Search This Blog

Thursday, January 3, 2013

WATU WA MPIRA NI KINA NANI ?

Education is a passage to a self determination(Raphael D.D, Problems of Political Philosophy 2nd edition, London: Macmillan Education Ltd,1976, p.32).The aims of education are basically the full development of individual’s personality, talents, and abilities, and enabling of all persons to participate effectively and responsibly in a free society (Hodgson Douglas, Human Right to Education:Aldershot:Ashgate Publishing Co, Ltd, 1998, p.18). “…if any of the young men and women who are given education by the people of this Republic adopt attitude of superiority, or fail to use their knowledge to help the development of this country, then they are betraying our Union.”(Julius K. Nyerere, 12th  May 1964).
                                                                                              [Msisitizo ni wa Kwangu]
Nukuu ya  kwanza inaeleza kuwa elimu ni njia ya mtu kujitambua na elimu ulenga kuendeleza utu wa mtu, vipaji na uwezo na kuwezesha watu wote  kushiriki  kisawa sawa na kuwajibika katika jamii huru.
Nukuu ya pili inatoka kwa Hayati Baba wa Taifa, pamoja na mambo mengine anatuhamasisha vijana tuliosomeshwa kwa kodi ya Watanzania kutokuwa na majivuno ya Elimu bali tutumie elimu yetu kwa maendeleo ya nchi yetu(Tanzania), tofauti na hapo tutakuwa wasaliti.  Maendeleo aliyosema Baba wa Taifa ni ya kila idara katika nchi hii, hakusema kuwa kuna idara ambayo utaalamu wa elimu hauhitajiki. Nashawishika kusema kuwa Baba wa Taifa alimaanisha kuwa Elimu ni jambo kubwa muhimu kwa maendeleo katika  nyanja yoyote.
Nukuu hizi zinalenga kueleza umuhimu wa elimu na nini watu wenye elimu wafanye kwa jamii zao  zilizotumia hela kuwasomesha.
Naandika makala hii baada ya kuhuzunishwa na nasaha za aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa chama cha soka mkoa wa Dar-es-salaam(DRFA) ndugu JUMA SIMBA “GADDAFI” akiwaasa wajumbe wa mkutano wa uchaguzi kuwa wanapaswa kuwa wanawapa kipaumbele watu wa mpira katika uchaguzi wa vyama vya mpira, eti wasomi hawawezi kuleta maendeleo katika mpira.
Kwa kujiamini ana amasisha kuwa wasikubali watu wenye stashahada, Shahada ya kwanza, Shahada za uzamili na uzamivu waongoze mpira/soka. Nilipatwa na mshangao kuwa huyu  kweli ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa DRFA?
Pole wasomi mliojaribu kugombea maana kumbe mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi alikuwa tiyari na upande katika uchaguzi yaani upande wa watu ambao hawana elimu. Na hili linathibitika hata katika hatua za awali kwa  baadhi yenu majina  kuondolewa kuwa mmekosa sifa,, ingawa walitaja kuwa mmekosa uzoefu ukweli ni kwamba kasoro mliokuwa nayo ninyi mna stashahada/diploma ama shahada/degree n.k(Yaani kuwa na elimu ilikuwa ni kukosa sifa) Yaani watu waliokuwa wanahitajika ni wale WASIOKUWA NA ELIMU ambao Mzee JUMA SIMBA “GADDAFI” anawapamba kwa kuwapachika jina la WATU WA MPIRA.
Inatia huruma sana, Tunaelekewa wapi Tanzania? Kama mtu mwenye kuaminiwa kupewa sifa ya uenyekiti wa kamati ya uchaguzi tena DRFA ana mawazo kama hayo. Sitaki kuamini kama Baba GADDAFI ndo uelewa wake unaishia hapo,, Siamini kwa sababu kuna watu waelewa lakini wanajifanya wajinga ilimradi wawafurahishe watu fulani.  Hawa watu wapo Tanzania hii,, PROFESA kujitia ujinga ilimradi amfurahishe mwanasiasa tena mwenye elimu ya darasa la saba la miaka ya tisini(Kheri la saba la mkoloni).(WATANZANIA si mnamkumbuka Yule PROFESSA aliyekuwa rafiki wa mahakama(amicus curie) katika lile shauri la  mgombea binafsi?)Yawezekana Mzee JUMA SIMBA “GADDAFI” ulifanya hivyo hili umfurahishe Yule aliyewekewa pingamizi na SHAFFII DAUDA kwa kuwa hakuwa na elimu inayohitajika  au ulifanya hivyo hili umfurahishe MZEE BAKHARESA ambaye ilithibitika kuwa hana elimu ya kidato cha Nne,.. Au walikushawishi ufanye hivyo? Kumbuka Baba wa Taifa aliwahi kusema kuwa  na nakuu
…mtu mjinga akijua kuwa wewe una akili timamu lakini akakupa wazo la kijinga na akijua kuwa unajua kuwa hilo ni wazo la kijinga na ukalikubali… huyo mtu atakudharau..
Basi hao watu kama kweli walikushawishi na kukupa wazo la kijinga nawe ukalikubali jua basi wamekudharau, tena sana. Yawezekana mawazo ni ya wao hao WATU WA MPIRA (WASIOKUBALI ELIMU KAMA MSINGI WA MAENDELEO), na maneno ni yao  ila sauti ndio ikawa ya kwako.(Yaani wamekutumia kuongea yaliyo akilini mwao na si wewe kuongea yaliyo yako).   Mawazo yangu yanatokana na huu ushahidi uliotolewa na mwenyekiti mpya wa DRFA. Kuna uwezekano mwenyekiti mpya  wa DRFA wala hakuwa na mpango wa kugombea nafasi hiyo lakini  WATU WA MPIRA  walimshawishi  kuwa agombee na kumhakikishia kuwa  atakuwa mwenyekiti wa DRFA na wakainjinia huo mpango mpaka ikawa hivyo, maana yake mwenyekiti mpya wa DRFA hataweza kufanya kinyume na matakwa ya Mzee BAKHERESA aliyemuahidi na ikawa hivyo. Hivyo basi maneno na mipango yote ya DRFA inaweza kufanywa na Mzee BAKHARESA ila msemaji akawa mwenyekiti MPYA, Yaani mwenyekiti mpya anaweza kutumiwa.
Au kweli ndio msimamo wako? Kama kweli ni msimamo wako Baba, Please sir get out of that shell? Kumbuka kuwa ulipewa dhamana kubwa sana hivyo epuka sana cheap arguments.
Kama kweli ndio msimamo wako, BABA unakosea sana,, kulingana na maneno yako ulimaanisha uongozi wa mpira unapaswa uwe chini ya watu wasio na elimu ambao ulijaribu kulemba hiyo category na kuipachika jina la WATU WA MPIRA.
 Nimejaribu kutafsiri ni yupi MTU WA MPIRA kulingana na ulivyoitoa. Nikaelewa kama vile ulimaanisha kuwa ni wale waliocheza ligi kuu, wale watu ambao wako karibu na wacheza mpira, waliowahi kucheza mpira(tena ligi kuu) na washinda vijiweni wakijadili leo tukampindue nani JANGWANI au MSIMBAZI, au nani tumpe madaraka DRFA (Yani watu wa FITINA). Yaani watu wasiokuwa na elimu, vibaraka, watu wa makundi. Ndio uliowaita watu wa MPIRA na unawahitaji sana waongoze SOKA la Tanzania. Ndo fikira zangu zilivyonipa jibu nini ulimaanisha kuhusu watu wa mpira, SAMAHANI kama nitakuwa nimekuelewa vibaya kwa hilo. Lakini kwa jambo ambalo nina uhakika nalo ni kwamba Ndugu JUMA SIMBA hutaki watu wenye elimu waongoze mpira/SOKA. Naweza nikawa nimekosea kutafsiri nini ulimaanisha watu wa mpira(na nisamehe kama nimekosea) lakini  kuhusu watu gani hutaki waongoze mpira sijakosea, wewe hutaki wasomi katika medani ya SOKA.
Hapa Mzee wangu ndipo tunapopingana.  Mimi naamini kuwa Mtanzania yeyote mwenye uelewa na mambo ya mpira(regardless kacheza mpira au la), mwenye elimu na uwezo wa kuongoza anaweza kuwa kiongozi wa SOKA.  Lakini kigezo cha uwezo wa kuongoza na uelewa ambavyo ni products/matunda ya Elimu ni JAMBO MUHIMU SANA.  Kwa hiyo Elimu na uongozi ni vitu viwili ambavyo ni ngumu kuvitenganisha.
Haiwezekani leo hii tukapinga watu wenye utaalamu wa fani mbali mbali kwa mfano Public Administration, Journalism, Law, Accountance, n.k kuongoza soka. USIJARIBU KUNISHAWISHI ETI LEO HII/ ama MIAKA IJAYO MRISHO KHALFAN NGASA anaweza kuwa kiongozi wa mzuri wa SOKA kunizidi mimi hapa, kisa mimi nachezea timu yangu ya MBAGALA KUU tena kwenye mazoezi maana hata kwenye mechi sipangwi. Yani huyo ndiye mtu wa mpira wa kuingoza DRFA au TFF kisa he is a star in our National Team. Mtu mwenye majibu rahisi katika issue ngumu ya kwanini kakataa offer ya kwenya El Mereikh(SUDAN),,mtu ambaye hawezi kusimamia maneno yake. Au Kocha Julio awe rais wa TFF? Eti kisa ni mtu wa mpira,, yani kocha aliyeiita timu yake kuwa ni kama mgonjwa wa ukimwi anayesubiri kufa(Mtu asiyejua madhara ya maneno yake),, au Godfrey Taita aliyeshindwa kujua thamani yake na majukumu yake kwa Taifa mpaka akaleta msichana ndani ya kambi ya Timu ya Taifa,, au Mwaikimba? Au Haruna Moshi Boban? Au Chuji?, Au Mwasika aliyempiga mwamuzi? Au Canavaro ambaye kasimamia hela ya mshindi wa tatu igawanywe kwa wachezaji wenzake?. Au mtu aliyedanganya kuwa ana elimu ya kidato cha nne wakati sio kweli(Je huyo ataweza kusimamia kwa nguvu zote kupinga udanganyifu michezoni), Au Mtu anayetoa rushwa katika chumba cha mkutano(Je huyo ataweza kupingaje rushwa michezoni?).
Umekaa ukafikiri hao niliowataja wanakosea wapi?tatizo ni nini?,,Hivi kwa nini hao unawaita WATU WA MPIRA washeshindwa kutuvusha tulipo kutupeleka hatua nyingine nzuri? hivi itakuwaje leo hii soka likiwa mikononi mwa hao wachezaji niliowataja hapo juu?. Huwezi nishawishi leo hii eti uongozi wa SOKA unahitaji watu ambao they can’t reason, wasioweza hata kutafsiri kwa ufasaha hata Article moja ya Katiba ya Vilabu vyao, au sheria za FIFA, watu wasiojua incase of disputes among the employees(players and other staffs) of the club, or the employees against the club, or incase of a strike which procedures should be applied/adopted to arrive at an amicable solution. Those who do not have knowledge of issues pertaining principles of Natural Justice(principles of the wise), Those who do not know principles pertaining administration, those who are unable to read and understand even a single English sentence, those who can not anticipate the impact of their words, KISA ETI WATU WA MPIRA. Au wale wanaoficha wachezaji wasiende kusign contract kujiunga na timu nyingine za nje NDIO WATU WA MPIRA.?
Karne hii unasimama kupinga watu wenye elimu kuongoza?  Wasomeshwa na serikali hili waletee maendeleo katika fani zote ikiwemo SOKA. IT SHOULD BE NOTED THAT, I do not deny WATU WASIO NA ELIMU ya stashahada, Shahada, Masters and PhD  haki ya kuongoza na kushiriki mambo ya mpira VIVYO HIVYO tusiwanyime watanzania wenye ELIMU kuwa viongozi wa soka kwa kutumia unreasonable ground “WATU WA MPIRA.” Mi nilitegemewa ndio wakati wa kuwakaribisha waje kutumia ujuzi wao walioupata vyuoni kuondoa utegemezi katika vilabu, kuondoa migogoro katika Nyanja zote za SOKA, kubuni njia za halali za mapato, kuzuia na kupambana na rushwa michezoni, kutafsiri kwa ufasaha sheria za michezo, n.k.
SWALI, Kwanini watu wasomi wasiongoze katika soka? Mnaogopa nini?,, Mh! Inatia shaka sana, IJULIKANE KUWA NI KAWAIDA MTOTO MDOGO KUOGOPA GIZA LAKINI AJABU KWA MTU MZIMA KUOGOPA MWANGA. (Bora huyo mtu mzima aogope giza basi, lakini anapoogopa  mwanga ,inashangaza) MTU Mzima akiogopa mwanga yawezekana yuko UCHI, tena uchi wa MNYAMA,, yani hata nguo za ndani hajavaa,, HIVYO BASI soka letu lawezekana liko uchi ndo maana MWANGA(WATU WENYE ELIMU WANAPINGWA).
NAJUA watanzania mmekuwa mkitilia shaka uwezo wa wasomi kwenye michezo,, na mna ushahidi kuwa baadhi ya wasomi hawajaleta lolote katika tasnia ya SOKA. Tatizo ni moja, hao wasomi waliopita walikuja kwenye michezo kisiasa,,The motive behind wasn’t to develop football but kujiimarisha kisiasa(political advantage/gain),,WAULIZE WANACHAMA WA SIMBA NINI KINAENDELEA PALE KWAO CHINI YA MWANASHERIA?Kipi anakipa kipaumbele CHAMA, JIMBO lake au SIMBA? WAULIZE MASHABIKI WA YANGA YULE ADVOCATE/MWANASHERIA alifanya nini?  Je aliwekwa na nani? Kwa manufaa ya nani au ilikuwa ni kumkomoa Mzee KIFUKWE!
Anyway nanyi wasomi mnatia aibu, Yani mwanasheria unasindwa kujua hata mipaka ya madaraka yako kikatiba,unajipa madaraka ya kufungia matawi ya club yako au unaconfiscate hadi nafasi ya msemaji wa club, Yani unamchezesha mchezaji aliye na kadi nyekundu mechi,, ni kwamba ulishindwa kutafsiri vifungu vya sheria mpaka timu ikanyanganywa point, Yani unasaini mkataba Kigali afu unaonesha umesainiwa Dar-es-salaam,Yani unaingia mkataba na mchezaji ambaye still ana mkataba na club nyingine ambayo imemtoa kwako kwa mkopo. Msomi wewe unaita mkutano na wahandishi wa habari kueleza ulilala hotel gani,  room namba flani wakati unaenda kumsainisha Mchezaji mkataba,(Hivi ungeulizwa kwanini unaingia gharama zote hizo wakati mchezaji tena muhimu ulikuwa naye siku zote na hajasaini mkataba mwingine mpaka upande wa pili unakaribia kumchukua na kuwaweka mashabiki roho juu ungejibu nini au ndo nao ungewafungia?) unajisifu kutumia ndege ya rais na kula aina flani ya chakula wakati Club yako haina hata Uwanja wa Mazoezi(Je hao wazee waliojenga hizo ofisi wasemeje), Unaapa eti leo siongei uongo kuna mtoto wa kigogo anatumiwa kuhujumu club yako(it means siku nyingine waga unadanganya).
TATIZO ni hili hapa: WAKATI upande huu unaogopa wasomi, Wasomi wanaoingia kwenye SOKA hawana nia na SOKA ama Wameletwa na WATU WA MPIRA AU WATAFUTA UMAHARUFU ILI BAADA YA MIAKA KADHAA AKAGOMBEE UBUNGE JIMBONI KWAKE. TUNAHITAJI WASOMI WENYE NIA YA KUENDELEZA SOKA, WATU WENYE UWEZO WA KUONGOZA, MAJASIRI NA WAELEWA WA MAMBO YA MPIRA. MNAOJIITA WA MPIRA MSIUKIMBIE MWANGA, MWANGA NI NURU YA MAENDELEO. Ndio ilivyo kwa elimu katika maendeleo ya mpira na mambo yote katika nchi yoyote. Tofautisha uelewa wa JOHN NJOROGE, JOSEPH OWINO, MIKE BARAZA, OKWI, PASCHAL OCHIENG, na hawa wetu utapata jibu, HONGERA GOLIKIPA WA TOTO AFRIKA YA MWANZA(Ngugu ERICK NGWENGWE) kwa kutambua umuhimu wa elimu, hongera ALLY MAYAI, CHAMBUA, SHAFFII, EDDO, na wengineo wengi kwa kulitambua hili twaweza kujua uelewa wenu hata kupitia kazi zenu. Si lazima uwe na shahada hata course ndogo zinafungua uelewa, pia kusoma vitabu na makala, kuwa na marafiki waelewa na wanaojitambua waweza ku-acquire ujuzi. TUSIWE WAVIVU WA KUFIKIRI na TUKAWA WEPESI WA KUONGEA, TUSIWE WAOGA WA CHANGAMOTO NA USHINDANI, Msiufanye mpira wa Tanzania ni wa familia ya mtu Fulani, ndugu na marafiki zake. WATANZANIA wanavyojitahidi kuteketeza mtandao wa MAFISADI, wafanye hivyo kuteketeza mtandao wa hawa wanao amini SOKA ni lao, “WATU WA MPIRA”
Let the eagles fly the sky, but the hens must stalk the ground
ELPHACE MWOMBEKI RWESHABURA.
0653210464
elphace.r@gmail.com

3 comments:

  1. Kaka uko deep sana naomba tupia madini kama haya atleast mara 2 kwa mwezi ikiwezekana tia hata magazetini coz ndo yanafikiwa na walio wengi.One love bro.BY JOHN MWAKALEBELA DSM

    ReplyDelete
  2. Kaka uko deep sana nmeipenda kaz yako,I wish ungekuwa unatupia madin km haya atleast mara 2 kwa mwezi au hata magazetin coz yanafikiwa na wengi.JOHN MWAKALEBELA DSM

    ReplyDelete
    Replies
    1. Haina shida kaka,, kazi itafanyika, tuombe wanipe nafasi kwenye media zao! PAMOJA KAKA TUTASHINDA!

      Delete