MSHAMBULIAJI wa Yanga, Jerry Tegete amesema amepania kujituma zaidi ili arudi kwenye kikosi cha Taifa Stars.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam Tegete amesema anafahamu kuwa Kim Poulsen ni kocha
ambaye hapendi maneno mengi bali anajali uwezo, juhudi na uzalendo.
Tegete amekiri kuwa mambo yanamwendea vizuri kwenye mzunguko wa pili wa
Ligi Kuu Tanzania Bara tangu timu hiyo ilipotoka Uturuki kwa kambi ya
wiki mbili kujiwinda na Ligi Kuu Bara.
Tegete katika siku za karibuni
alikuwa ameshuka kiwango kiasi cha kufanya asote benchi huku akiwaachia
mastraika wenzake Didier Kavumbagu, Hamisi Kiiza na Said Bahanuzi
wakitamba kikosi cha Yanga.
Hata hivyo, kwa sasa imekuwa kinyume chake kwani ndiye chaguo la kwanza
la kocha Ernie Brandts huku Bahanuzi na Kiiza wakianzia benchi.
“Nina usongo na Stars lakini nawaachia walimu na benchi la ufundi waangalie maendeleo yangu,” alisema nyota huyo.
Tegete alijumuishwa kwenye kikosi cha Stars na kocha Mbrazili Marcio
Maximo, ambaye akiwa anasoka katika shule ya Sekondari Makongo.
Stars
kwa sasa ipo kambini kijiwinda na mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi
ya timu ya taifa ya Cameroon Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam.
Mchezo huo upo kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa)
No comments:
Post a Comment