Search This Blog

Wednesday, January 16, 2013

MATOKEO YA MECHI ZA LA LIGA YANAPANGWA - ASEMA MAKAMU WA RAISI WA LA LIGA

Javier Tebas, makamu wa raisi wa Liga de Futbol Profesional (LFP), anaamini kwamba kuna mchezo wa upangaji matokeo kwenye La-Liga, na anaogopa skendo iliyowahi kuikumba Serie A maarufu kama Scommessopoli ipo njiani kuja kwenye ligi kuu ya Hispania.

Tebas ana mashaka kwamba kuna matokeo ya baadhi ya mechi yanapangwa, lakini anakiri kwamba anakosa ushahidi wa kutetea tuhuma zake.


"Mechi zinauzwa kwenye La Liga na wanaofanya mambo hayo inabidi waekwe hadharani," makamu huyo wa raisi wa LFP amesema kwenye mahojiano na Onda Cero.

"Kwa bahati mbaya nashindwa kutoa uthibitisho, lakini matokeo ya mechi yanapangwa nchni Hispania. Naona ile skendo ya ibu iliyotokea Italy ikija hapa kwetu."

3 comments:

  1. Yaani mi naweza kuamini kabisa juu ya suala hili...haiwezekani ligi ikawdrida ya timu mbili tu....barca na real madrid....nashauri kungekuwa na mechi mbili tu!!kati ya timu hizi mbili nyumbani na ugenini atakayeshinda awe bingwa wa La liga.....hakuna ushinda ukilinganisha na EPL au B-sliga ama Serie A. Kibaya zaidi hata FIFA na UEFA wameingia kwenye mtego huo...ili uwe mchezaji bora wa DUNIA basi ni lazima uwe na passport ya SPAIN....this is shame!!!!

    ReplyDelete
  2. hii inaweza kuwa kwel haiwezekani timu zngne hazitoi ushindan wala kkukamia game ndo maana msimu huu ligi haina mvuto

    ReplyDelete
  3. watu wa epl tukiwapa barca mtawaweza?

    ReplyDelete