Search This Blog

Friday, March 15, 2013

BEKI WA YANGA NA UVIMBE WA SHAVU ALIODUMU NAO TANGU UTOTONI - AFANYIWA UPASUAJI SASA SAFI

Mbogo mwenye uvimbe
BEKI wa Yanga, Ladislaus Mbogo ameeleza kufurahi kuondokana na hali ambao ilikuwa ikimfanya kujihisi tofauti na wengine.
Mbogo alifanyiwa upasuaji kwenye uvimbe wa shavu la kushoto, Jumatano iliyopita katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Beki huyo aliyejiunga na Yanga msimu huu akitokea Toto African ya Mwanza alisema;
"Furaha yangu kubwa ni kuondokana na hali ambayo nimekuwa nayo tangu utotoni wangu."
"Pia, ushirikiano ambao nimeupata kutoka kwa wachezaji wenzangu na viongozi wa timu yangu."
Mbogo alisema; "Hali ya uvimbe ilikuwa ikinifanya nijione tofauti na wengine na kunikosesha raha."
"Kubwa ambalo siwezi kulisahau ni shukrani zangu za dhati kwa uongozi wa Yanga kunitibu."
"Nadhani ni jambo la kuigwa na wengine kuwa na moyo wa kusaidia. Nimecheza Kagera na Toto African lakini hawakuweza kunitibu." alisema mlinzi huyo wa kati.
Kuanza mazoezi, Mbogo alisema amepewa wiki mbili ikiwa moja ya kutolewa nyuzi na nyingine kufuatiia hali ya jeraha hilo la upasuaji.
"Daktari amesema kwa sasa hawezi kuniambia siku wala tarehe ya kuanza mazoezi isipokuwa nimepewa wiki mbili kupewa jibu sahihi."
"Wiki moja itakuwa yakutoa nyuzi na nyingine atafuatilia hali yangu kujua kama nitakuwa tayari kuanza mazoezi mepesi." alisema Mbogo.

5 comments:

  1. Big up kwa uongozi.MNAJALI nguvu kazi yenu.Kijana amekuwa motivated sana na sana.akipona apewe mechi acheze ili muone alivyokuwa inspired na timu.

    ReplyDelete
  2. hayo ndiyo mambo ya kujadiliwa na wanamichezo jinsi gani timu inajali afya za wachezaji wake

    ReplyDelete
  3. inapendeza kwa upendo wa kweli kama huo pamoja na kuishabikia simba lakn natoa big-up kwa uongozi wa jangwani ktk hili.

    ReplyDelete
  4. PETER MASHOSHO NG'OLLAHMarch 17, 2013 at 8:37 PM

    kazi nzuri viongozi wetu wa Yanga mliyofanya kwa Mbogo klabu nyingine igeni mfano huo by Peter Mashosho Ng'ollah CUHAS-BUGANDO MWANZA

    ReplyDelete
  5. Toto la home hilo mitaa ya Kirumba, Mbogo Mnyama get well soon my little brother nimekuona toka mtoto viwanja vya magomeni kirumba unasukuma ndinga pamoja na hali uliokuwa nayo, you have a big heart Brother Mungu akuzidishie.

    ReplyDelete