwa kukiwepo na timu ambazo hazipewi nafasi kabla ya mashindano ambazo huja kufanya vizuri. Uruguay ilisafiri kwenda South Africa wakiwa kama underdog mwaka 2010 lakini uwezo walionyesha uliwashangaza wengi. Wakiwa kwenye kiwango bora kabisa katika hatua za mwanzo, na hatimaye wakaishi mikononi wa Uholanzi kwenye nusu fainali.

Swali la kawaida ambalo lnaulizwa ni timugani isiyopewa nafasi itakayowasumbua vigogo katika kombe la dunia lijalo. Kuna timu nyingi kama vile Colombia, mabingwa wa AFCON Nigeria, labda Japan, lakini timu ambayo inaaminika italeta usumbufu mkubwa bila shaka ni Ubelgiji. 

Mapinduzi ya kizazi cha dhahabu cha soka la Ubelgiji:
Kizazi cha soka cha sasa cha Ubelgiji kinatajwa kutokea kwenye kipindi hiki wakiwa na lundo la wachezaji wenye vipaji vikubwa kwenye nafasi zote dimbani. Ukiacha wachezaji wanaoanza kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya taifa, walio benchi karibia wote wanatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya £10M. Rekodi yao kwenye cha hivi karibuni ni nzuri na kuvutia mno. Uimara wa timu yao upo kwenye maeneo yote muhimu. 



Kwenye ulinzi:
Wanaonza: Jan Vertonghen, Daniel Van Buyten, Vincent Kompany/ Thomas Vermaelen, Guillaume Gillet.

Tangu ahame kutoka Ajax kwenda Spurs kipindi cha kiangazi kilichopita, nafasi ya Jan Vertonghen katika kikosi cha kwanza imekuwa sio swali. Akiwa na uwezo wa kucheza kama beki wa kati pamoja na nafasi ya kushoto, Vertonghen amecheza part kubwa sana katika ukuta wa Spurs msimu huu. Uwezo halisi wa  Vertonghen uliwekewa kizuizi kwa majukumu ya ulinzi tu lakini ana uwezo mkubwa wa kushambulia na kufunga pamoja na kutengeneza nafasi kwa wenzie, angalia uwezo alionesha kwenye mechi dhidi ya Liverpool na Manchester United akifunga mabao muhimu.

Ukuta wa UBelgiji pia unaundwa na mchezaji mwengine kiraka aitwaye Guillaume Gillet. Mchezaji mwenye umri wa miaka 28 ambaye ana uwezo wa kucheza kama kiungo wa kati pia beki wa kulia, akicheza kwa kiwango kikubwa kwenye sehemu zote hizo. Goli lake dhidi ya Croatia katika mechi za kufuzu kombe la dunia, mwezi wa tisa mwaka jana, mchezo ulioisha kwa matokeo ya 1-1 lilionyesha ana msaada gani kwa timu yake. 


Nafasi ya ulinzi ya kati ya Ubelgiji inaonekana kuwa imara anapocheza Van Buyten na Kompany katikati. Van Buyten amekuwa na wakati mzuri na Bayern Munich msimu huu, akicheza karibia kila mchezo kwa timu hiyo ya Ujerumani. Ameweza kuuleta ushirikiano wake na Dante kwa Kompany. Uelewano uliopo baina ya wawili hawa ni mzuri sana. Komapny, ambaye alishinda taji na City msimu uliopita ana uwezo wa kucheza kwa kiwango cha juu sana, uelewano wao na Buyten unafananishwa na Maldini-Nesta Partnership.

 
Nafasi ya kiungo:
Waanzaji: Mousa Dembele, Kevin Mirallas, Eden Hazard, Marouane Fellaini, Axel Witsel.

Jukumu alilopewa Mousa Dembele ndani ya Spurs ni tofauti na alilokuwa nalo Fulham. Martin Jol alimchezesha Dembele kama mchezeshaji wakati akiwa Fulham, wakati Villas boas amempa majukumu ya kiungo wa ulinzi. Kiwango cha Dembele kama kiungo mchezeshaji kilikuwa kizuri sana lakini majukumu mapya ya kiungo mkabaji yamezidi kumkamilisha Dembele, na ushirikiano wake aliounda na Scot Parker umekuwa na mafanikio sana kwenye kikosi cha Spurs. Namna anavyoutumia mwili wake na uwezo anakuwa kiungo mzuri sana wa ukabaji. 

