Search This Blog
Tuesday, February 5, 2013
HUU NDIO UKWELI WA KUENGULIWA KWA SHAFFIH DAUDA KTK UCHAGUZI WA TFF - NA MADUDU MENGINE YA KAMATI YA UCHGUZI
Februari, 2013 Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilitoa majina ya wagombea waliopitishwa kuwania uongozi katika ngazi mbalimbali ndani ya TFF na Bodi ya Ligi Kuu ya Bara.
Katika majina hayo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Deogratias Lyatto, ambaye ni mchumi aliyebobea, yapo majina ya wagombe ambao wamekatwa kuwania uongozi katika TFF kutokana na sababu mbalimbali ambazo hata hivyo, mtandao huu unaona bado kuna maswali mengi ya kujiuliza kutokana na uamuzi wa kamati hiyo.
Hapa chini baadhi ya maamuzi ya kutatanisha juu ya kamati hiyo, inayoongoza na mwanasheria aliyebobea, Lyatto.
Kwa mfano;
Shafii Dauda anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 13 (Dar es salaam) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa si mkweli: aliposhindwa kwenye uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam (DRFA) alipotosha umma kuhusu ushiriki wake kwenye uchaguzi huo na mchakato mzima wa uchaguzi. Pia hana ufahamu kuhusu Katiba ya TFF na majukumu ya Kamati ya Utendaji ya TFF.
Mantiki:
Kwa mujibu wa kamati hiyo, Dauda amebainika hana sifa za kugombea uongozi TFF kutokana na kutokidhi Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwamba, ameonekana kuwa kwa kuwa si mkweli, alipotosha umma na hana ufahamu kuhusu Katiba ya TFF.
Kwa kuwa si mkweli – Kwa mujibu wa kamati ya uchaguzi, Dauda anaonekana si mkweli hasa baada ya kushindwa nafasi ya ujumbe katika uchaguzi wa DRFA pale aliposema uchaguzi huo haukuwa huru na haki kwani wapiga kura wake walionekana wakipokea maelekezo ya nani wa kumpigia kura kutoka kwa kiongozi mmoja wa DRFA.
Alipotosha umma – Kamati inadai, Dauda mara baada ya kushindwa katika uchaguzi wa DRFA alidanganya umma kuhusu ushiriki wake kwa kusema, alikwenda kushiriki kwa kazi maalum ya kubaini madudu yanayoendelea ndani ya chaguzi za vyama vya soka. Hayo aliyasema kupitia kipindi cha michezo cha Sports Xtra kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha Clouds FM ambacho Dauda ni mwajiriwa.
Hana ufahamu kuhusu Katiba ya TFF- Kama inavyojieleza, kamati imesema Dauda hana ufahamu wowote juu ya katiba ya TFF ambayo ipo katika ofisi za shirikisho hilo Ilala jijini Dar es Salaam.
Ukweli wa mambo;
Kwa kuwa si mkweli- Si kweli kamba Dauda hakuwa mkweli kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi wa DRFA kwani kila kitu kilikuwa wazi, umma mzima wa Watanzania uliona kupitia luninga namna wapiga kura wa DRFA walivyokuwa wakipokea maagizo ya nani wa kumpigia kura ndani ya ukumbi kulikofanyika uchaguzi huo kitendo ambacho si halali huku muda wa kampeni ukiwa umekwisha. Hapo ushahidi wa sauti na picha upo, Je, uongo wa Dauda umetoka wapi. Kamati ilipaswa kutafuta ushahidi huo kwa njia inazojua ili kubaini uongo wa Dauda. Yawezekana wazi kwamba, kamati ilihofu Dauda anaweza kufichua mambo mengi zaidi endapo ataruhusiwa kuingia katika chumba cha mkutano wa TFF.
Alipotosha umma – Inaweza kuwa kweli Dauda alitamka kwamba alienda kugombea uongozi DRFA kwa kazi maalum, lakini halikuwa tamko rasmi la kituo cha redio au mgombea binafsi. Lazima vitu viwili vitenganishwe hapa, kwamba Dauda mfanyakazi wa Clouds na Dauda mgombea wa DRFA, hawa ni watu wawili tofauti. Kama mgombea wa DRFA, Dauda hakupotosha umma na hata akiwa mfanyakazi wa Clouds, hana kosa alilofanya juu ya kauli hiyo isiyo rasmi.
