Search This Blog

Monday, March 25, 2013

EXCLUSIVE: SERIKALI KUUNDA KAMATI YA USHINDI YA STARS - YASEMA ITAENDELEA KUMLIPA KIM POULSEN

Siku moja baada ya kuiongoza timu ya Taifa ya Tanzania kuitandika Morocco 3-1 na kujiweka kwenye nafasi nzuri kwenye michuano ya kugombania nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia 2014. Leo serikali kupitia naibu waziri wa michezo na habari Mh.Amos Makalla imesema itaendelea kumlipa mshahara kocha wa timu ya taifa Kim Poulsen.

Kim Poulsen ambaye alichukua nafasi ya Jan Poulsen mwaka jana kuiongoza timu ya soka ya wakubwa ya Tanzania, amekuwa na rekodi nzuri katika kuiongoza timu ya taifa kwenye kipindi kifupi alichokaa huku timu ikionyesha mwelekeo mzuri kwa kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali inayoshiriki.

Akizungumza na mtandao huu asubuhi ya leo Mh.Amos Makalla alisema: "Naipongeza sana Taifa Stars kwa ushindi walioupata, nawapongeza wachezaji kwa kujituma muda wote hakika wameijengea heshima Tanzania nawataka waongeze bidii wasibweteke! Nampongeza kocha mkuu na benchi la ufundi kwa muda mdogo ameijenga timu vizuri na amewaelewa wachezaji vizuri. Nawashukuru watanzania kwa kujitokeza kwa wingi na kuishangilia timu yao muda wote, aidha serikali inakusudia kuunda kamati ya kusaidia Taifa Stars ili kuongeza nguvu haraka iwezekanavyo ili kuiwezesha kufanya vema katika mechi zilizobaki! Pamoja na kamati serikali itaendelea kulipa mishahara wa kocha wa timu ya taifa." - alimaliza Makalla

6 comments:

  1. HIZI KAMATI HAZISAIDII NI ULAJI WA WATU TU

    ReplyDelete
  2. Hizo kamati za kusaidia timu ishinde mimi nadhan hazina maana sana, kuna haja gani ya kamati ya kusaidia timu ishinde? Kazi ya hiyo kamati hasa ni nini? Maana ingekuwa timu haina ufadhili tungesema labda kamati hii itashughulika na kukusanya hela kwa ajili ya kambi au kulipa wachezaji posho lakini sasa TBL wanatoa hela zao hiyo kamati ni ya nini au ndo washaona mwanga kwa stars kwa hiyo wanataka wawepo watu wengine wa kusifiwa zaidi ya kocha, benchi lake la ufundi pamoja na wachezaji?

    ReplyDelete
  3. Mimi nadhani kipindi kama hiki tunahitaji tuwe na mwalimu wa saikoloji ni muhimu sana na itasaidia kuwaweka sawa wachezaji wetu wasihogope majina makubwa @ the end tunapokwenda tutatafuta sababu zingine eti tumefungwa kwasababu wenzetu wanawachezaji wakubwa wanaocheza ulaya, mwalimu wa saikoloji ni muhimu kwa kipindi hiki, na nahmini tutafika mbali tukihondoa uwoga, mpira wa majina kwa sasa africa umeshakwisha kwahiyo tusaidiane tufanye hivyo ili tuhondoe visingizio vya baadae hapo.

    ReplyDelete
  4. Hizo ni siasa tu na wanataka kumweka Jamal Malinzi kwenye hiyo kamati ili kumpigia kampeni.Halafu walikuwa wamekaa kimya sakata la mkataba wa kocha leo ndiyo anasema wataendelea kumlipa baada ya kuona stars imeshinda na sakata la katiba ya TFF limemalizika.Walikaa kimya kumfitini Tenga na NYAMLANI ionekane TFF imeshindwa kumuongezea mkataba kocha kutokana na uhusiano wake mbaya na serikali.

    ReplyDelete
  5. Kwa hyo wangefungwa mngeacha kumlipa

    ReplyDelete
  6. huyu kim poulsen tunamuhitaji kuliko yeye anavotuhitaji amejua kutengeneza patern ya team. ila wengi wetu tutamcritisize ngoja tufungwe mechi moja tu,
    hizo kamatiu zenu zisizokuwa na kichwa wala miguu hatutaki kuzisikia wacheni vijana wafanye kazi msiwalete upuuzi kama wa kulwa na doto kwenye team ya taifa

    ReplyDelete