KOCHA wa Simba, Patrick Liewig ametoa onyo kali kwa nyota wake kwa kusema hakuna mchezaji anayeweza kuwa juu ya timu hiyo.
Kauli
hiyo imekuja, baada ya hali ya nidhamu kwa wachezaji wa Simba kuwa
mbovu na kuchangia timu hiyo kupata matokeo mabaya kwenye ligi.
Mfaransa huyo alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa tatizo hilo ameona zaidi kwa wachezaji 'mafaza'
Hali ambayo imemlazimu kutumia wachezaji watano hadi sita vijana kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
"Nafikiri kama nidhamu itakuwa mbovu kwenye timu. Kamwe hatuwezi kufikia malengo ambayo tumejiwekea."
"Kwa hiyo ni sahihi kwangu kwenda na wachezaji ambao wananielewa ambacho wanatuma kukifanya uwanjani."
"Hakuna mchezaji anayeweza kuwa juu ya timu." alisema kocha huyo aliyerithi mikoba ya Mserbia Milovan Cirkovic.
Pia, alisema amefundisha soka katika klabu tofauti barani
Afrika, lakini anashangazwa na jinsi wachezaji wa timu yake wanavyoendesha maisha yao ya soka.
"Kwa ninavyoelewa mchezaji anatakiwa kujitambua na kuipenda kazi yake. Lakini ninachokiona hapa ni tofauti kabisa."
"Pia, timu kuwa nzuri ni lazima wachezaji wawe na nidhamu na ushirikiano wa pamoja bila kubaguana."
Hata hivyo, kocha huyo amewapumzisha nyota kadhaa wa timu hiyo kutokana na kutoridhishwa na viwango vyao pamoja na nidhamu.
Pia, Mfaransa huyo ameahidi kuendelea kuwatumia wachezaji vijana katika mechi zilizobaki kwenye ligi.
Bila NIDHAMU huwezi kufanikiwa jambo lolote lile.
ReplyDeleteNi vyema kocha amelitambua hilo na atekeleze hayo bila ya kuingiliwa na mtu yeyote yule,mafanikio yatapatikana.
safiiii sn kaza butiiii hivyooo hivyooooo kochaaaaaaaa hakunaaaa kulegezaaaa hapoooo,,,,we panga vijanaaa wachezeee nasi 2takujaaaa uwanjani kukuusaport,,hao mafaza waende Yanga hukoooooo,,,,,,sisi 2nawataka vijanaaaa plzzzz wanasimba wenzanguuu 2muunge mkonooo kocha kwa maamuzi yake magumu,,hata hao mafaza wameifanyiaa nini Simbaaa,,,?,ss ni zamu ya vijanaaa mafaza 2pa kule.na nyie viongoziii mwachieni kocha afanye kile anachoona kinafaa kazi yenu ni kumtengenezeaaa mazingira mazuri kocha na vijanaa wake Simba itakucha 2 kupitiaaa vijanaaaaaaaa
ReplyDeleteUkweli upo wazi! Maisha ya wachezaji wa tanzania hawafuati miiko na kanuni! Wakisifiwa tu basi vichwa hivyo!!angalia wanavyochoka mapema! Umri mdogo wapo kama wazee! Nenda kenya kule!wapo na umri mkubwa na wanapiga soka! Jamani badilikeni na mkubali ukweli acheni ujinga na wapenzi achani kukumbatia mafaza wakati hawana nidhamu.lewig kp it up jenga timu iwe bora na yenye nidhamu.
ReplyDelete