Search This Blog
Wednesday, February 6, 2013
LIVE MATCH CENTRE: TANZANIA 1-0 CAMEROON FULL TIME
DDk 90 FULL TIME! Taifa Stars 1-0 Cameroon.
Dk 89 Goooo..! Mbwana Samatta anaifungia Taifa Stars bao la kuongoza akiunganisha krosi ya Erasto Nyoni.
Dk 85 Cameroon inafanya mabadiliko wametoka Aboubakar Vincent na Bouba wameingia Bakinde Gerard na Makoun Jean.
Dk 83 Amri Kiemba wa Taifa Stars anakosa bao la wazi bao la wazi baada ya mpira aliokuwa akiusubiri kuingiliwa na beki wa Cameroon, Assou Ekotto.
Dk 79 Kaseja anadaka shuti kali la Ashu Clovis wa Cameroon. Walikuwa wamebaki wawili tu.
Dk 73 Cameroon inafanya mabadiliko anatoka Bedimo Henri anaingia Ashu Clovis.
Dk 70 Sure Boy anapiga shuti kali langoni kwa Cameroon lakini beki Ngoula anautoa nje na kuwa kona butu.
Dk 68 Cameroon inafanya mabadiliko anatoka Olinga Fabrice anaingia Edoa Charle.
Dk 66 Sure Boy anapiga shuti kali katika lango la Cameroon lakini kipa Effala Komguep anadaka.
Dk 60 beki wa Cameroon Aminou Bouba anabanwa misuli na kutibiwa uwanjani wakati Taifa Stars ikiwa katika shambulizi kali.
Dk 60 beki wa Cameroon Aminou Bouba anabanwa misuli na kutibiwa uwanjani wakati Taifa Stars ikiwa katika shambulizi kali.
Dk 58 Cameroon inafanya mabadiliko anatoka Tchami Herve anaingia Eloundu.
Dk 56 Taifa Stars inafanya mabadiliko anatoka Mwinyi Kazimoto anaingia Thomas Ulimwengu.
Dk 54 Ngoula wa Cameroon anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Mrisho Ngassa.
Dk 48 Taifa Stars inafanya shambulizi kali langoni kwa Camerooni.
Dk 48 Taifa Stars inafanya shambulizi kali langoni kwa Camerooni.
Dk 45 Kipindi cha pili kimeanza
Dk 45 HALF TIME. Taifa Stars 0-0 Cameroon
Dk 41 Timu zinaendelea kushambuliana kwa zamu na Taifa Stars inafika mara kadhaa langoni kwa Cameroon.
Dk 28 Shomari Kapombe wa Taifa Stars anaonyeshwa kadi ya njano kwa mchezo mbovu.
Dk 26 Taifa Starz inapata penalti ilikuwa krosi ya nyoni kabla ya beki ngoula kushika mpira. Nyoni anapiga anakosa.
Dk 25: Tanzania 0-0 Cameroon
Dk 20 Kipa wa Taifa Stars, Juma Kaseja anatibiwa baada ya kugongana na mshambuliaji mmoja wa Cameroon.
Dk 19 Frank Domayo anaonyeshwa kadi ya njano kwa mchezo usiofaa kwa mchezaji wa Cameroon.
Dk 15 Timu zinashambuliana kwa zamu na zinatawala kwa pamoja sehemu ya kiungo. TAIFA STARS 0-0 CAMEROON
DK 1: Mpira umeanza Tanzania 0-0 Cameroon
LINE UP: TAIFA STAS, Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Kelvin Yondan, Aggrey Morris, Salum Aboubakar 'Sure Boy', Mrisho Ngassa, Frank Domayo, Mbwana Samatta, Mwinyi Kazimoto na Amri Kiemba
CAMEROON: Effala komguep,assou ekotto,aminou bouba,ngoula,nyom allan,pierre wome nlend,kingue mpondo,bedimo henry,tchami herve,olinga fabrice,aboubak vicent.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Leo safi, umejitahidi sana, kutoa live yanayo jiri uwanjani. Keep it up!
ReplyDeleteSamagooooooooooooooooooooooooooaaaaaaaaaal anatishaaaaaaaa! viva tanzania viva taifa stars
ReplyDeleteBaba Faheemah
thnx brooooo,,,Startv na TBC ame2bania...keep it up..Congratz 2 Tz
DeleteCongrats stars kwa mchezo mzuri pia nimefurahishwa na support ya wa Tanzania huu ni mwanzo mzuri
ReplyDeletePlease uwe unaweka picha ya wachezaji waliocheza siku ya mchezo.. sio picha inayowa include wavuta bangi akina Boban!! Ovyooo sana huyu jamaa!!
ReplyDeletethnx brooooo,,,Startv na TBC ame2bania...keep it up..Congratz 2 Tz
ReplyDeletethnx brooooo,,,Startv na TBC ame2bania...keep it up..Congratz 2 Tz
ReplyDeleteSamata sio mtanzania. subirini tukate rufaa
ReplyDeletethnx brooooo,,,Startv na TBC ame2bania...keep it up..Congratz 2 Tz!!proud
ReplyDeletethnx brooooo,,,Startv na TBC ame2bania...keep it up..Congratz 2 Tz
ReplyDeletethats 9c, 2nataka tena! Bado hatjashba, ila leo wanaume wampga game, mchezo kama huo inatkiw 2kaupgie africon!
ReplyDeletethats 9c, 2nataka tena! Bado hatjashba, ila leo wanaume wampga game, mchezo kama huo inatkiw 2kaupgie africon!
ReplyDeleteSafi sana yatakiwa mambo kama hayo hakuna kuogopa timu kubwa nyie pi waweza kama wao nataka mambo kama haya mfanye na morocco
ReplyDeleteOngezeni juhudi na kusikiliza maagizo y mwalimu anavotaka naamini tutaenda afcon sidhani timu kama ethiopia au niger ina uwezo kupita sisi nazo zimeenda tushndw siee
ReplyDeleteLampard
Hapa umetuonyesha vema kilicho endelea huko Uwanja wa Taifa kumbe Simba wasiofungika leo wamefungika asante sana mchambuzi wetu.Mr. Lungo wa Lushoto Tanga.
ReplyDeletehongera xana taifa stars
ReplyDeletesimba oyeeeeeeeee
ReplyDeletecross haikupigwa na Nyoni kaka, kama unakumbuka Nyoni alikua amepanda na akaumia ila alikua ndio anarejea uwanjani upande ule ule cross ilipotoka tena kama ingekua bado sheria ya offside haijabadilishwa ile ingekua ni offside.
ReplyDeletekrosi ilipigwa na frank domayo mkubwa ila big up kwa kazi
ReplyDelete