Hali ya usafi katika uwanja wetu wa taifa sio nzuri na inatia kinyaa kwa kweli pia ni aibu kwa soka letu na nchi kiujumla.
Katika mchezo wa Jumatano kati ya Tanzania na Cameroon katika jukwaa la VIP C nilishuhudia kinyesi cha binadamu kikiwa kimezagaa katika ngazi za kwenye siti za uwanja huo.
Kutokana na kuona uchafu huo ikabidi nianze kufuatilia suala hilo kwanini kinyesi kile kipo pale, katika kuuliza kwangu nikagundua kwamba baadhi ya vyoo vilikuwa vimejaa na kutapika hivyo inawezekana kuna shabiki mmoja wapo aliyekosa ustaarabu aliamua kujisaidia kwenye eneo hilo baada ya kubanwa na haja.
Lakini uwanja huu wa taifa umetoka kuchezewa mechi mbili kubwa wikiendi iliyopita na katika mechi hiyo tuliambiwa kwamba kuna mamilioni yalikuwa yamekatwa, katika mechi ya Yanga na Mtibwa zilikatwa shilingi millioni 15,435,255.48, wakati kwenye mechi ya Simba vs JKT zilikatwa
8,869,704.64, hivyo ndani ya siku mbili uwanja ulichukua zaidi ya Millioni 24.
8,869,704.64, hivyo ndani ya siku mbili uwanja ulichukua zaidi ya Millioni 24.
Sasa kweli kihulasia ni wapi fedha hizo zinakwenda kiasi cha kushindwa hata kutoa fedha za kusafisha uwanja pamoja na kuvuta vyoo au kurekebisha hali iliyopo vyooni ili kuepeuka uchafu unaokuwepo uwanjani?
Tunatia aibu kwa jambo hili na pia tunahatarisha afya za mashabiki wanaoingia uwanjani kuangalia mechi.
Jamani sisi watanzania tuna matatizo gani? hata usafi tu mahali penye kuingiza mamilioni kwa siku inashindikana? tunapata wasiwasi na utendendaji wa wanaohusika kusimamia uwanja huu na iwapo mgawanyo wa mapato ni kwa maslahi ya Taifa (uwanja au matumbo ya watu?) Naomba niishie hapo kwani nakosa maneno mazuri mwishoe ntakosea na inatia uchungu sana! Au na uwanja tuubinafsishe? NURU SPORTS MSM.
ReplyDeleteNtumaini aliyefanya hivyo unaweza kumuona mjinga lakini ndo mwelevu kuonyesha jinsi gani mazingira alivyo.
ReplyDeleteSwali,Je mpaka mtu akajisaidie pale hakuna walizi,au wafanyakazi,?
Swali,Je kama vyoo vimejaa nani angejua kama wahusika awavikaguiii?
Jibu, WAHUSIKA NDO WALIOJOISAIDIA PALE NA SI MGENI ANAYEKUJA KUANGALIA MPIRA.
sema kaka maana TFF hawawajibiki wapo kimaslahi tu..............Vipi rufaa yako kaka
ReplyDelete#Team shaffi dauda.
Wadau wa mchezo mm noamba picha za hali ya vyoo itolewe kwenye vtombo vya habari, uenda ikasaidia kwan hali ni mbaya tena mbaya sana.
ReplyDeletenajiuliza ni kuwa watanzania hatuna ustaarabu hata kidogo wa matumizi ya vyoo au ni uhuni tu baadhi ya watu.
Usafi huanzia nyumbani, kwan hata majumbani kwetu ni kuchafu tutaweza ambapo hapatuhusu!!!
Serikali imefikia wapi kwa kampuni ya kutunza uwanja wa taifa!!! kumbukeni umegharimu pesa nyingi na unachakaa kwa kasi sana.
Huo uwanja ni mali ya wachina wenyewe wanakusanya hela zao mpake deni liishe lote wanatuachia vinyesi sisi tusafishe.
ReplyDeleteukienda vyoo vya uwanjani ni aibu sana hata kusema ni aibu alafu unasema tutunze vyetu kwa staili hile amna kwa kweli vyoo vinatia aibu sio vipc wala b vyoo vyetu vichafu yani ni vinyaa kweli kukamata watu na kuwapa 5000 kusafisha wanashindwa daah aibu
ReplyDelete