“Nafikiria sana kucheza nje ndiyo ninachokiwaza
kutwa nzima” anasema kiungo mshambuliaji, Zahoro Pazi ambaye anacheza kwa
mkopo katika timu ya soka ya JKT Ruvu ya Pwani akitokea timu ya Azam FC. Zahoro
ambaye alikuwa nchini Afrika ya kusini akifanya majaribio ya kucheza soka la
kulipwa katika timu ya Bloamfontein Celtic ya ligi kuu ya SA na kukosa nafasi baada
ya timu hiyo kuhitaji mchezaji mmoja tu ili wafikishe idadi ya wachezaji watano
wa kigeni wanaotakiwa kisheria nchini humo.
Katika
majaribio hayo yaliyochukua siku kumi, Zahoro alifanya vizuri lakini Celtic
ilikuwa ikihitaji mshambuliaji zaidi kuliko kiungo na hivyo kujikuta akipoteza
nafasi ya kucheza soka nchini humo.
“ Namshukuru Mungu nimepigana mpaka mwisho na kiukweli sikufeli katika yale majaribio, ila sheria
za kule ni kila timu kuwa na wachezaji watano wa kigeni, na kulikuwa na nafasi moja tu iliyokuwa
imebaki, na jamaa ( Celtic) walikuwa wakihitaji mshambuliaji zaidi, na mimi
nilikuwa winga, nafasi hiyo akapata raia wa Zimbabwe” anasema, Zahoro jioni ya
leo wakati akizungumza na tovuti hii.
“ Nimerudi Najiandaa upya nitafanya kazi katika
timu yangu ya JKT Ruvu, na nafikiria kuwa huu utakuwa msimu wangu wa mwisho
kucheza katika ligi kuu ya Tanzania na klabu za hapa nyumbani, Mungu akiitikia
kilio changu kuna mahali nafikiria kwenda, lakini yote namuachia yeye kwa
sababu ndiye anayepanga kila kitu hapa duniani” anamaliza kusema kiungo huyo wa
zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania na vilabu vya Mtibwa Sugar na African Lyon
SAFIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII
ReplyDelete