Search This Blog

Tuesday, March 26, 2013

MBWANA SAMATTA AKIRI DOMAYO NA SURE BOY NI KIBOKO DIMBANI

SALUM Abubakari na Frank Domayo ni wachezaji ambao wameleta mapinduzi makubwa kwenye kikosi cha Taifa Stars.
Hiyo ni kutokana na vijana hao kucheza kwa kiwango kikubwa kwenye safu ya kiungo.
Mshambuliaji, Samatta amekiri kuwa vijana hao licha ya kuwa na maumbile madogo wanafanya kazi yao ipasavyo.
"Jamaa wapo vizuri. Ukiwatazama maumbile yao na kazi ambayo wanaifanya ni vitu viwili tofauti." alisema Samatta anayekipiga na klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.
Katika mchezo wa Stars na Morocco uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi Jumapili kusaka kufuzu fainali za Kombe la Dunia, Brazil mwakani.Stars ilishinda mabao 3-1.
Kiungo Salum Abubakari wa Azam FC aliyekuwa akicheza nafasi ya kiungo mchezeshaji alipiga jumla ya pasi 66 wakati Frank Domayo wa Yanga aliyecheza nafasi ya kiungo mkabaji alipiga 54.
Kati ya pasi 66 alizopiga Sure boy kwenye mchezo huo. Pasi 56 zilikuwa sahihi wakati 10 zikipotea njia.
Frank Domayo aliyekuwa na jukumu kucheza nafasi ya kiungo mkabaji, alipiga jumla ya pasi 54. Kati ya pasi hizo 48 zilikuwa sahihi wakati sita zilienda fyongo.
Pia, Domayo alipiga mashuti matatu kwenye lango la Morocco huku Sure boy akijibu kwa kufumua mashuti mawili.

6 comments:

  1. Sure boy na Domayo wako vizuri lakini wasibweteke na kuona bila wao mambo hayataenda kama vp waongeze bidii zaidi ya hapo nawakubali sana by PETER MASHOSHO- BUGANDO UNIVERSITY MWANZA

    ReplyDelete
  2. Yaaap jamaa wako fiti sana kikubwa wajiepushe na mambo yasiyo na msingi nje ya uwanja

    ReplyDelete
  3. Tanzania kwanza....

    ReplyDelete
  4. kaka shaffih ih umeipata na hii http://googlehabari.blogspot.com/2013/03/mbwana-samata-atamba-kwenye-magazeti-ya.html

    ReplyDelete
  5. Hao jamaa wako fit sana ..ningependa tuwe kama waspain ..tujaribu kuwatengenezea mazingira ili wawe pacha bora zaidi..ningependa kwa upande wangu. Dumayo amfwate sure Azam.

    ReplyDelete
  6. kwa kweli wako sawa kazeni vijana muende mbele msilidhike na maneno ya sifa.shaffihdauda.com

    ReplyDelete