Search This Blog

Tuesday, January 15, 2013

BREAKING NEWS: EMMANUEL OKWI AUZWA KWA DOLA LAKI 3 ETOILE DU SAHEL YA TUNISIA

Sakata la mchezaji wa kimataifa wa Uganda anayeichezea klabu bingwa ya Tanzania Bara Simba SC, Emmanuel Okwi kwenda kujiunga na kambi ya Simba iliyopo nchini Oman limefikia mwisho.

Kwa taarifa za ndani kutoka ndani ya klabu ya Simba ni kwamba timu hiyo imefikia maamuzi ya kumuuza mshambuliaji huyo kwenda Etoile du Sahel ya Tunisia kwa ada ya uhamisho itakayovunja rekodi ya uhamisho hapa nchini ya $300,000.

Mwenyekiti wa klabu hiyo ya Simba Mh. Aden Rage kwa sasa yupo nchini Tunisia akisimamia taratibu zote za uuzwaji wa Okwi ambaye alisaini mkataba mpya wa kuitumikia Simba hivi karibuni.

"Ni kweli Mwenyekiti yupo Tunisia akishughulikia uuzwaji wa Okwi kwa klabu ya Etoile du Sahel. Ada ya uhamisho ni dola laki tatu na muda mchache ujao dili litakamilika na Okwi atapewa ruhusa ya kuzungumza maslahi binafsi na klabu yake mpya." - kilisema chanzo cha habari kutoka ndani ya Simba.

Etoile du Sahel ni klabu mojawapo yenye mafanikio makubwa barani Afrika, ikiwa inashikilia rekodi ya kuwa klabu pekee barani afrika kushinda kila kombe linaloandaliwa na CAF.

Kwa taarifa zaidi kuhusu ukamilikaji wa dili hili endelea kutembelea tovuti hii.

4 comments:

  1. Woe!good news he is good player, all the best hero!

    ReplyDelete
  2. Hivi vihela vidogovidogo sio mbaya! lakini haviwezi kuwa vya kudumu kama, ubabaishaji utakuwa huuhuu!Mipango madhubuti ni muhimu,mbona hata hatujachelewa jamani? Tunataka uwanja wetu "Uwanja wa Simba Sports Club","Taifa Kubwa Stadium", usanii wa kuchezea akili zetu tumechoka,uza hata wachezaji wote,hata tukirudishwa daraja la kwanza! lakini mipango ya uwanja iwe namba moja! Mkiwa tayari kwa hilo ndio nitarudi tena Simba!

    ReplyDelete
  3. Iko poa, atafutwe mbadala mwingine atakayeiziba vyema nafasi yake....

    ReplyDelete