Search This Blog
Sunday, February 10, 2013
MBUYU TWITE, KIIZA NA NIYONZIMA WAREJEA NA YANGA WAINGIA KAMBINI KUANDAA MAUAJI YA AFRICAN LYON JUMATANO
Wachezaji 26 wa timu ya Young Africans wanaingia kambini leo jioni katika hosteli zilizopo makao makuu ya klabu mitaa ya Twiga/Jangwani tayari kwa maandalizi ya mchezo wa ligi Kuu ya Vodacom siku ya jumatano dhidi ya timu ya African Lyon katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans ambayo inaongoza msimamo wa ligi kuu ya Vodacom (VPL) kwa kuwa na pointi 33 huku ikiwa imecheza michezo 15, inafuatiwa nafasi ya pili na timu ya Azam FC yenye pointi 30 ambayo leo inacheza dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro katika uwanja wa Manungu Complex.
Wachezaji wote walikuwa wamepewa mapumziko ya siku mbili kwa siku za jumamosi na jumapili kabla ya leo jioni kuingia kambini na kesho asubuhi kuanza mazoezi ya pamoja katika uwanja wa mabatini Kijitonyama.
Ikumbukwe Young Africans ilitoa wachezaji 8 kwa ajili ya kujiunga na timu zao za Taifa kwa ajili ya michezo ya kirafiki ya kalenda ya FIFA lakini wachezaji 18 waliobakia walikua wakiendelea na mazoezi kila siku asubuhi mpaka wachezaji wengine waliporejea na kuendelea na mazoezi kwa pamoja.
Didier Kavumbagu ana nafasi ya kuongeza idadi ya mabao katika mchezo wa jumatano kufuatia kurudi katika hali nzuri ya kimchezo, huku Jerson Tegete, Hamis Kiiza na Said Bahanuzi nao wakiwa na nafasi ya kuongeza mabao katika mchezo huo.
Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Hamis Kiiza walisharejea tangu siku ya ijumaa tayari kabisa kuungana na wachezaji wenzao na leo jioni wataingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo dhidi ya African Lyon siku ya jumatano.
Katika mchezo huo wa jumatano Young Africans inahitaji ushindi ili kuendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu kisha kuweka mazingira mazuri ya ushindi katika mchezo utakaofuata dhidi ya Azam Fc februari 23, 2013 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment