Search This Blog

Friday, January 4, 2013

NANA MENSAH-GHANA TUNAAMINI ILI UWE NA KIPATO KIZURI SI LAZIMA UFANYE KAZI BENKI,TUNAKUJA TANZANIA KUBORESHA CV ZETU


                   Nana Mensah kushoto,namimi mwenyewe

Tanzania imekuwa kimbilio la wachezaji kutoka ukanda wa Afrika ya Magharibi hasa kutoka nchi za Cameroon,Ghana na Nigeria.
mwanzoni nilikuwa na maswali mengi ya kwanini wachezaji hawa wanakimbilia sana Tanzania na wakifika hapa kwa kipindi chote wanachokaa  wanapata wapi pesa za kujikimu,Jana nimekutana na kiungo Nana Mensah raia wa Ghana aliyeko hapa nchini pamoja na mdogo wake wakisaka timu ya kujiunga nayo nikafanikiwa kufanya nae mahojiano machache.

Alikoanzia Nana Mensah
nilianzia kwenye kikosi cha vijana wa umri wa miaka 12 kwenye timu ya great united , nikaenda kwenye timu ya all stars ya vijana wa under 16, baada ya hapo nilienda liberty Professionals under 17 halafu nikarudi all stars baada ya hapo nikasajiliwa  kwa mkopo wa mwaka mmoja kwenye klabu ya nania ya daraja la kwanza baada ya hapo nikaenda tena Great united timu nyingine ya daraja la kwanza , nilienda thailand kwa miezi sita kwenye mechi za under 20 nikarudi Ghana nikaenda timu nyingine ya Kedia Hotspurs ya ligi kuu na baada ya hapo nikasafiri kwenda india  kwenye mechi za under 20 na sasa nipo Tanzania .
 nini siri ya mchezaji kupata mafanikio
kusema kweli ghana na watu wa afrika mashariki wanaamini kwenye kujenga CV , huwezi kwenda ulaya kirahisi bila kujenga cv nzuri wachezaji wote wakubwa wanaanzia sehemu kama hizi , nimekuja tanzania kujenga cv yangu kabla ya kwenda mahali kwingine
 unaizungumziaje ligi ya Ghana
ligi ya Ghana ni ngumu sana , kuna watu milioni 22 na nusu ya hao ni vijana wenye ndoto ya kuwa wacheza mpira sio issue ya wewe unaweza kucheza,unaposaini mkataba wa kucheza mwaka mmoja  mwaka unaofuata kuna mtu anakuja kukunyang'anya namba  huwezi kukaa mahali kwa muda mrefu, hata uongozi wa timu haukuruhusu ufanye hivyo , ni vigumu sana kupata nafasi na kila mtu anapambana  na timu zote zinatoa nafasi kwa wachezaji kucheza
 unafahamu chochote juu ya wachezaji raia wa ghana waliokuja tanzania
namjua Wahab Yahya aliwahi kucheza King Feisal , namjua Daniel Akuffor naye alitokea King Feisal , aliwahi pia kucheza Israel huko ndio nilimsikia sana , siwezi kusema kuwa wamenivuta kuja , nimekuja hapa mimi mwenyewe , mimi ndio nimejipa hamasa ya kuja hapa  kwa kuwa najua ninachotafuta , unapaswa kuamini kuwa unaweza na unatakiwa kujituma leo uko hapa , kesho uko mahali kwingine,wala hata sikufahamu kama Akuffor yuko hapa.

Nini kimekupa motisha ya kutoka Ghana kuja Tanzania
sababu ya mimi kuja hapa , naamini soka lliko mahali kokote na hata hapa naweza kufanikiwa, hata gwiji wetu kule ghana alianzia mahali pa chini,Abedi Ayew  alianzia Benin,wakati huo Benin haikuwa inafahamika, akatoka huko akaenda Marseile kwa hiyo siangalii wapi , najua ninachotafuta,naangalia soka na si vitu vingine.
nimefuatilia soka la hapa hasa michuano ya Afrika Mashariki na kati ,nchi kama Kenya,Congo ,nimeona mashabiki wanavyojaa uwanjani hapa Tanzania, ni kitu kizuri na naamini kuna mazingira ya kucheza soka hapa ,naamini ni vyema kuanzia hapa.
ni nani anayekudhamini
nina meneja ambaye ananisaidia katika masuala yangu ,nikipata safari na mahali pa kwenda kama ni majaribio ananisaidia ila sio timu ,nimekuja mwenyewe.

una mahusiamo na klabu gani tanzania kwasasa
nilipokuja siku najua mengi , nimefikia African lyon ambako nafanya mazoezi , ninafahamiana na kocha msaidizi mr Otieno,ni mtu mzuri sana , ila si kwamba nimesajiliwa huko,nafanya mazoezi binafsi .

ndani ya miaka 5 ijayo utakuwa wapi
 najiona nikienda mahali pakubwa sana kama wachezaji wakubwa ,nataka kwenda ulaya.
nini kinawapa hamasa wachezaji wa ukanda wa afrika magharibi kufika mbali,siri kubwa ni juhudi,mazoezi,kujituma , hakuna kitu kingine zaidi ya hayo, hakuna uchawi ,kujiamini ni muhimu na kumtanguliza mungu,soka sio vita hata kule kwenye vita soka huunganisha watu ,hakuna haja ya woga , inategemea imani yako na juhudi,unapaswa kuwa mbali na madawa ya kulevya na kujiweka fit .
Ghana tunaamini kuwa si lazima uwe daktari au mtu wa benki ndo uwe tajiri,ni mazoezi tu , Ghana ndio vijana wanavyowaza , kipaji unapewa lakini lazima ufanye mazoezi,kuna watu hawapendi kufanya mazoezi ,nimeona hapa,wanaamini wanajua lakini siri ni mazoezi sio kitu kingine,ni wewe mwenyewe,mazoezi ndio kikubwa ,ukienda Ghana ukitazama majumba ya Essien unapata hamasa ya kuwa kama wao,ukienda kwa Gyan unaona mwenyewe unachopaswa kufanya.

ungependa kuwashauri nini wanasoka wa Tanzania
nawashauri wakae mbali na madawa,pombe , soka ni bidii,wala hupaswi kukata tamaa kuna wengine umri ukisogea wanakata tamaa,hakuna haja ya kuogopa,mungu humuwekea kila mmoja njia , ni kipaji ambacho hakifundishwi shuleni,mungu ndio amekupa,kama we ni kijana unacheza leo napenda kukwambia ufanye kazi,wasikilize makocha , usisikilize wala kuwaza wanayokwambia marafiki wabaya,jisukume na ujiamini,usifikirie kuwa hakuna fedha,Ghana wachezaji wote wanatoka vijijini,wanakuja mjini wanacheza na wanafika mbali,kipaji chako kitakufikisha mbali

No comments:

Post a Comment