Search This Blog
Wednesday, February 6, 2013
BOBAN, CHOMBO WATIMULIWA MAZOEZINI, KAZIMOTO, NGASSA, BOBAN KIKAANGONI
KLABU ya soka ya Simba, ipo mbioni kuwatimua kikosini wachezaji wake watatu na jana kocha Patrick Liewig aliwatimua mazoezini wachezaji Haruna Moshi ‘Boban’ na Ramadhan Chombo ‘Redondo’.
Habari zaidi ambazo zimethibitishwa na Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, wachezaji hao watajadiliwa na kamati ya utendaji kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utovu wa nidhamu.
BOBAN, CHOMBO WATIMULIWA MAZOEZINI
Wachezaji Boban na Chombo jana walitimuliwa katika mazoezi ya timu hiyo kwa kile kilichoelezwa kwamba, hawaendani na mazoezi ya Kocha Liewig.
Baada ya kuwavumilia kwa muda mrefu, Liewig aliwaita wachezaji hao na kuwataka kutoka katika kundi la wenzao kisha akawalekeza kwenda kaskazini mwa Uwanja wa TCC.
Wachezaji hao walifanya hivyo hadi wenzao walipomaliza mazoezi na moja kwa moja ilionekana Liewig amefikisha suala lao kwa uongozi ili waweze kuchukuliwa hatua zaidi.
Hata hivyo, mara baada ya kuondoka baadaye, meneja wa Simba, Moses Basena, alimpigia simu Chombo na kumtaka leo audhurie mazoezi ya timu hiyo kama kawaida.
Hiyo ina maana kwamba, Chombo hana kosa kwa Liewig lakini Boban amekalia kuti kavu, kwani hajaitwa na moja kwa moja jina lake limepelekwa kwa uongozi kwa hatua zaidi.
MWINYI KAZIMOTO, NGASSA, BOBAN KIKAANGONI
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ameuambia mtandao huu kwamba wachezaji watatu wa timu hiyo, Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto na Boban majina yao yametua kwa uongozi ili waweze kujadiliwa kutokana na kukithiri kwa utovu wa nidhamu kikosini.
Bila kufafanua aina ya utovu wa nidhamu walionao wachezaji hao, Kaburu anasema; “Kocha ametuletea majina ya wachezaji hao na kusema tukae nao kisha tujue kama wanataka kuendelea kuichezea Simba au vinginevyo.”
“Kocha wetu yupo makini katika suala zima la nidhamu na kama mchezaji hana nidhamu, tutatmwondoa kikosini.”
Mtandao unakuahidi kufuatilia zaidi matokeo ya kikao cha uongozi wa Simba juu ya kuwajadili wachezaji hao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Its time to invest on youth. Kendelea kuwakumnatia akina Boban ni kupoteza musa. Simba ilikuwepo na itaendelea kuwepo bila ya Boban,Ngasa wala Kazimoto. Nakusaport Coach na endelea kukaza uzi!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
ReplyDeleteHivi simba kuendelea kumkumbatia Boban mpaka lini? Its time kuachana nae wachezaji wapo wengi nchi hii hawajapewa nafasi tu!
ReplyDeleteits time also hata wachezaji wawe wanapewa nafasi wakazungumza. tusihukumu kwa kusikiiza upande mmoja tu. Naanza kuamini kuwa hata viongozi wanaweza kuwa na matatizo lakin kwakuwa wachezaji hawana platfom ya kuzungumzia basi hukumu huwadondokea wao.
ReplyDelete