Search This Blog

Thursday, March 7, 2013

ITS OFFICIAL KABURU AJIUZULU UMAKAMU UENYEKITI SIMBA SC - HANS POPE NAE ABWAGA MANYANGA


Hatimaye makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba Godfrey Nyange Kaburu ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake kwenye klabu ya Simba mapema leo.

Taarifa rasmi kutoka kwenye uongozi wa Simba ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba Kaburu leo ametuma barua pepe kwenda kwa mwenyekiti wa klabu ya Simba Mh.Aden Rage akimuelezea maamuzi yake ya kujivua madaraka ya kuitumikia Simba kutokana mgawanyiko mkubwa uliopo kwenye uongozi wa klabu hiyo.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari Kaburu ameelezea kwamba kamati ya utendaji imegawanyika na ufa uliopo hautoi nafasi nzuri kwake kuitumikia vizuri Simba, akisema ni moja ya sababu ya timu yao ya Simba kutofanya vizuri katika michuano mbalimbali inayoshiriki.

Pia Kaburu amesema amechukua maamuzi hayo ni njia mojawapo ya kuwajibika kama kiongozi kutokana mambo kutokwenda vizuri hali ambayo imesabababisha kutukanwa na kupigiwa kelele nyingi na wanachama na wapenzi wa Simba SC Mwenyekiti. Hivyo ameamua kujiuzulu kupisha wanachama wengine wa Simba waweze kuliongoza jahazi la klabu hiyo.


Katika hatua nyingine mwenyekti wa kamati ya usajili na mjumbe ya kamati ya utendaji Zacharia Hans Pope nae ametangaza kujiuzulu kwenye nafasi zote alizokuwa akishikilia Simba.

Pia kwenye taarifa yake ya kujiuzulu Pope amesema mgawanyiko uliopo kwenye uongozi ndio chanzo cha kujiuzulu kwake katika kuitumikia Simba kupitia nafasi za uongozi alizokuwa nazo kwa takribani miaka 3.

12 comments:

  1. Bado RAGE.Ikiwezekana atume barua yake tokea huko huko INDIA au akishuka pale JNIA.

    ReplyDelete
  2. Kwakweli m2 kama kaburu ndy alikuwa tatizo simba coz alikuwa anaingilia majukumu ya mwalimu kwnz amechelewa kujiuzuru!

    ReplyDelete
  3. sio kuingilia tu mambo ya simba pia alikua na malengo ya kujinufaisha yeye angalia kamsajili samata alipouzwa kwenda mazembe akataka pesa ya samata apewe yeye aliponyimwa kwa hasira akamuuza yondan yanga kama malipizi haijaishia hapo hata hii hela ya okwi kunafungu lake ndio maana ukifikria Sana kaburu alikuja simba kibiashara zaidi akawa ananunua wachezaji ili aje awauze kwa gharama kubwa ili mpira wetu uendelee watu aina ya kaburu hawatakiwi

    ReplyDelete
    Replies
    1. jamani hayo ni matatizo ya wanaojiita wanachama wote, maana wanajazana kwenye vikao kushabikia watu na sio kuongea mambo ya msingi ya klabu, leo tunaongelea kaburu kanunua mchezaji, na sio klabu imenunua mchezaji, mi naona kama kweli kaburu katoa hela yake unategemea nini? muuze halafu mchukue hela nyinyi? haiwezekani hela ya watu ilitumika na ni lazimzima irudi. leo nimesikia timu anapewa malkia wa nyuki, yale yale mambo ya kizamani, huu ni ujinga sana, hizi klabu tajiri jamani, mishahara na fedha za uendeshaji ikiwemo safari zinalipwa nawadhamini wakubwa wawili yaan voda na kilimanjaro, kila wiki hizi timu zinacheza na zinaingiza minimum 20m zinaingia hapo bado hatujatumia oppotunities nyingi ambazo zilizopo kwa klabu hizi, jamani tuache kutumia mifuko ya watu, haiwezekani kaburu akawa na hela kuliko simba. simba badilikeni, igeni kidogo yanga ya sasa

      Delete
  4. Huo ndo uwajibikaji.

