Search This Blog

Wednesday, February 27, 2013

YANGA YAENDELEA KUJIKITA KILELENI,YAIFUNGA KAGERA SUGAR BAO 1:0

 
YANGA imeendelea kujikita kileleni   na kuicha Azam kwa pointi 6 baada ya  kuichapa Kagera Sugar kwa bao 1-0  katika mchezo wa jana kwenye Uwanja  wa Taifa, Dar es Salaam.  Kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Niyonzima aliwainua mashabiki  wa Yanga baada ya kufunga bao hilo kwa shuti la umbali wa mita 20, lililomshinda kipa wa Kagera Sugar, Hannington Kalyesubula.
Kwa matokeo hayo Yanga sasa imefikisha pointi 42 ikifutiwa na Azam (36), huku mabingwa watetezi Simba  akiwa nafasi ya tatu na pointi zake 31.Kipa wa Kagera,  Kalyesubula alifanya  kazi nzuri kuinyima Yanga bao la  mapema baada ya kupangua kichwa  kilichopigwa na Didier Kavumbagu  aliyeunganisha kwa uzuri krosi ya Simon Msuva dakika ya kwanza.
Viungo wa Yanga, Frank Domayo, Athumain Idd na Haruna Niyonzima walitawala sehemu kubwa ya mchezo huo na kuwafanya Kagera Sugar muda  wote kucheza kwa kujiami.Katika dakika 15, Yanga ilikuwa imefika langoni kwa Kagera mara tano wakati vijana wa Kaitaba wakijibu mapigo mara moja tu.
Kocha wa Yanga, Ernest Brandts alimweka benchi mshambuliaji wake Jerryson Tegete baada ya kuonyesha kiwango cha chini katika mchezo uliopita dhidi ya Azam na kumwazisha Kavumbagu.Mshambuliaji huyo wa Burundi, alinyima Yanga bao katika dakika 45 baada ya mkwaju wake wa penalti kupaa juu ya lango la Kagera Sugar.Yanga ilipata penalti hiyo baada ya kipa Kalyesubula kumwagusha Kavumbagu kwenye eneo la hatari na mwamuzi Simon Mberwa wa Pwani kupuliza filimbi.
Yanga walirudi kwa kasi kipindi cha pili katika dakika 48, shuti la Domayo  liligonga mwamba na kurudi uwanjani.Kagera Sugar iliwapumzisha Julius Mrope na Darlington Enyinna na kuwaingiza Temi Felix, Paul Ngwai, wakati Yanga iliwatoa Said Bahanuzi na Kavumbagu kuwaingiza Jerryson Tegete na Hamis Kiiza.Mabadiliko hayo yalikuwa na faida kwa Yanga katika dakika 65 walifanikiwa kupata bao lililofungwa na Niyonzima kwa shuti la umbali wa mita 20.
Katika michezo mingine Polisi Morogoro wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani Jamhuri waliwatambia  Mgambo JKT kwa kuichapa bao 1-0.Shujaa wa Polisi alikuwa Nahoda Bakari aliyefunga bao akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa Mgambo, Tonny Kavishe akipangua penalti Kondo Salum baada ya beki Musa Ngunda kushika mpira kwenye eneo la hatari. Mkwakwani, Coastal Union walishindwa kuhutumia vizuri uwanja  wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa kwenda suluhu na Ruvu Shooting, sawa na matokeo ya Mtibwa
Sugar na Prisons uliochezwa Manungu, Turiani.

2 comments:

  1. siku moja nilibahatika kukaa na wewe shaffii jukwaa la vip taifa katika mechi yanga na prisons, tuliongelea tabia ya wachezaji wa yanga kushangilia kwenye benchi lao wakifunga goli kwamba watakuja kufungwa goli wakati wanashangilia goli lao maana huwa wanarudi wote, sasa jana kagera sugar kidogo watumie mwanya huo, ingawa oscar alibaki ila akajisahau akakaa kwenye edge jamaa wakaanza mpira wakati yanga wanashangilia kidogo wapate bao, hii tabia ya kushangilia kwa kuvuka msitari wa katikati itakuja kuwatokea puani. basi kama wanataka kumpanga mtu wa kubaki akae ndani katikati sio kwenye marefa saa ingine wanajifanya hawaoni kama jana oscar alibaki pembeni mara kainama, refa akawaruhusu waanze jamaa

    ReplyDelete