BEKI wa Yanga, Ladisalus Mbogo anatarajia kufanyiwa upasuaji Machi 12, mwaka huu katika hospitali ya Mwananyamala.
Kwa
mujibu wa daktari wa timu hiyo, Nassor Matuzya alisema jana jijini Dar
es Salaam kuwa beki hiyo atafanyiwa upasuaji huo kuondoa uvimbe kwenye
shavu lake la kushoto.
“Upasuaji wake utafanyika kwenye hospitali ya Mwananyamala, Jumanne ya wiki ijayo."
Matuzya alisema; "Vipimo vyake alivyofanyiwa katika hospitali ya Muhimbili na madaktari bingwa vimetoka."
"Tuliamua kushirikiana na madaktari wa Muhimbili ili kujiridhisha zaidi kama hapatakuwa na madhara, baada ya kumpasua."
Alisema; “Upasuaji huu umekuja baada ya Mbogo kutueleza kuwa hafurahishwi na hali ya tatizo hilo,”
Mbogo
ambaye alijiunga na Yanga msimu huu akitokea Toto African ya Mwanza
alisema; "Hali hii nimekuwa nayo tangu utoto wangu. Nitashukuru endapo
upasuaji
utakwenda vizuri na kupona."
Pia, aliwashukuru viongozi wa Yanga kumsaidia kutibu tatizo lake bila kusukumwa.
"Nafikiri
tatizo hili nimekuwa nalo muda mrefu. Sina budi kuwashukuru viongozi
wangu kujitolea kunitibu. Nadhani ni jambo zuri na la kuigwa katika
jamii." alisema beki huyo aliyeichezea Yanga kwa dakika 19 kwenye
michuano ya Kombe la Kagame mwaka jana.
No comments:
Post a Comment