Search This Blog

Tuesday, January 8, 2013

Je Barcelona inamtegemea sana Lionel Messi?na je Guardiola ndiye anastahili hizi tuzo za Messi ? (PART 11)

Lionel Messi and Pep Guardiola - FIFA Ballon d'Or Gala 2010

GUARDIOLA AUNDA MZIMU AMBAO UNAITAFUNA BARCA TARATIBU.
 Hakuna pingamizi kuwa Messi amekuwa mchezaji bora duniani kwa muda wa miaka minne iliyopita, ametwaa taji la ufungaji bora kwenye ligi ya mabingwa mara nne mfululizo huku akiwa sehemu ya kikosi kilichotwaa ubingwa mara mbili akifunga kwenye fainali hizo.
Pep Guardiola alijenga ukaribu na Messi katika miezi yake ya mwanzo kama kocha wa kikosi cha kwanza. Alimpa Muargentina huyu sababu ya kuamini kuwa yeye ni bora na anaweza kuwa juu ya Dunia. Kocha mwingine angeweza kufeli kwenye hili na tusingeona kipaji cha Messi.
Guardiola alijifunza kuwa Messi angekuja kuwa na upekee kwenye timu yake, ila pia alijifunza kuwa ili Messi awe bora ni lazima afurahishwe kwa kubembelezwa. Mwenyewe anasema kuwa 'Messi akitabasamu kila kitu ni rahisi",hii ni hatari kwa future ya Barcelona.
Muendelezo wake kama mfungaji bora kwenye soka la dunia unaonekana tangu ujio wa Guardiola , mabao 38 kwenye msimu wa kwanza, 47 kwenye msimu uliofuata , 53 na 73 katika misimu iliyofuata huku akifunga zaidi na zaidi katika siku zilizofuata . Cha muhimu ni kwamba mafanikio ya timu yametokana pia na kazi za wenzake na si Messi pekee.


Timu ya mafanikio haiwezi kuwa inategemea mchezaji mmoja pekee. Hakuna ubishi kuwa ubora wa mchezaji una umuhimu ila si utegemezi kwa mchezaji mmoja kwani hili hufanya timu kuonekana ina mlengo mmoja tena unaotabirika unaoifanya kuwa rahisi kucheza dhidi yake.Siku zote lazima kuna mchezaji atajitokeza kuwa nyota ila timu ni muhimu zaidi kuliko upekee wa mtu mmoja .
Kwenye msimu wa kwanza wa Guardiola kulikuwa na Eto'o , Henry na Messi . Magoli yalifungwa na wachezaji wote hawa ambapo kulikuwa na namba kama 36,26 na 38 huku wachezaji wengine kama Bojan na Xavi wakifunga mabao 10 kila mmoja . Msimu huo Barca hawakuacha taji lolote.
Wakati Eto'o alipoondoka alibadilishwa na Ibrahimovic katika msimu wa 2009/2010 na hapo magoli yakaanza kuonekana kusambaa kwa utofauti kidogo. Messi alifunga mabao 47, Zlatan 21, Pedro 23 na Bojan 12. Walishinda ligi lakini Ligi ya mabaingwa hawakuweza kuitetea.     Jaribio la Zlatan lilionekana kushindwa baada ya ugomvi baina yake na Messi wa majukumu ya kucheza huu wote wakiwa wanataka jukumu moja (ugomvi ambao baadae ulinunuliwa na Pep na kugeuka kuwa wake yeye na Zlatan) Guardiola akamtupia Zlatan Virago.
David Villa alinunuliwa na hapo Barcelona ilionekana kuwa na balance tena tofauti na kabla ya ujio wake. Maforward watatu Messi , Villa na Pedro walikuwa hatari sana kwa msimu wa 2010-2011 huku wakiwa wanacheza katika mfumo wa 4-3-3. Viungo Xavi, Busquets na Iniesta walikuwa bora sana kiufundi huku wakifanya kazi ya kuwalisha kina Messi mipira ya moja kwa moja na ya kupenya ambayo ilikuwa migumu sana kwa timu pinzani kuidhibiti. Messi alicheza kama namba 10 na kusaidia kutengeneza mabao kwa Villa na Pedro wakiwa wanatokea pembeni wanaingia ndani, wakati mwingine alicheza kama namba 9. Messi alifunga mabao 53, Villa 23 na Pedro 22.
Lionel Messi and Pedro Rodriguez - FC Barcelona v Real Racing Club  - Liga BBVA

Msimu uliopita na msimu huu umeonyesha mwenendo wa kutia hofu. Hakuna mchezaji zaidi ya Messi aliyefunga zaidi ya mabao 20 kwa Barcelona. Fabregas ,Xavi ,Pedro na Sanchez wote walifunga zaidi ya mabao kumi , Villa alifunga 9 pekee kabla ya kuumia mwezi desemba.
Messi alifunga mabao 73. Mafanikio ya Messi yaliwashangaza wengi na hakuna wa kumkosea fadhila kwa kushindwa kutambua alichokifanya kama mchezaji. Hata hivyo timu ya Barcelona taratibu ilizidi kuonekana inamzunguka Messi . Balance ya timu na ubora ukaanza kupotea, Messi akawa ndio Barcelona.
 Maendeleo yake kama mchezaji yalimfanya kuwa na umuhimu wa kipekee kwa Barcelona akionekana anahusika katika kila kitu kinachofanyika kwenye timu hiyo kuelekea mbele na hapo ndio mafanikio ya timu yalipoonekana kupungua.
Kwa kujaribu kumfurahisha Messi , Guardiola alitengeneza zimwi la ufungaji mabao la Barcelona , zimwi ambalo lilionekana kuwameza wenzie na kuwatawala kwa wakati huo huo hasa mchezaji yoyote aliyejitokeza kujaribu kuwa muhimu kwa timu hiyo zaidi yake.
Mpaka kufikia wakati huu Messi ndiye mchezaji pekee aliyefunga mabao kwa style ya "double digits",Villa ana mabao nane, Fabregas ana mabao 7 , Adriano ana mabao 6 na Messi tayari ana 35, takwimu hizi zinamaanisha nini?
Maendeleo ya Messi kama mchezaji hayapingiki,hakuna aliyedhani kuwa kijana toka Argentina aliyepewa mechi yake ya kwanza mwaka 2004 atakuja kuwa huyu ambaye leo amepewa tuzo nne za mchezaji bora wa dunia kwa miaka minne mfululizo.
Hata hivyo Barcelona wako katika kipindi ambacho mchezaji huyu amekuwa na kauli na umuhimu mkubwa kuliko mtu mwingine yoyote. Hili ni tatizo kubwa sana, tatizo ambalo limeonekana kukosa wasaidizi kama ilivyokuwa kipindi cha Eto’o, Henry na Pedro na hii itafanya timu nzima isiwe na mafanikio.
Itaendelea……..

No comments:

Post a Comment