Wachezaji wa Stars - Mbwana Samatta, Chuji, Kaseja na Mwinyi Kazimoto wakipongezana baada ya ushindi dhidi ya Cameroon. |
Juma Kaseja akimpa pongezi Samatta baada ya mechi |
Mrisho Ngassa vs Assou Ekotto - Mtu aliwekwa mfukoni leo |
Samagoal na Assou Ekotto shughuli nyingine ilikuwa leo |
Mrisho Ngassa vs Assou Ekotto shughuli ilikuwa pevu leo kwa Ngassa |
Mchezaji wa Cameroon akitolewa nje ya uwanja kutibiwa baada ya kupata maumivu |
Amri Kiemba langoni mwa Cameroon |
Mshikemshike wa Samatta na beki wa Tottenham Hotspur Assou Ekotto |
Wachezaji wa Stars wakishangilia goli lao |
Frank Domayo alipiga mpira mwingi sana |
It was amazing performance,stars deserved to win
ReplyDeleteHuyo kocha Mdenish namkubali sana habadilishi kikosi ameshaunda kikosi cha kudumu hii ndio inavyotakiwa, leo hii ukiitaja first eleven ya Taifa Stars inajulikana ni nani wanaiunda na reserve wake, sio kama Maximo kila kukicha timu mpya, akawa haeleweki wachezaji wa kutegemewa kama akina Kaseja, Maximo anawaacha.
ReplyDeleteKuna watu wanaobeza mafanikio ya timu yetu ya Taifa kwa sasa na wanadhani hakuna hatua yoyote inayofikiwa na timu yetu na kuhusudu tu michezo ya ughaibuni! Huenda wako sawa lkn wanasahau kuwa mafanikio kama yaliyofikiwa na timu kadhaa barani Afrika yalianza hivihivi. Kwa kweli kwa sasa Timu yetu ya Taifa inacheza mpira unaoeleweka. Tangu jinsi wanavyoposses mpira wana vitu ambavyo ungependa kuviona Mf. chenga aliyopiga Kiemba kwenye mechi ya jana ni wachezaji wachache hata ulaya wenye ujuzi huo! wanaposhambulia unaoma kweli wanatafuta goli n.k. Kwa mwendo huu hatuko mbali na Ethiopia na Cape verde na tuongeze tu sapoti kwa wachezaji wetu na kuwapa moyo mafanikio yanakuja! Hongera Kim na Marshi kazi mnayofanya inaonekana! wachezaji msibweteke kazeni uzi kwani wengi wenu bado umri unaruhusu kufanya makubwa! Mungu awabariki sana kwa kazi nzuri na kutupa raha sisi tulio wazalendo na taifa letu. NURU SPORTS MSM!
ReplyDeleteahsantenin stars kazi nzuri tumeiona damu changa tgemeo la kesho kutengeneza timu bora zaidi walicheza vizuri pasi zilionekana na walistahili kushinda chamsingi ni kuwaomba viongozi wa soka waweze kuendeleza vipaji na sio kuvitupa vipaji hapo tutafika.
ReplyDeleteHakuna jambo linalofurahisha kama ushindi! Timu ilicheza vizuri sana, ilicheza kitimu ikianzia mashambulizi nyuma ilisukuma mipira mbele kwa mpango uliyoonekana dhahiri ila ilikuwa na upungufu mdogo tu kwenye umaliziaji wa mipira ya mwisho.
ReplyDeleteTimu yetu inakiwango cha kuvutia kwa sasa kizuri zaidi ina vijana wadogo wengi wenye nafasi ya kuitumikia timu kwa kipindi kirefu kama watakuwa na nidhamu hasa kwenye swala la kutunza na kukuza viwango vyao. Nawapongeza sana na kuwatakia kila lakheri kwa siku za usoni.
Shaffih kama inawezekana tunaomba pia uwe unatuwekea video clips coz sisi tulio mbali (ughaibuni)tunahisi kudhurumiwa. hatufaidi kabisa mbali na wewe kutujuza kwa njia hii. Big up sana mzee.MIYAGAJr (BELGIUM)
ReplyDeleteHatupaswi kumjadili Maximo,kwa kuwa hakuwa anafikiri kitanzania. Na ndio kilichommaliza, "ukikaa na waongo ongopa kwanza,wakukubali,ndio uanze kusema ukweli".
ReplyDelete