Search This Blog
Tuesday, January 15, 2013
YANGA KUKIPIGA BLACK LEOPARD YA AFRIKA YA KUSINI JUMAMOSI UWANJA WA TAIFA
Katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako (kushoto) akiwa na mwakilishi wa Prime Time Promotion Shaffih Dauda (kulia) wakizungumzia mchezo wa jumamosi dhidi ya Black Leopardrd ya Afrika Kusini
Timu ya Young Africans Sports Club inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Black Leopard ya Afrika Kusini, mchezo utakaofanyika siu ya jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akiongea na wandishi wa habari, mwakilishi wa Prime Time Promotions Shaffih Dauda amesemam timu ya Black Leopard inatarajiwa kuwasili siku ya alhamisi ikiwa na msafara wa watu 37 wakiwemo viongozi na wachezaji.
Black Leopard ni timu nzuri, inashiriki ligi kuu ya Afrika Kusini ipo katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi hyo PSL, hivyo tunaaamini utakua mchezo mzuri kwa Yanga, ukizingatia walikuwa kambi ya mafunzo ya wiki mbili nchini Uturuki hvyo itakua ni fursa kwa wapenzi, washabiki na wanachama na wapenda soka kwa ujumla kuona soka la wana jangwani alisema 'Shaffih'
Kuhusu viingilo vya mchezo huo ni VIP A 30,000/=, VIP B 20,000/=, VIP C 15,000/=, Orange 7,000/= na Blue & Green 5,000/=
Kocha Mkuu Ernest Brandts (kulia) akwia na Afisa Habari wa klabu wa Yanga Baraka Kizuguto (kushoto) wakiongelea juu ya ziara yao ya mafunzo nchini Uturuki
Aidha kocha mku wa Yanga Ernest Brandts ameongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu kuhusiana na ziara ya mafunzo ya wiki mbili mjini Antalya nchini Uturuki.
Brandts amesema anashukuru kwa uongozi kwa kuweza kuwapa nafasi ya kufanya kambi ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacom kwani uwepo wao Uturuki kwa pamoja wamepata nafasi ya kuiunganisha timu kw apamoja.
Unajua mzunguko wa kwanza wa ligi timu sikukaa nayo kambini kwa ajili ya maandalizi ya ligi ila kwa sasa nimepata nafasi ya kukaa nao kuongea na kuwafunza kwa pamoja, mazingira ya kambi yalikuwa mazuri na huduma nzuri hviyo madhumuni yetu ya kuweka kambi ili kujiandaa yamekwenda vizuri alisema 'Brandts'
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment