Juma Omary akiwa na mkufunzi wa Azam Academy Alando |
Siku moja baada kuchukuliwa rasmi na Academy ya klabu ya
Azam, kijana Juma Omary ameongea na tovuti hii na kutoa shukrani kwa uongozi wa
klabu ya Azam, Clouds FM huku akitoa ushauri kwa vijana wenzie wenye ndoto za
kufanikiwa kimaisha kupitia soka.
Akizungumzia mapokezi aliyoyapata Azam Academy Juma alisema:
“Nashukuru mungu kwa kuwapa moyo mwepesi viongozi wa Azam na kunipokea kujiunga
na kituo chao cha kukuza vipaji vya vijana kama mimi. Nimepokelewa vizuri,
nimepewa malazi na mahitaji yote muhimu. Tayari nimekutana na mwalimu wa hapa
na nimeonyeshwa sehemu tofauti ambazo nilikuwa nazishuhudia kwenye TV tu.
Nawahaidi viongozi wa Azam, Clouds FM na watanzania kiujumla kwamba nitafuata
maelekezo na mafunzo yote kwa nidhamu ya hali ya juu ili niweze kutimiza ndoto
yangu ya kuwa mchezaji wa kulipwa. Naahidi sitowaangusha.”
Pia Juma alitoa shukrani kwa Clouds FM – “Kwa kweli kutoka chini ya uvungu wa moyo
wangu shukrani zangu ziende kwa timu nzima ya Clouds FM. Wamenisaidia sana
mpaka nimefanikiwa kufika hapa Azam Academy, kama wanavyosema kwamba wao ni
Radio ya watu basi kwa utu walionionyesha mie nathibitisha kweli hiki kituo ni
cha watanzania na watu wote. Wana moyo mzuri watu wa Clouds na nitawashukuru
daima uku nikiwaombea kheri zaidi kwa mola.”
“Ushauri wangu kwa vijana wenzangu wasiwe watu wa kukata tamaa,
tupigane katika kufanikisha ndoto zetu, mungu anamsaidia yule mwenye kuonyesha
nia ya dhati ya kutaka msaada wake. Nawashauri tuwe wavumilivu na tusiwe wavivu
katika kutaka kufanikisha ndoto zetu.”
Natumai dogo atafanikiwa kama atajua nini anataka kwani wanasoka wengi wakubwa kutoka nchi za Afrika magharibi huwa wanajipeleka wenyewe Ulaya wakiwa na umri mdogo na kuonesha vipaji vyao! Ni lazima uonekane ili uendelee! Big up dogo na utambue ni kitu gani umekifata mjini!
ReplyDeleteSasa shaffih hapa interview ikwapi?
ReplyDeleteDOGO CHEZA MPIRA BADO HUJAFIKA SAFARI NDO KWANZA KIPYENGA KINALIA,BIG UP SHAFFIH N CLOUDS CREW
ReplyDelete