Biashara ya kusafirisha bianadamu ambayo kwa hapa nchini imekuwa ikionekana kutajwa kufanyika kwa baadhi ya wahamiaji haramu kutoka nje kupewa hifadhi na wazawa kwa njia za magendo pamoja na ile ya nchi kutumika kama njia ya wahamiaji kupitishwa kuelekea nchi za kusini mwa Afrika, sasa biashara hiyo imehamia kwa vipaji vya soka nchini Tanzania kutoroshwa kwenda nchi jirani.
Jijini Mwanza Mchezaji mahiri wa zamani wa timu za Pamba Fc na Kagera ambaye pia alikuwa kocha wa kituo cha timu ya vijana wadogo ya Alliance Academy ya jijini humo Furgance Novatus ametiwa mbaroni kwa kuhusishwa na tuhuma za kuuza vijana watatu nchini Uganda kwa thamani ya Shilingi milioni 60 za kitanzania...
Bofya play sikiliza zaidi kisa hicho...
Bofya play sikiliza zaidi kisa hicho...
Hati ya kusafiria ilionyesha kuwa
anaitwa Abdulatif Mohamed badala ya Abdalah Juma
|
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa,Mkurugenzi wa
shule ya Alliance Academy James Bwire (pichani) alisema kuwa timu yake ya wachezaji chini
ya miaka 15 ilialikwa kwa ajili ya kushiliki michuano ya soka nchini Uganda na
kufanikiwa kutwa ubingwa hivi karibuni.
Bwire alisema kuwa baada ya kumalizika kwa michuano hiyo
viongozi kadhaa wa soka nchini Uganda pamoja na Waziri wa michezo wan chi hiyo
walivutiwa na uwezo wa wachezaji wake watatu ambao ni golikipa Calvin
Richard(16), mshambuliaji Athanas Mdaulu(16) pamoja na mchezaji wa kiungo
Abdallah Juma(15) na kuuomba uongozi kuwaruhusu kubaki nchini Uganda kwa ajili
ya kuchezea katika timu za watoto za nchi hiyo.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa alikataa maombi ya waganda hao
na kuwaeleza kuwa alikuwa nchini humo kwa ajili ya kushiliki michuano ya soka
na sio kuwauza wachezaji na kuwataka viongozi hao kama kweli wana nia hiyo
kuwasiliana na wazazi wa wachezaji hao.
Lakini hatimaye Waganda hao walifanikiwa kuchukuwa mawasiliano ya kocha Fulgence
Novatus aliyeingia 'kingi' na kucheza mchezo huo mchafu.
|
No comments:
Post a Comment