Yusuf Msakni alifunga bao dakika ya tisini na kuisadia Tunisia kuanza
kampeini yake kwa ushindi, katika michuano ya kuwania kombe la mataufa
ya Afrika inayoendelea nchini Afrika Kusini.
Kama
ilivyotabiriwa, vigogo hao walishambuliana vikali wakati wa mechi hiyo,
lakini juhudi za kufungana ziliambulia patupu hadi dakika za mwisho
pale Youssef Msakni alipovurumisha kombora kali kutoka zaidi ya mita
ishirini hadi kimnyani.
Katika kipindi cha kwanza timu hizo zilishambuliana kwa zamu na hadi kufikia mapumziko hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
Hata hivyo Tunisia ilipoteza nafasi nyingi za kufunga na kunako
dakika, ya 78 ya mchezo huo, Hamdi Harbaoui,alipoteza nafasi nzuri baada
ya kupewa pasi na Oussama Darragi.
Kufuatia ushindi huo Tunisia sasa inashikilia
nafasi ya pili na alama tatu sawa na Ivory Coast iliyoiilaza Togo kwa
magoli 2-1 katika mechi ya awali ya kundi hilo, lakini inadunishwa na
idadi ya magoli.
Algeria ni ya tatu huku Togo ikivuta mkia bila alama yoyote.
Katika timu 16 zinazowania Kombe la Mataifa ya
Afrika, ni timu mbili tu zilizopata ushindi baada ya kucheza mchezo
mmoja kila moja.
Timu hizo ni Mali iliyoifunga Niger bao 1-0
katika kundi B na Ivory Coast kuicharaza Togo magoli 2-1 kwenye kundi D.
Timu hizo sasa zina pointi 3 kila moja.
No comments:
Post a Comment