Search This Blog

Friday, February 22, 2013

DOLA 5000 ZA ASAMOAH KUWAPELEKA YANGA FIFA

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limesema linapeleka rasmi madai ya mchezaji wa zamani wa Yanga, Kenneth Asamoah kwenye chombo chake cha utatuzi wa migogoro (Dispute Resolution Chamber) baada ya klabu hiyo kutojibu chochote.

Awali FIFA ilipokea malalamiko ya Asamoah kuwa anaidai Yanga dola 5,000 za Marekani ambapo ilikuwa ni sehemu ya malipo yake (signing fee) baada ya kujiunga na klabu hiyo.

Desemba mwaka jana FIFA iliiandikia barua Yanga kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikitaka maelezo yake kuhusu madai hayo ya Asamoah, lakini hadi sasa haijajibu madai hayo.

Kwa mujibu wa FIFA, hatua ya uchunguzi wa suala hilo umekamilika, na sasa linapelekwa rasmi katika chombo chake cha utatuzi wa migogoro (Dispute Resolution Chamber) kwa ajili ya kufanya uamuzi.

3 comments:

  1. Hawa Yanga ipo siku watakuwa kama Juventus maana kila siku wao hupelekwa fifa tu .
    Daraja la nne litawahusu.

    ReplyDelete
  2. yaani mbwembwe zote hizo kumbe hata hela ya usajili hawakumpa! wakamtafute malikia wa nyuki awalipie! shwaini hawa!

    ReplyDelete
  3. Hapo ndio ninaposema timu za tanzania ( big two) zimejaa ubabaishaji, hakuna viongozi wenye taaluma ya uongozi katika masuala ya michezo.Ni aibu dola 5000!!! ni image gani twajenga!! viongozi wamebakiza sifa kwa washabiki na mambo binafsi.
    Hv ikitoka amri ya kuishusha daraja yanga -TFF mtatekeleza !!!!

    ReplyDelete