Search This Blog
Tuesday, February 19, 2013
KWANINI NIZAR KHALFANI ANAIPENDA JEZI NAMBA 16? - SIRI YAFICHUKA
NIZAR Khalfan amekataa kufichua siri ya kuvaa jezi yenye namba 16 mgongoni tangu akiwa na timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro 2005, lakini rafiki yake wa karibu amefichua siri hiyo.
Kiungo huyo wa Yanga alisema jijini Dar es Salaam ametokea kupenda kuvaa jezi yenye namba 16 mgongoni na hakuna lolote ambalo limejificha dhidi ya namba hiyo.
"Nafikiri nimetokea tu kuipenda. Hakuna siri yoyote ambayo imejificha juu ya namba 16 kwenye maisha yangu binafsi."
Lakini utafiti uliofanywa umebaini kuwa nyota huyo amekuwa akipendelea kuvalia namba hiyo akiwa anamaanisha idadi ya mabao aliyoifungia Mtibwa Sugar ambayo ndiyo timu iliyomtambulisha kisoka.
Nizar alijiunga na Mtibwa Sugar mwaka 2005, baada ya kumaliza kidato cha nne katika shule ya Sekondari Ocean iliyopo mkoani Mtwara.
Kiungo huyo alifanikiwa kuichezea timu hiyo mechi 57 katika mashindano tofauti kwa misimu miwili ya ligi. Kati ya mechi hizo alifunga mabao 16.
"Nizar ni rafiki yangu wa karibu. Aliwahi kuniambia, anapenda kuvalia jezi namba 16. Kwa sababu ndiyo idadi ya mabao aliyoifungia Mtibwa." alisema rafiki yake Nizar ambaye ni mchezaji mwenzake.
"Kama unataka kujua hilo, jezi namba 16 ilikuwa ikivaliwa na Rashid Gumbo. Lakini alipoondoka kwenda Mtibwa. Nizar aliomba kuvaa jezi hiyo."
"Aliniambia mwenyewe kuwa jezi hiyo huwa anajisikia vizuri akiwa ameivalia. Tofauti akivaa jezi yenye namba nyingine. Nizar amekuwa akivalia jezi yenye namba 16 akiwa na Mtibwa Sugar, Taifa Stars na sasa Yanga.
Wakati anajiunga na Yanga alikuta jezi hiyo ikivaliwa na Gumbo na kulazimika kuvaa jezi namba saba.Lakini alivyohama kwenda Mtibwa, Nizar alichukua jezi hiyo na namba saba akachukuliwa na Mrundi Didier Kavumbagu aliyekuwa akivalia jezi yenye namba 21 mgongoni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Huko Mtibwa alikuwa akivaa jezi namba ngapi ?
ReplyDeleteushaambiwa hata huko mtibwa alikua akivaa jezi namba 16 au hukusoma habari hii vizuri mdau hebu rudia tena kuisoma.
Delete