Wakati tunajadili kuhusu kiungo wa aina ya When we discuss about box-to-box kwenye soka la kisasa, tunaweza tukamuweka mtu kama Artuto Vidal, Yaya Toure na listi haitokamilika kama tutashindwa kumuweka,  Marouane Fellaini. Kiungo mwenye miaka  25 anayeichezea, amekuwa tishio kubwa sana kwenye ligi kuu ya England, anaweza akasababisha hatari kwenye eneo lolote dimbani. Stamina alionayo, kasi, uwezo wa kupiga mipira mirefu imemfanya thamaniyake ipande mpaka kuwa £25M.
Kevin Mirallas ni tunda jingine linalopikwa pale Merseyside, kiungo ambaye ana uwezo wa kuchachafya ngome za wapinzani akitokea pembeni. Akicheza upande wa kushoto, Mirallas amekuwa na uelewano mkubwa na Fellaini, wakicheza wote kwenye klabu moja, uelewano wao unaleta taabu sana kwa wapinzani wao.

Manchester City, Manchester United na Chelsea walikuwa ladhi kulipa zaidi ya £30M kwa kiungo wa Lille, Eden Hazard mwaka jana. Baada ya tetesi za muda mrefu Hazard akaamua kujiunga na Chelsea kwa ada ya uhamisho wa £32.5M. Alipowasili  Stamford Bridge, Hazard alionyesha kiwango kizuri na kuleta mabadiliko ndani ya timu chini ya kocha aliyetimuliwa Roberto Di Matteo. Jukumu la Hazard kwenye kikosi cha sasa cha Chelsea ni muhimu sana, hasa kwenye siku za hivi karibuni ameonyesha kiwango kizuri, akiisadiai timu yake kuendelea kuwa ndani ya FA Cup akifunga goli la kusawazisha dhidi ya Man United wiki mbili zilizopita pale Old Trafford.
Bado wana kiungo mwingine mwenye thamani ya £32.5M, anayeichezea klabu ya Russia Zenit, Axel Witsel. Zenit walilipa fedha nyingi sana kwa Benfica ili kumsajili Witsel, ingawa bado hajaonekana kuwa muhimu sana nchini Russia, bado anahesabika kama mmoja ya viungo bora barani ulaya wenye uwezo wa kubadilisha matokeo muda wowote dimbani. Timu kubwa barani ulaya zimeonyesha zipo tayari kulipa kiasi kisichopungua £25M kumtoa mbelgiji huyo kutoka Russia.


Ushambuliaji:
Muanzaji: Christian Benteke.
Ukiachana na Christian Benteke, Romelu Lukaku ni mshambuliaji mwingine ambaye anaweza akaanza kwenye kikosi cha kwanza, lakini kutokana uwezo mkubwa umaliziaji Benteke anaaza mbele ya kinda la Chelsea, kocha Wilmots amekuwa anapenda kumuanzisha mshambuliaji wa Aston Villa siku za hivi karibuni.

World Cup 2014:
Belgium kwa sasa ndio wanashika nafasi ya pili katika kundi A kuwania kufuzu kwenda Brazili, wakiwa na pointi 13 kwenye mechi tano walizocheza, wakiwa nyuma ya Croatia waliowazidi kwa tofauti ya mabao.
 Ukiangalia ubora wa kikosi chao cha sasa, inategemewa kwamba  Belgium wanaweza kufuzu kwenda Brazil. Ikiwa watafuzu, wakaenda na kufanya vizuri hata kufikia hatua ya nusu fainali haitowashangaza wengi kama ilivyotokea kwa Uruguay, South Korea au Turkey miaka nyuma, kutokana na ubora wa wachezaji waliojazana kwenye kikosi chao.

3 comments:

  1. BELGIUM WANAONGOZA KUNDI KWA TOFAUTI YA MAGOLI MATATU.

    BELGIUM: GD 10

    CROATIA: GD 7

    ReplyDelete
  2. ni kweli shaffiah watatisha sana hawa jamaa

    ReplyDelete
  3. Kwa wachezaji hao hata mi naumga mkono hii itakuwa timu yenye kuleta changamoto kubwa! tuwaombee tu wafuzu tupate uhondo!NURU SPORTS MSM

    ReplyDelete