Azam FC yatwaa kwa mara ya pili Kombe la Mapinduzi
Goli la mshambuliaji Gaudence Mwaikimba wa Azam FC limeipa ubingwa wa
Kombe la Mapinduzi kwa mara ya pili mfululizo timu hiyo katika mchezo wa
fainali ulimalizika kwa Azam FC kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Tusker FC ya Kenya.
Azam FC imeweza kutetea kombe hilo na kilibakisha nchini katika mchezo
ulitumia dakika 120 kumalizika kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani
Zanzibar.
Mabingwa hao kwa mara ya pili walipewa medali za
dhahabu, kombe na kitita cha shilingi milioni kumi kama zawadi ya kutwaa
ubingwa huo.
Katika mchezo huo kipindi cha kwanza kilimalizika
kwa timu zote bila kufungana, kipindi cha pili Tusker walianza kupata
bao kupitia kwa mchezaji Jese Were aliyetumia uzembe wa beki ya Azam FC
katika dakika ya 59.
Azam FC kupitia kwa beki wake mpya Jockins
Atudo alisawazisha goli hilo kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa
Tusker Luke Ochieng kunawa mpira wakati akizui mpira wa kichwa uliopigwa
na Mwaikimba, penati ilimriwa na mwamuzi Ramadhan Kibo.
Goli hilo la kusawazisha kwa Atudo, ni goli lake la nne katika mashindano hayo, akifuatiwa na Mwaikimba mwenye magoli mawili.
Matokeo ya sare ya 1-1 yalimaliza dakika 90, katika dakika za nyongeza
Mwaikimba alitumia vema nafasi aliyoipata katika dakika ya 92 na
kupachika goli hilo wavuni na kumaliza mchezo Azam FC ikitwaa ubingwa
kwa ushindi wa 2-1.
Baada ya goli hilo Azam FC walituliza mpira chini na kucheza mtindo wa kulinda lango lao kwa muda wote wa dakika 28 zilizobaki.
Katika mchezo wa leo Azam FC walifanya mabadiliko mawili, walitoka
Uhuru Seleman dk 64 nafasi yake ikachukuliwa na Abdalah Seif na dk 126
aliingia Malika Ndeule kuchukua nafasi ya Brian Umony.
Tusker
walifanya mabadiliko walitoka Fredrick Onyango, Andrew Tololwa, Jese
Were, Khalid Aucho na Ismail Dunga nafasi zao zikachukuliwa na Mark
Odhiambo, Edwin Ombasa, Andrew Sekayambya, Benson Amianda na Michael
Olunga.
Baada ya kutwaa Kombe hilo, kocha mkuu wa Azam FC
amewapongeza wachezaji wake kwa kubakisha kombe hilo na kusema ni
muendelezo wa mipango ya mafanikio katika klabu hiyo.
Amesema
safari inaendelea ya kupeleka makombe katika klabu hiyo, walianza na
Mapinduzi 2012, Ngao ya Hisani walilochukua nchini Congo DRC na hili la
Mapinduzi 2013.
Kikosi cha Azam FC kilichotwaa ubingwa, Mwadini
Ally, Himid Mao, Samih Haji Nuhu, David Mwantika, Jockins Atudo,
Michael Bolou, Humprey Mieno, Khamis Mcha, Gaudence Mwaikimba, Uhuru
Seleman/Seif Abdalah 64’ na Brian Umony/Malika Ndeule 126’.
Wengine waliokuwa na kikosi hicho, Aishi Salum, Wandwi Wiliam, Luckson
Kakolaki, Omary Mtaki, Abdi Kassim ‘Babi’, Jabir Aziz, Ibrahim
Mwaipopo,Salum Abubakar, Tchetche Kipre kabla ya kuumia, waliokosa
mashidano hayo ni Abdulhalim Humud, John Bocco, Waziri Salum ambao ni
majeruhi. (SOURCE: AZAM FC PAGE ON FACEBOOK)
No comments:
Post a Comment