YANGA inashuka uwanjani Jumatano kuikabili African Lyon, lakini Azam inampa presha kubwa kocha Ernest Brandts ambaye ameagiza wachezaji wake kuhakikisha wanaishushia mvua ya mabao Lyon ili kuwadhibiti wana lamba lamba hao.
Azam iliibamiza Mtibwa Sugar jana Jumapili mabao 4 – 1 na kukabana koo na Yanga kileleni. Timu zote hizo zina pointi 33, lakini Yanga inaongoza kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa wakati Simba bado inachechemea katika nafasi ya tatu baada ya kulazimishwa sare yabao 1 – 1 JKT Oljoro Jumamosi iliyopita jijini Arusha.
Brandts amesema kuwa ligi sasa imefikia patamu na hakuna kudharau timu hata moja ingawa kasi wanayokuja nayo Azam ni kubwa na inamuogopesha katika harakati zao za kutwaa ubingwa ingawa amedai kuwa atawatuliza tu na Yanga itakuwa bingwa msimu huu.
Kocha huyo raia wa Uholanzi amewaambia wachezaji wake wajifunze kutokana na matokeo wanayopata Simba hivi sasa kwa kutambua kuwa sasa ni muda wa kazi na wanatakiwa kujituma zaidi ili kusaka amafanikiop.
“Nafurahi matokeo ya Simba kwa sabbau ni moja ya wapinzani wetu wakubwa ingawa Azam nao wanakuja spidi hivyo lazima tujihadhari maana wameamsha mapambano makali ambayo hatuna budi kuyashinda.
“Matokeo ya Simba kuna kitu yanatufunza , Lazima wachezaji wanatakiwa wajitume na kuiacha mbali ikiwa kushinda kila mechi. Hakuna mechi rahisi kwani hivi sasa kila timu inakomaa haitaki kufungwa ingawa mikakati yetu ni kuhakikisha tunashinda na kutangaza ubingwa mapema” alisema Brandts.
Aliongeza” Tunacheza na African Lyon Jumatano( kesho) hatuwezi kuwadharau licha ya wao kupoteza michezo yao yote ya raundi hii lakini hii ni soka wanaweza wakaja wakabadilika na ukizingatia kuna wachezaji wane walitoka kwetu hivyo haitakuwa mechi rahisi.
“ Lakini nasisitiza kwa wachezaji wangu hasa washambuliaji kuhakikisha tunashinda mchezo huo tena kwa mabao mengi ili kupambana na Azam kileleni” alisema Brandts.
Vita ya ubingwa imeonekana kupamaba moto katika timu tatu Yanga, Azam na Simba ingawa wekundu hao wa Msimbazi wameonekana kuchechemea katika mbio hizo.
Ingawa Yanga inaonekana ina ahueni zaidi katika michezo yake 11 iliyobaki kwani mechi sita ndio zinaonekana zitaipa shida timu hiyo katika harakati zake za kuwania ubingwa wakati Azam ina mechi saba ngumu pia wakati Simba ndio ina kazi kubwa zaidi kwani ina mechi tisa ngumu.
Yanga ina mechi ngumu dhidi ya JKT Ruvu, Azam, Kagera Sugar, JKT Oljoro, Coastal Union na Simba ingawa inapata haueni kwani mechi nyingi inacheza kwenye Uwanja wa nyumbani wakati Azam ina kazi dhidi ya JKT Ruvu, Yanga, Ruvu Shooting, Simba, Coastal na Oljoro na Mgambo Shooting.
Simba yenyewe itabidi ifanye kazi ya ziada kuziadabisha Prisons, Ruvu Shooting, Mtibwa Sugar, Coastal Union, Kagera, Azam, Toto, Mgambo Shooting na Yanga kama kweli inataka kutetea Ubingwa wake
No comments:
Post a Comment