Wakati wa mechi zao nne za nyumbani zilizobakia, ikiwemo mechi yao dhidi ya mahasimu wao Man City na Chelsea, Man United wataonyesha moviez ya kutoka Hollywood kwenye screen kubwa kwenye dimba la Old Trafford. Klabu hiyo imesema lengo ni kuwapa burudani zaidi wanunuzi wa tiketihuku wakielekea kushinda taji lao 20 ikiwa watashinda mechi nne au tano zijazo za ligi.
"Tuna furaha sana kuwepo kwenye nafasi tuliyopo kwenye ligi," manager wa Man United aliwaambia waandishi wa habari wakati akitangaza uamuzi huo. "Huwezi kuchoka kushinda ligi, lakini suala la kushinda ligi mapema kukiwa kumebakiwa na mechi nyingi, mashabiki wanaweza wakapoteza hamu ya kwenda uwanjani kwa kiasi fulani. Hivyo tumeamua kuanza filamu ili kuzidi kuwaburudisha mashabiki. Nadhani wakati wa mechi na Man City tutakuwa tukionyesha filamu iitwayo You Got Served, then kwenye mechi ya Aston Villa tutaonyesha Apocalypse Now, na Chelsea tutaonyesha Run Fatboy Run na dhidi ya Swansea itakuwepo filamu ya The Silence of the Lambs."
Msimu uliopita, Man United walipoteza taji kwa Man City kwenye dakika ya mwisho ya msimu. Ingawa Red Devils wanaonekana kuwa vizuri tofauti na msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment