Search This Blog

Friday, February 8, 2013

SPORTS EXTRA YA CLOUDS FM YAMPATIA MZEE ATHUMAN KILAMBO SHILINGI LAKI TANO - NA HIVI NDIO HALI YAKE ILIVYO SASA

Kipindi bora cha michezo nchini Tanzania kutoka kwenye super brand radio station, Sports Extra jana kilionyeshwa kuguswa na hali ya kiafya aliyonayo gwiji wa soka nchini aliyewahi kuipa mafanikio makubwa klabu ya Pan Africa, Mzee Athuman Kilambo.

Kama ambavyo mtandao huu ulivyowahi kuripoti kuwa muanzilishi huyo wa klabu kongwe ya Pan African amekuwa akiugua ugonjwa wa kansa ya koo na alikuwa akihitaji msaada wa matibabu, jana mchana mwakilishi wa Sports Extra Shaffih Dauda alienda kumtembelea Mzee Kilambo nyumbani kwake na kumpatia kiasi cha pesa cha shilingi laki 5 ili ziweze kumsaidia kujitibu.

Kiukweli hali ya Mzee wetu imezidi kuwa mbaya na anakosa msaada wa kutosha ili aweze kujitibia ugonjwa huo ambao umedhoofisha kabisa afya yake.

Wanamichezo tuungane kumsaidia huyu Mzee wetu ili aweze kutibiwa kwani anahitaji fedha nyingi ili aweze kufanyiwa upasuaji na matibabu mengine. Viongozi wa soka, wapenzi, wanasoka na mashabiki wa mchezo huu, huu ndio wakati kuonesha umoja kama waliona wacheza filamu kama walivyoonesha wakati mwenzao Sajuki anaumwa.

Athumani Kilambo, ameifanyia makubwa taifa letu na soka letu, amefanya mambo mengi makubwa ambayo nikiyataja sitoweza kuyamaliza leo, kwa ufupi Watanzania huu ni Muda wa kurudisha fadhila, huu ni muda wa wanamichezo kuonesha uwanamichezo wetu. 

Shirikisho la soka nchini na wanachama wake mna fursa za kuandaa japo mechi kwa ajili ya kuweza kupata mapato yatakayoweza kwenda kumsaidia huyu mzee, tusisubiri mtu afariki (siombei) ndio tuanze kujionesha kwamba tulikuwa tunamjali.  

Tumsaidie mwenzetu wanamichezo.  

2 comments:

  1. Asanteni sana kwa moyo wenu wa Upendo! Hii pia inaonesha jinsi tusivyo na mipango endelevu na watu mbalimbali hasa wale waliotutangulia katika kuliletea Taifa heshima. Hii ni challenge kwa TFF na Wizara husika kwanza kuwa hawana mipango madhubuti na watu mbalimbali waliolitumikia Taifa. Tunafahamu hawawezi kumsaidia kila mtu lkn japo kuwashika mkono na kuwasaidia watu kama hawa wanapofikwa na matatizo! Wachezaji pia hii ni changamoto kwenu kuwa ni vizuri kuwa na chama chenu kitakachowasaidia pindi mnapokuwa aidha mmestaafu au mmefikwa na madhira kama haya! hasa kwa wachezaji wetu wa sasa ambao hali zao angalau zinaeleweka! Mwisho kwa kweli hali hii ngumu wadau tumshike mkono mzee wetu! Naomba kuwasilisha. NURU SPORTS MSM

    ReplyDelete
  2. Hongereni sana sports xtra kwa kujitolea kumsaidia mzee wetu. Mi naamini kama tungewajali wazee wetu waliopigania timu yetu ya taifa tungekuwa na baraka zao kwa kuwa tumewatupa ma legend wetu ndo maana timu zetu hazifanyi vizuri.

    ReplyDelete