Search This Blog

Wednesday, March 20, 2013

HATIMAYE SERIKALI NA TFF ZAFIKIA MUAFAKA KUHUSU UCHAGUZI MKUU

Serikali imekubali mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uendelee kwa sharti la kuhakikisha haki inatendeka kwa wagombea waliofika mbele ya Kamati ya Rufani ya Uchaguzi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mchana, Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao kati ya uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo chini ya Waziri Dk. Fenella Mukangara, TFF na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Amesema baada ya maafikiano hayo, TFF italiandikia barua Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo ndilo lililosimamisha mchakato huo ili litume ujumbe wake kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya wagombea walioenguliwa.

Rais Tenga ambaye ameishukuru Serikali kwa kuruhusu mchakato huo uendelee, pia ameahidi kuwa uchaguzi wa TFF utafanyika kabla ya Mei 25 mwaka huu kama walivyokubaliana na Serikali, na kuwa haki si tu itatendeka bali ionekane imetendeka.

“Serikali imetuelekeza uchaguzi ufanyike kabla ya Mei 25. Tumewaambia kwetu huko ni mbali. FIFA wakija hata kesho wakituambia endeleeni sisi tuko tayari. Hesabu zetu ziko tayari, makabrasha yote yako tayari yanasubiri mkutano tu. Labda itakuwa kutoa muda tu kwa wajumbe walioko mbali waweze kujiandaa, maana wajumbe huwezi kuwaita ghafla,” amesema.

Amesisitiza kuwa TFF ilishapanga tarehe ya uchaguzi, lakini ukasimamishwa na FIFA baada ya baadhi ya walioenguliwa kulalamika huko. Hivyo maneno kuwa TFF hawataki uchaguzi kwa sababu wanataka kuendelea kubaki madarakani haya maana hata kidogo.

Hivyo amewataka wagombea wote waliofika kwenye Kamati ya Rufani ya Uchaguzi na wakaendelea kujiandaa vizuri, kwani FIFA watakapofika watawasikiliza wao na vyombo vilivyowaengua.

Pia amesema TFF ina heshimu Serikali na itaendelea kufanya hivyo, lakini vilevile lazima iheshimu FIFA sababu iko kwenye mpira wa miguu, na FIFA ndiyo wasimamizi wa mchezo huo duniani.  

Amewakumbusha wanachama wa TFF, hasa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufahamu kuwa TFF ina katiba, lakini ni lazima pia wafahamu kwanini kuna FIFA.

Rais Tenga amewahadharisha watu wanaopitapita mikoani kuomba saini za wajumbe ili kuita Mkutano Mkuu wa dharura wakati wanajua mkutano ulishaitishwa, lakini ukasimamishwa na FIFA. Jambo hilo kikatiba ni kosa.

5 comments:

  1. ha ha ha, habari nzuri hiyo!!!

    ReplyDelete
  2. Mimi nilitegemea hayo ndio yatatokea, kina makala walikurupjka sana. Sasa tuache haki itendeke kama wanastahili tutaona fifa sio wahaya au wazaramo. Shaffii kwa maoni yangu kutokana na jinsi nilivyofuatilia mchakato hakuna aliyeonewa na mgombea ni mmoja kama ilivyomuliwa

    ReplyDelete
  3. TANGU MWANZO WATU WENYE UPEO TULISHAONA KWAMBA SERIKALI ILIKOSEA LAKINI WATU WENYE UPEO MDOGO WALIKUWA WAKIPINGA KWA SABABU ZA KISHABIKI NA HISIA TU,NA BAHATI MBAYA WENGI WAO WALIKUWA NI WAANDISHI WA HABARI.CHA KUSHANGAZA SERIKALI INAITAKA TFF IHAKIKISHE HAKI INATENDEKA,HII INAONYESHA KWAMBA TATIZO HAIKUWA KATIBA YA TFF BALI WAGOMBEA FULANI WALIOTEMWA.HII SIYO FAIR HATA KIDOGO,MTU ANAAMUA KUIINGIZA SERIKALI KWENYE MGOGORO WAKE BINAFSI NA TFF NA SERIKALI NAYO BILA KUJIJUA INATUMBUKIA KICHWAKICHWA.

    ReplyDelete
  4. Thanks God hili suala limefikia hapa maana Serikali kiukweli inanishangaza maana ni wazi kabisa haikutumia busara kulipalamia hili suala, mi niwapongeze viongozi wa TFF maana hata kama kuna magumashi wanafanya lakini wanajua kucheza karata zao vizuri kabisa...! Upande mwingine ni somo kwa wadau wote wa soka hasa waandishi ambao kimsimngi wananafasi kubwa kusaidia wananchi wa kawaida kuelewa mambo yanaendaje hasa linapokuja suala la Kisheria kama hili ushabiki uwekwe pembeni na kama kunakasoro basi ifafanuliwe kiuwazi na kiuharisia na si kukurupuka tu na kugeuza mambo nyeti kuwa mitaji. Naamini hapa suala si KATIBA bali ni baadhi ya watu na watu wao.

    ReplyDelete
  5. We BWEGE MWANJALA suala la Uhaya na Uzaramo linakujaje hapo?Nyie ndio miongoni mwa wale wanaofikiri kwa kutumia makalio yao kama alivyowahi kusema Mheshimiwa mmoja

    ReplyDelete