Hana ufahamu kuhusu Katiba ya TFF - Si kweli kwamba Dauda hana ufahamu wa katiba ya TFF, katika usaili aliulizwa kuhusu kazi ya kamati ya utendaji naye alijibu kwa ufasaha lakini kamati ya uchaguzi ilitaka ataje kazi hizo katika mlolongo kama ulivyoandikwa katika katiba hiyo. Yawezekana kamati ilitaka Dauda awe amekariri katiba hiyo kama masomo mengine ya darasani tena wale wa shule ya msingi. Ajabu ni kwamba, wagombea wengine wa nafasi aliyoomba Dauda hakukumbana na swali hilo.
MSIMAMO WA MTANDAO HUU;
Inaonekana wazi uongozi ndani ya TFF hautaki kuingiza sura ngeni na tayari mfumo umewekwa kuhakikisha viongozi ndani ya taasisi hiyo wawe wametokana na TFF yenyewe, MTU MPYA hatakiwi ndani ya TFF.
Tazama zengwe lingine;
Omary Isack Abdulkadir anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 13 (Dar es salaam) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa alikaidi maagizo ya TFF ya kuahirisha uchaguzi wa chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) na maagizo ya TFF kwa kuwa alienguliwa kwenye mchakato wa uchaguzi wa FRAT kwa kutotimiza matakwa ya Kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.
Ukweli na haki;
Baada ya kuenguliwa katika uchaguzi wa FRAT, Abdulkadir alitumia haki ya msingi ili kupata haki yake, hilo ni kosa kwa TFF na moja kwa moja imemtosa katika uchaguzi huu. Walichotaka TFF ni kwamba, Abdulkadir hata kama aliona hakutendewa haki katika uchaguzi wa FRAT angekaa kimya ili matakwa ya baadhi ya watu yatimie.
Hii ndiyo aibu nayo;
Eliud Peter Mvella anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 7 (Iringa, Mbeya) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa si mwaminifu kwa kukiuka uamuzi wa pamoja wa Kamati ya Utendaji ya TFF kuhusu mabadiliko ya Katiba.
Ilivyokuwa;
Mvella ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF akiwakilisha mikoa ya Mbeya na Iringa, sasa katika ule mchakato wa TFF kutaka kubadilisha katiba, yeye alikataa kukubaliana na wajumbe wenzake wa kamati ya tendaji. Mtu kutetea haki yake na maslahi ya soka Tanzania, ameondolewa kuwania uongozi TFF.
Kamati ya uchaguzi ya TFF ilitaka Mvella akubali kila kitu kutoka TFF ili mambo ya baadhi ya watu yaweze kwenda. Hii si haki.
MSIMAMO WA MTANDAO HUU;
Abdulkadir na Mvella wameonyesha wao ni watu makini pia ni wawakilishi wa kweli kwa watu wao, lakini kwa kuwa ni wabishi wa kutaka kupelekwa pelekwa tu na TFF wameondolewa katika mchakato wa uchaguzi. Hii ina maana, ukiwa ndani au nje ya TFF unatakiwa kukubali kila kitu kinachotoka au kusemwa na TFF jambo ambalo si sahihi katika nchi ya demokrasia kama Tanzania na hata katiba ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) haielekezi hivyo.
Tunaamini kwa kuwa kamati ya uchaguzi ina watu makini inawezaaa kupitia upya uamuzi huu muda mfupi tu baada ya wagombea hawa walioenguliwa watakapokata rufaa kama wakiona kuna haja ya kufanya hivyo.
hhh
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
umeweza na umbea wako,nabora walivyo kuengua ulivyo na tabia ya kujifanya mjuaji ndio mgeuua kabisa mpira wa tanzania
ReplyDeletehujui mpira wewe... Shaffih angekua mmbeya vp unafatilia blogu yake? Hhhhh.
