Search This Blog
Monday, February 4, 2013
JOHN BOCCO KURUDI DIMBANI DHIDI YA AFRICAN LYON
MSHAMBULIAJI wa Azam FC, John Bocco anatarajiwa kurudi uwanjani kuikabili African Lyon, mwezi ujao.
Bocco ambaye ni mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita ameshindwa kuichezea timu yake mechi hata moja kwenye mzunguko wa pili wa ligi, kutokana kuwa majeruhi.
Akizungumzia hali ya mchezaji huyo, daktari wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa alisema kuwa Bocco kwa sasa anaendelea vizuri na ameshaanza mazoezi mepesi.
“Hali yake kwa sasa inaendelea vizuri. Anazidi kuimarika siku hadi siku."Alieleza kuwa, baada ya wiki nne zijazo anaamini atakuwa fiti na kurejea uwanjani kuitumikia timu yake ya Azam FC.
Bocco aliumia akiwa na kikosi cha Kilimanjaro Stars mwaka jana kwenye mashindano ya Kombe la Chalenji yaliyofanyika jijini Kampala, Uganda .
Nyota huyo aliporejea nchini alipelekwa India na kufanyiwa upasuaji wa goti.
John Bocco atakuwa amekosa mechi tano za ligi. Tayari amekosa mchezo wa Kagera Sugar na Toto Africans. Pia ataikosa Mtibwa Sugar, JKT Ruvu na Yanga.
Staa huyo hadi sasa amezamisha mabao matatu. Kati ya magoli hayo moja amelipachika kwa penalti.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment