Mnamo mwaka 2011, Unal Aysal alichaguliwa kuwa Raisi mpya wa Galatasaray, klabu ambayo wakati huo ilikua na deni linalozidi euro milioni 240.
Kwa kifupi
klabu ilikuwa ni kama mufilisi.
Tangu Unal
Aysal alipoichukua timu takribani miaka miwili iliyopita Galataray mambo yake
kiuchumi yanakwenda vizuri, kwasasa wanashika nafasi ya 30 kwenye msimamo wa
vilabu tajiri ulimwenguni.
Baadhi ya wanasoka mahiri ulimwenguni kama vile Didier Drogba na Wesley Sneijder wamevutiwa na Gala inayoutumia uwanja mpya wa kisasa wa Turk Telekom pamoja na wachezaji wengine wenye majina kama Fernando Muslera, Emmanuel Eboue, Johan Elmander na Burak Yilmaz.
Namna gani mambo yamebadilika ghafla bin vuu?
Jibu jepesi la mafanikio ya Galatasary ni jina la mmiliki wa timu hiyo ndugu Aysal, tajiri anayeshika nafasi ya 45 kwenye orodha ya matajiri nchini Uturuki, aliutumia utajiri wake kutatua matatizo lukuki yaliyokuwa yanaikabili Gala kama ambavyo Abramovich alifanya kuinusuru chelsea.

Aysal aliwekeza kwa
wachezaji wapya mara tu baada ya kuwasili pamoja na kumuuza aliyekuwa nahodha Arda Turan kwenda Atletico Madrid, aliwasajili
wachezaji kama golikipa wa timu ya taifa ya Uruguay Muslera, Eboue, Elmander na Felipe Melo.
Uwekezaji huo ulilipa mara moja kwani Galatasaray walishinda ubingwa wa Uturuki, ubingwa uliowaingizia kitita cha euro milioni 30m, kwa kufuzu tu kwenye michuano ya Uefa champions league pia waliweka kibindoni kiasi cha euro milioni 27. Kufunguliwa kwa uwanja mpya wa Turk Telekom Arena wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 52,000 wakiwa wameketi vitini walifanikiwa kuingiza kiasi kingine cha Euro milioni 30 kutokana na VIP lounges pamoja na ununuzi wa tiketi za msimu.

Sehemu ya utata
kwenye deals za biashara za Galatasaray ilionekana kwenye soko la hisa . Kati ya
mwezi agosti na mwezi desemba mwaka 2011, waliuza asilimia 28.35 ya hisa za
klabu toka kwenye kampuni mama ya Galatasaray AS deal ambayo iliingizia klabu
euro milioni 70 .
Hii ilifuatiwa
na tangazo kuwa mapato yote ya mlangoni kwenye uwanja wa Turk Telkom Arena
yataenda moja kwa moja kwenye tawi la soka la timu hiyo kinyume na ilivyokuwa awali chini ya kampuni
mama ambayo iliingiza sehemu ndogo ya mapato kwneye maendeleo ya timu.
Kisha likaja
ongezeko la asilimi 400% la hisa za kampuni ongezeko ambalo lilishusha thamani
ya wana hisa binafsiambao walilazimika kulipa euro 11 kwa kila hisa jambo
ambalo liliongeza mapato na kufikia idadi ya euro milioni 117. Kinyume na
ilivyo kawaida, klabu haikulipa faida kwa wanahisa kama inavyohitajika faida
ya euro 65 bali iliandika toka kwenye makato ya mlangoni ya mechi za usoni .
Miezi mitano
baadaye kampuni iliripoti ongezeko la asilimia 300% kwenye hisa za msingi,
jambo ambalo bodi maalum ya uangalizi wa masuala ya biashara ilizuia .
Kubalance mahesabu ilikuwa sehemu ya mpango mkubwa wa
kuifanya Gala kuwa kampuni inayofanya vizuri kibiashara . Mfano mzuri ni
usajili wa Drogba na Sneijder ambao wamesajiliwa kwa malengo ya kuleta ushindi
uwanjani na upande wa biashara huku kodi zao zikilipwa na watu wengine.
CEO wa kampuni inayomiliki Galatasaray amesema kuwa lengo
ni kutwaa ubingwa wa ligi ya Uturuki na kufanya vizuri Ulaya na kuifanya Gala
kuwa klabu bora ulimwenguni. Hilo linaendana na kauli ya mkurugenzi huyo ambaye
amesema kuwa klabu hiyo inahitaji wachezaji wakubwa ili kutimiza malengo
makubwa.
Wakati Gala walipotwaa kombe la UEFA mwaka 2000 ,
mishahara ya Gheorge Hagi, Gheorge Popescu, Claudio Tafarrel na wengine
ilileta balaa katika miaka iliyofuatia hali iliyosababisha kikosi kupunguzwa na
hili liko hatarini kutokea kwa sasa.
Jinsi ya kutatua tatizo hili Aysal anasema kuwa falsafa
yake kama mfanyabiashara anaamini kuwa mfanyabiashara anapaswa kuwa mtu mwenye
uthubutu, na mbishi. Kwake kuwa mbahili hakukufanyi uwafurahishe mashabiki na
kuuza tiketi.
Mashabiki kwa sasa wana furaha, na Aysal anaamini kuwa
Gala itakuwa klabu kubwa duniani siku si nyingi na hili ni jambo ambalo
mashabiki wa Fernabace na Besiktas wanacheka wakilisikia. Ila hawacheki
wakiona Gala inawapanga Drogba na Sneijder kwenye mechi zao huku wakijiandaa
kucheza 16 ya Ligi ya mabingwa.
Kamari aliyocheza Aysal inaonekana kulipa ila lazima
klabu ishinde nyumbani na ulaya ili kuepuka historia ya kina Hagi na Tafarel
kujirudia .
No comments:
Post a Comment