DeleteWewe wajua mpira ndio maana umeenguliwa kamkatie rufa.Nakama unaona vibaya watu kufatia blog yake kamwabie ifunge.
DeleteTeh!teh!teh!
BMT inanuka, TOC IMEOZA, TFF ndo balaa... Eeeeeh Mwenyezi Mungu tunakuomba utuepushe na huu udhalimu, Wanaopigania haki wape nguvu wasiteteleke kama mlima Sayuni,... Ameeeeen
ReplyDelete.....* HAKI HAIPOTEIN ILA INACHELEWESHWA TU *... Endeleeni kupambana Vijana Ipo siku kila kitu kitakua sawa
Pole sana shaffih...
ReplyDeleteIla broda bado mm cjakuelewa ktk kipengele cha kupotosha umma,hapo kiukwel bro ulichemka baada ya kushndwa drfa kuanza kusema ww hukuenda kwa lengo la kua kiongoz bali ulienda kujua madudu wanayofanya ktk uchaguzi.
Ukwel wamefanya madudu kila mtu kayaona ktk kideo cha clouds ila ww hapo imekulostsha kiukwel.
Ulitakiwa utulie na ungesubil hii season two utupe movie mzma sasa unaona umetukosesha hii season two ambayo ndio tamu zaid?pole sana broda.
Ila komaa kwani strong point sana,lakin tafuta sabab za kutosha kuitetea hyo kasoro 'kupotosha umma juu ya ushiriki wako drfa'
Hzo zlizobak za kawaida....
Dont give up broda.
Dauda alisaha ule usimi"usitukane mkunga uzazi ungalipo"sasa kafanyiwa ananza lalama,bora hakupita huyo enge enda ingiza ujuzi wake na ndio ingekuwa mwisho wa nakufa kabisa mpira TZ
DeleteHiyo ndio TFF siipendi na naihukia sanaa kwa ukorofi na uhuni wao wanaoufanya kwenye kuendesha soka.. Hakika soka letu halitaendelea kwa upumbavu huu unaofanya na TFF, Hivi wanadhani milele watabaki wao?? Hell no, wataondoka tu iwe kwa nguvu au kwa hiari.. "No longer........".
ReplyDeleteHata kama haujaingia kwenye kamati kaka Shaffih endelea kuyatoa yale yanayofanywa na TFF kwani yapo wazi na yanaonekana ila pia kuna vibaraka wanashindwa kuyasema kwa kuogopa kama hayo yaliyotokea.. #Pambana.
Mo de bebeto
ReplyDeletemhhhhhh,hii ndio tff ,ambayo mpaka leo kimbangulile wamenjimwa haki yao,huyo Njamlani ndo fisadi mkubwa alie hua soka temeke,wakati yupo vice president alikua anashinda kufuatilia gate correction ili apate mgao,HAKIKA TUNAUA MPIRA WETU
ReplyDeleteMwalimu Nyerere aliwahi kusema kwamba "sheria na haki ni mambo mawili tofauti kabisa"
ReplyDeleteunajua bwana DAUDA kny msafara wa mamba na kenge wapo ila katika kamat ya uchaguz kenge ni wengi haswa! na ndo wanaoharib mpira wa Tanzania.givi wahusika wa ngaz za juu hili suala hawalion!?!.mpira wetu unakwenda wap!yaan watu wametanguliza maslahi yao tu!vita huwa inaanza hivhiv! watu tumechoka na haya mambo! tunahitaj mabadiliko.kila cku tunawashuhudia akina Gervinho tu, sisi lini?mbona wagen wengi wakija wanashangaa vpaj vya mpira tulivyonavyo?na kwa nini hatufik popote?!?! inaniuma sana
Deleteeeeee m/mungu itokomeze tff na waliomo ndani ya tff,,hivi lini tutakuja kucheza kombe la dunia na sisi tukawemo kwenye ulimwengu wa soka duniani,,tuje kushangilia taifa stars,,na sio bukifaso,,,,,,kwa madudu haya yanakatisha tamaaa kabisa,,kwa watu wenye uchungu na soka la tanzania,,,
ReplyDeleteHII NDIYO TFF NA HUYU NDIYE LAYTO, ila kaka nakumbuka kipindi kile cha uchaguz wa vyama vya soka mikoan wewe na alex mlimsifu sana huyo LYATO, kaka kumbuka friji bovu hujulikana wakat wa joto, LYATO NI BONGE LA CHUI ILA SEMA TU JAMAA KAVAA NGOZI YA KONDOO
ReplyDeletePole mkuu.Tuko pamoja.TFF=CCM
ReplyDeleteDavid V