    ReplyDelete
  5. Safi sana..rage nae ajiuzulu.
    Timu ikabidhiwe kwa akina Evans Aveva, magori, Kassim Dewji ili isukwe upya kwa ajili ya msimu Mpya. Kuna dalili METL itarudisha udhamini....

    ReplyDelete
  6. Kaburu alikuwa anangoja pesa za Okwi kwanza azitafune halafu ndo ajiuzulu??????

    ReplyDelete
  7. nampa pole sana kaburu, huyu jamaa kajitolea sana kuitumikia simba, ila nilijua hawezi fanikiwa tena baada ya kugombea maana alikuwa mtu muhimu sana alipokuwa nje ya uongozi, bahati mbaya alikuwa na rage ambaye anafikri mpaka leo mpira ule ule wa fitna na kudanganya watu ili usurvive. mimi ni mshabiki wa yanga ila namuomba sana nyange assikimbie kabisa simba maana yanga inahitaji changamoto zake. tujifunze kwa viongozi wa sasa wa yanga haitakuwa mbaya hata kama ni wa wapinzani wenu. najua simba mtatuletea viongozi makini ili kuendeleza soka. tunaweza

    ReplyDelete
  8. Mimi nahisi Mh. Rage ameziba maslahi ya hawa watu wajanja. Kwakuwa wao wanapenda kunufaika sana na Rage amestukia hili dili. Japo hawasemi ila fedha za Okwi zitakuwa tatizo.

    Siku zote tuogope watu wanaotoa fedha zao mfukoni kwa ajili ya kusajili wachezaji. Lazima tujiulize watarudishiwaje hela zao? Je riba ni kiasi gani? haiingii akilini mtu atoe kiasi kikubwa kwa ajili ya kumsajili mchezaji eti kwa mapenzi tu ya timu tu hivi hivi. Watu hao ni wachache sana. Hivi hizo hela zao wao wanaokota? Wanatoa jasho kuzipata hivyo kwenye Simba kwa kiasi kikubwa ni biashara ya wanaosajili na kutumia fedha za wadhamini. HAPA NAONA RAGE KAWADHIBITI KWA SABABU HIYO WANAFANYA NJAMA KUIHUJUMU TIMU KWA KUWA WAO NDIO WALIWASAJILI WACHEZAJI, SASA PALE RAGE ANAPOZUIA FEDHA ZA UUZWAJI WA OKWI JAMAA HAWAFURAHII WATAMPIGA MAJUNGU SANA TENA SANA. YULE JAMAA ANA ELEMENT (CHEMBE CHEMBE) ZA UADILIFU. KWA SIMBA NA YANGA HIYO NI SUMU.

    FUJO HAITAISHA USIJE SHANGAA YANGA INAIFUNGA SIMBA MABAO MATANO KWA HUJUMA ZA SIMBA HAWA HAWA.

    ReplyDelete
  9. kuna watu wako mbali sana na Simba wanaongea utumbo.uvumi wa vijiweni hauna maana.
    Mimi kama mchezaji<nawaambia wana Simba<Rage hajawahi kutoa msaada wowote,mnazidi kuleta matatizo.Muulize Rage hata mazoezi tunafanyia wapi kama atakujibu

    ReplyDelete
  10. Huo ndio uwajibikaji nivizur wakae pembeni wapishe wengine uwezo wao ndio umefikia pale so bwna kaburu yapo mengi mazur umeyfny lakini kwa maamuz uliofikia nakupongeza sana upshe watu wengine wenye mtazamo na fikra mpya wakusukuma club yetu mbele pasipo kuwa na mgawanyiko wa wapenzi na wanachama wa simba.

    ReplyDelete