MWENYEKITI wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Rahma Al Kharusi ameahidi
kumlipa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Milovan Cirkovic dola 32,000 ambazo
anaidai klabu hiyo.
Milovan anaidai Simba fedha hizo kutokana na
kuvunjwa kwa mkataba, malimbikizo ya mshahara miezi mitatu iliyobaki
pamoja na mshahara wa mwezi mmoja.
Al Kharusi alimwalika Milovan
raia huyo wa nchini Serbia na kuzungumza naye kwa kirefu juu ya madai
yake kwa Simba katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kharusi ambaye ameondoka jana kurejea Oman alisema:
"Nitamlipa Milovan (Cirkovic) fedha zake zote ambazo anaidai Simba kabla ya Jumatano ijayo.
Alisema yeye haogopi chochote na anasema kitu ambacho anakiona hakifai ndani ya uongozi wa timu
hiyo.
"Kwa sababu sitaki kuona ubabaishaji nitasema jambo lolote ambalo naliona halina mashiko na timu."
"Unajua ni kitu cha ajabu, kocha huyu tunaweza kumwitaji baadaye, kwa hiyo si vizuri kumchosha,"alisema Al Kharusi.
Akizungumzia
pambano la Simba na Libolo Ligi ya Mabingwa alisema; "Timu haikucheza
vizuri kabisa naona kama walikuwa wanafanya mazoezi."
No comments:
Post a Comment