HII NDIYO TFF NA HUYU NDIYE LYATO THE BIG BOSS, kumbeni mlimsifu sana wakati wa chaguzi za mikoa na mkasahau ya kuwa "friji bovu hujulikana wakati wa joto kali" haya joto limepanda jamaa kaonesha madhaifu yake, neno 1 la kuzingatia ni kwamba "HATA USKU UWE MREFU KIASI GANI LAKIN ASUBUHI LAZIMA IFIKE" IPO SKU TU YAJA HAWA VIBARAKA YATAWATOKEA PUAN
ReplyDeleteTZ NI ZAIDI YA UIJUAVYO! NAFIKIRI HII NAYO YAHITAJI MAANDAMANO MAANA AMANI HAIJI ILA KWA NCHA YA UPANGA.
ReplyDeleteHivi huyu Michael Richard Wambura ana dhambi gani kubwa inayomfanya akatwe kila anapogombea nafasi ya kuongoza michezo?Kwanini wadau hawajulishwi?Lakini kama ana mabaya yaliyochupa mipaka kwanini wapiga kura hawapewi nafasi ya kumkataa?Kama woga ni kwamba wanatampa hao wanaomkata hawaoni kwamba wanawanyima wenye dhamana ya mpira chaguo lao?Nadhani muda wa mizengwe na ukosefu wa uwazi unabidi vifanyiwe kazi na hii Movie ya "Kukatwa Wambura" ambayo pengine wakipewa watu wa Bongo movies wanaweza kutoa part hata 10 iishe
ReplyDeleteShaffih,
ReplyDeleteinawezkana unayosema ni sahihi kabisa lakini tatizo ninaloliona mimi ni kutumia chombo chako cha habari kutoa malalamiko----naamini huwezi kubalance habari.
Pole sana dogo
duh TZ..kwa fitna yaani kuanzia bungeni mpka URAIANI,michezoni,makanisani and misikitini,shafii na wambura kwa ninavyoijua bongoo hamtapata nafasi tenaaa mpka wafe waliotia zengwee wote...
ReplyDeletePOLENI...
ndugu zangu wambura na shafii hapo mpaka wazee wa zengwe wafe ndo mtapata NAFASI ktk michezo bongo,hii nchi ishauzwa kila kikundi kimehold sehemu yake,ufisadi from bungeni mpka michezoni OOOH lord of mercy...
ReplyDeletepoleni.
jamani dauda nawe ukishindwa tuhuma kibaoooooooooo, we sawa na wanasiasa wakishindwa kuhama vyama vyao na kwenda vyingine wakidai kule kuna madudu hivyo sio vyema walikkujua toka awali kaka we mmbea kama mwanamke walishakusoma. Acha umbea uone kama hawatakuchagua. UMBEA WATU HAWAPENDI
ReplyDeletebaadhi ya watendaji wa tff ni hatari kuliko kirusi cha ukimwi.wamejaa tamaa,wivu,majungu,fitina na unazi.wapo pale kwajil ya maslahi binafsi na kupanga matokeo.kamwe soka la nchi hii halitabadilika
ReplyDeletekwani dauda unatka TFF ya nn,umeambiwa kuna nn huko,tulia na ajira yako unaweza kutafuta kitu cha kukutoa ukiwa huko huko......au una taka umaarufu/shortcat ya ubunge/tafuta ur own njia sio laim hii...............wambura nae nunda,mwmbie imetosha afanye yake
ReplyDeleteHAo ndo TFF ki ukweli demokrasia hapa nchini bado ipo makaratasini waache watu waamue sio wachache kwa mfano Michael Wambura kila sehemu wanamtenda hiv alichokifanya kibaya nchi ndugu yetu Wambura nini? Alafu pia hawa kina Lyato wanajua wkiweka watu wano jua mambo wataumbuliwa hivyo ndugu Shafii usikate tamaa endelea kuwatikisa mwishoe watang'ooka tu
ReplyDeleteTFF pale mizengwe ni mingi sana. Nia ya dhati ya kulikomboa soka letu la bongo hakuna. Watu pale wamejijengea ka syndicate kao ili wawe wanakula pesa tu na kurithisha viongozi watakaolinda maslahi yao tu. Ni kama serikali ya CCM tu inavyofanya. Hakuna jipya hapo. Huku chama chetu cha mpira kimejaa mamburula tupu na mpira kamwe hautaendelea namna hii. Wizara ya michezo na serikali kwa ujumla nadhan kama haitafanya jambo la kuingilia hata kama FIFIA inakatza, soka letu kamwe halitaendelea.
