Search This Blog

Tuesday, March 26, 2013

ERASTO NYONI: KWANINI SIKUCHEZA VIZURI DHIDI YA MOROCCO?

MLINZI Erasto Nyoni amevunja ukimya na kukiri kuwa hakuwa kwenye kiwango chake wakati Taifa Stars ilipocheza na Morocco.
Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kusaka tiketi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazopigwa, Brazil mwakani. Stars ilishinda mabao 3-1.
Kiraka huyo wa Azam FC na Taifa Stars alisema; "Kiukweli hali yangu haikuwa freshi kivile."
"Kuna wakati nilijiona mzito. Nafikiri hilo linachangiwa sana na kutoshiriki ligi."
Beki huyo alisema amekuwa akifanya mazoezi ya kujiweka fiti na timu tofauti za mchangani jijini Dar es Salaam tangu aliposimamishwa na Azam kwa tuhuma za kupokea rushwa mchezoni.
"Kuna timu ambazo nafanya nazo mazoezi. Dah! litakuwa suala gumu kidogo kuzitaja kwa muda huu."
"Nadhani kule ushindani ni mdogo ukilinganisha na ligi. Kucheza ligi kunasaidia sana kujijenga mchezaji kimashindano." alisisitiza.


6 comments:

  1. KWA UELEWA WANGU MCHEZAJI ANAITWA TIMU YA TAIFA BAADA YA KUONEKANA KATIKA MECHI ANAZOCHEZEA KLABU YAKE NA SIO MAZOEZINI.KOCHA WA TIMU YA TAIFA HAENDI KATIKA MAZOEZI YA KLABU AU TIMU ZA MCHANGANI BALI HUANGALIA KATIKA MECHI NA KUJUA KIWANGO CHA MCHEZAJI ANAYESTAHILI KUITWA TIMU YA TAIFA.KWA UPANDE WA NYONI KOCHA HAJAMUONA TANGU ALIVYOCHEZA MECHI YA STARS NA CAMERON TAREHE 7/2/2013.MECHI INAYOFUATA NI JUNI 2013,JE KOCHA ATAENDELEA KUMWITA NYONI?KWA MAONI YANGU UMEFIKA WAKATI WA KUMJARIBU MICHAEL PIUS AIDAN WA RUVU SHOOTING AU NASSORO SAIDI CHOLO KATIKA NAFASI HIYO.VINGINEVYO ANAWEZA KUMTUMIA KAPOMBE NA NAFASI YA BEKI WA KUSHOTO ACHEZE IDRISSA RASHIDI"BABA UBAYA" AU IDRISSA RAJABU

    ReplyDelete
  2. Anonymus 1: kumbuka kinachompa nafasi Nyoni katika timu ya taifa ni suala la ufundi zaidi, japo fitness inamata sana katika soka lakini Poulsen anakuwa na wakati mgumu kumpata mbadala wa Nyoni katika ligi yetu inayoendelea. ukimwangalia Nyoni umbo lake limekaa kimchezo wakati wote, ana nguvu na ana uwezo mzuri wa kuusoma uchezaji wa timu pinzani, na ni mchezaji makini muda wote awapo mchezoni. wachezaji wa aina hii huandaliwa kwa muda mrefu.

    ReplyDelete
  3. Mshaanza wabongo kujifanya much know! mara pale fulani anafaa.Tumwache kocha mtaalam profeshono anajua kila kitu kinachoendelea ndio maana tumefika hapa.Kumdunda Morocco si mchezo!! Tumpe sapoti

    ReplyDelete
  4. Haya ni maoni ambayo yanatokana na maelezo ya Nyoni mwenyewe hapo juu.Tatizo letu wabongo tunasubiri mpaka timu ifungwe ndio tuanze kukosoa.Unaposema hakuna mbadala wa Nyoni katika nafasi hiyo maana yake ni kwamba siku Nyoni akiumia itabidi nafasi hiyo ibaki wazi. Erasto mwenyewe kakiri mapungufu yake yanayotokana na kukosa match fitness.Duniani kote hakuna mchezaji wa kudumu wa timu ya Taifa bali ni yule aliye katika kiwango cha juu katika nafasi yake kwa wakati husika ndiye anayeitwa.Kwa yule aliyekuwepo uwanjani juzi hawezi kubisha kwamba Erasto alikaribia kuigharimu timu katika kipindi cha kwanza.

    ReplyDelete
  5. Tanzania angalau sasa tumeanza kuiona timu iliyokaa pamoja kwa muda mrefu na hivyo kuanza kuonyesha mwanga.Kocha huyu analijua hilo na habadilishi timu bila mpangilio.Tatizo letu sisi tunawaondoa wachezaji wetu mapema kwa kuwaondolea confidence wakiwa bado kabisa!tumefanya hivyo kwa Nsajigwa, na ilikuwa bado kidogo tumpoteze john boko.Lazima sasa tujiamini na tuwajengee kujiamini wachezaji wetu kwamba wanaweza.Angola jirani yetu aliweza kushiriki world cup kipi kinachotushinda.Tusilianzishe mapema.safari badoo!!!!

    ReplyDelete
  6. tatizo kiswahili kigumu, hakuna paliposemwa kwamba hakuna mbadala wa Nyoni, ila pamesemwa kwamba Poulsen anakuwa na wakati mgumu kumpata mbadala wa Nyoni, maana yake ni kwamba wapo wachezaji wengi wanaoweza kucheza nafasi yake lakini inakuwa vigumu kumpata mwenye sifa kama za Nyoni ambazo ndio inaelekea kocha anazihitaji, vinginevyo kwa muda ambao Nyoni hajacheza kwenye ligi wangeshaitwa wengi na kupewa nafasi hiyo kucheza

    ReplyDelete