Young Africans leo asubuhi imemaliza mazoezi yake kwa kufanya
mazoezi ya kujenga mwili na uimara (Gym) iliyopo katika hoteli ya Fame
Residence leo asubuhi na yakiwa ndio mazoezi ya mwisho katika kambi ya
mafunzo ya wiki mbili iliyokuwa ikiendelea katika viwanja vya Fame
Residence Football mijini Antlaya.
Kocha mkuu Ernest Brandts akishirikiana na Fred
Felix Mizniro na Razaki Siwa leo waliongoza mazoezi ya Gym kuanzia
majira ya saa tatu na nusu asubuhi mpaka majira ya saa saa tano na nusu
asubuhi ambapo baada ya mazoezi hayo wachezaji wamepewa nafasi ya
kupumzika kujiandaa na safari ya hapo kesho kurudi Tanzania.
Akiongelea
michezo ya kirafiki mitatu waliocheza na timu za Armini Bielefeld,
Deinizlispor na Emmen Fc kocha mkuu wa Yanga Ernest Brandts amesema
michezo ilikuwa ni mizuri na wamepata nafasi ya kuona mapungufu machache
yaliyojitokeza na anaamini watayafanyia kazi na kuendelea kufanya
vizuri.
Tumecheza michezo mitatu, wa kwanza
tulitoka sare na Amrinia Bielefeleld, mchezo ulikua mzuri na timu yangu
ilicheza vizuri kwa dakika 90 zote za mchezo licha ya Arminia
kusawaisha bao dakika za lala salama huku mwamuzi aklishindwa kutoa
maamuzi sawa na mshika kibendera wake, ambapo mfungaji alikua maeotea.
Mchezo
wa pili dhidi ya Denizlispor nao pia timu ilicheza vizuri na kuweza
kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini umakini wa washambuliaji
ulitukosesha ushindi kwani Tegete alitumia nafasi aliyoipta kufunga bao
la mapema kabla ya Waturuki hawajasawazisha kwa bao la utata kisha
kupewa penati ya utata pia.
Mchezo wa mwisho dhidi
ya Emmen FC ulikuwa mzuri pia na kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza
tuliutawala mchezo na kupata nafasi kadhaa za kufunga mabao lakini
kutokua makini wa washambuliaji wetu pia kulichangia sisi kukosa
ushindi, kabla ya kipindi cha pili Emmen FC kucharuka na kupata mabo
mawili ya haraka haraka kutokana na uzembe wa walinzi na mlinda mlango
Yusuph abDUL
Tunaushukuru uongozi kwa kukubali
kutupa nafasi ya kuweka kambi Uturuki, tumkeaa pamoja kwa mda mrefu huku
tukitoka mafunzo kwa vitendo, vifaa na mahitaji yote vikiwepo ,kukiwa
na hali ya utulivu, kifupi tumejifunza mambomengi sana ya msingi ambayo
yatatusaidia kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya
Vodacom na mashindano yatakayotukabili alisema 'Brandts'
walete vibonde wa uturuki ,hakuna la maaana walilofanya huko,sanasana kuonyesha maji ana hela basi,kiufundi hakuna lolote,nadhani simba watakuwa wamelenga ukizingatia wanamechi za kimataifa itakuwa exposure nzuri kwao!njooni tucheze chandimu letu jamhuri basi ,hizo ni kelele tu!hakuna kitu,poleni sana!!!
ReplyDelete