ReplyDeleteMi nadhani ifike mahali hizi kamati za vyama za michezo Tanzania zione aibu na kuiga mazuri(benchmarking) toka kamati ya vyama vingine vya michezo na taasisi zake ili soka la tanzania likue na michezo mingine iwe katika kiwango cha kimataifa,wafike mahali viongozi wa taasisi hizi waachane na siasa za kibinafsi na waangalie maslahi ya taifa,mi sijaona sababu za kumwondoa shaffii dauda na hao wagombea wengine kwenye mchakato wa kugombea hizo nafasi,kaka mi naomba usiishie hapo hata kama haitakua leo hakika kesho itawezekana ,siku hazifanani,wapenda mabadiliko ya michezo Tanzania tupo pamoja nawe.
ReplyDeletenyie mnao mponda shaffih wote wajinga,kuna watu hapa tff wamekaa miaka kibao katika uongozi wa mpira hakuna manufaa yoyote zaidi ya kujinufaisha matumboa yao tu,sasa kuna watu ni wasema kweli na wanataka kugombea ili kuleta mabadiliko ktk soka lazima muelewe,kwa hio hawa watu hawatakiwi kule tff kwa kua watafichua maduu yao ndio maana hawatakiwi,,mi naamini shaffih kama akigombea atashinda na ndio uovu wa tff utaanza kufichuka,
ReplyDeleteMimi bado siungi mkono Shaffih kugombea Uongozi pale TFF, sio kwamba namchukia dauda la hasha na mimi ni mfatiliajia sana wa vipindi vya dauda na namkubali sana hapo alipo ila kwenda TFF hapana siungi mkon kabisa , Samahani kwa nitakaowaumiza. Dauda anafit hapo alipo kama presenter na si kama kiongozi afu mi hii kasumba ya kujipatia umaarufu kwenye media ili kugombea uongozi huwa siipendi kabisa na ndio maana napenda dauda aendelee huku alipo na kule awaachie wengine.Hatuwezi wote tukawa viongozi bwana tugawane majukumu sasa kila alie kaibu na fani flani lazima agombee? mwone michael Maluwe alikua bonge la presenter wa michezo leo yupo wapi sijui ni nani uko kwenye nasket ball sasa kama lengo la hawa young presenter kupata umaarufu ili kugombea TFF mi ntaanza kuwaona wanasiasa na mi si wapendi sana wanasiasa. Shaffih we tuendelee tu huku au usubiri mpaka muda wako ufike na sio kulalamika kwenye media zako bila kujua upande wa pili wanasemaje ..........078567082***
ReplyDeletePOLE SHAFII,
ReplyDeleteKUMBUKA KWAMBA MDOMO HUPONZA KICHWA.kama ulikuwa na nia hiyo ungetulia kwanza hadi utimize malengo yako ndio uibue madudu ukiwa ndani ya system.
Kuhusu Wambura,hana jipya atakuja kuvuruga soka letu kwa kulipiza visasi kwani ameumizwa miaka mingi.
Brother Wambura Jipange kwa inshu zingine,mbona town dili kibao sio lazima TFF.