UONGOZI wa timu ya Azam umeliandikia barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ya kuomba kocha wao msaidizi Kali Ongala aruhusiwe kukaa benchi, baada ya kocha wao Mkuu Stewart Hall kufungiwa mechi tatu na kulipa faini ya Sh500,000 kwa kosa la kuvua bukta Uwanjani.Ongala amesimamishwa na TFF, kwa
kwa kuwa hana yeti vinavyo mtambulisha kama kocha msaidizi wa Azam.Kamati ya ligi kuu ilitangaza kumfungia kocha Stewart mechi tatu na faini ya Sh500,000 kwa kosa la kuvua bukta uwanjani wakati wa mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar.
Katibu Mkuu wa Azam, Idrissa Nassor alisema kuwa baada kufungiwa kocha wao wameiandikia barua TFF, kuomba wamruhusu Ongala kukaa benchi mpaka uchunguzi wa vyeti vyake utakapokamilika.''Ongala alifungiwa lakini tulishapeleka vyeti vyake muda mrefu lakini mpaka sasa wamekaa kimya hivyo tumewaandikia barua ya kumruhusu kocha huo msaidizi mpaka pale watakapojiridhisha na uchunguzi wao'' alisema Nassoro.
Katika hatua nyingine, Nassor alisema kuwa timu yao inatarajia kuondoka nchini Jumamosi Asubuhi kwenda Sudan kusini kwa ajili ya kucheza mchezo wao wa marudioano dhidi ya El Nasri Juba.Alisema wanatarajia kupata upinzani mkubwa ugenini kwa kuwa nia yao na ya kwao wote ni kuakikisha wanasonga mbele katika michuano hiyo.
Alisema timu itaondoka ikiwa na wachezaji 20 na viongozi saba tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Jumapili
No comments:
Post a Comment