Siku chache zilizopita msenegali Demba Ba alihama kutoka kwenye klabu ya Newcastle na kwenda kujiunga na mabingwa wa ulaya klabu ya Chelsea baada ya kuwa na misimu miwili yenye mafanikio kwenye klabu ya Mike Ashley. Ni uhamisho ambao ni mzuri kwa Chelsea na mzuri zaidi kwa mchezaji husika ambaye alipitia taabu nyingi mpaka kufika hapo alipo. Lakini siku chache baada ya kuhamia London baadhi ya wadau wa soka ulimwenguni wamekuwa na maswali wakijiuliza Je Ba ni mroho wa fedha au mjasiriamali mwenye tamaa ya kufanikiwa zaidi? ............................
Wakati Ba alipokwenda England akitokea Ujerumani alipewa jina la 'bomu la muda linalosubiri kulipuka' na kocha wa Stoke City Tony Pulis. Ada ya uhamisho ilikuwa imeshakubaliwa na kilichokuwa kimebakia ni vipimo vya afya lakini akafeli vipimo kutokana na jeraha la goti alilougua kwa muda mrefu ikizingatiwa ada ya uhamisho ilikuwa ni £6m.
West Ham wakafunga macho na masikio wakamchukua Ba kwa kutoa £500,000 tu, huku akiingia mkataba wa kulipwa kadri anavyocheza. Ingawa alicheza vizuri na kupachika mabao lakini alishindwa kuinusu timu hiyo kushuka daraja.i
Hapo ndipo Ba akaamua kutumia kifungu kilichopo kwenye mkataba kilichokuwa kikimruhusu kuondoka bure kwenye mkataba wake, hivyo akaondoka na kuwaacha washabiki wa wagonga nyundo wa London wakiwa na hasira dhidi yake.
Newcastle ndio kilikuwa kituo chake kilichofuatia ingawa tangu mwanzo ilionekana asingekaa sana. Akaingia mkataba na kama kawaida kipengele cha kumuuuza ikiwa timu itakuwa inamtaka kikawekea fedha kidogo £7m katika dili lake na klabu ya St.James Park - kipengele ambacho kilikuwa kinajulikana karibu na wadau wengi wa soka, hasa zaidi pale zilizipoanza tetesi za kutakiwa na vilabu vingine katika dirisha za usajili. Hivyo halikuwa jambo gumu kwa Benitez kumshawishi bosi wake mrusi kutoa kiasi cha £7m ukizingatia tayari Sturridge alikuwa anaondoka huku Torres akiwa hatabiriki.

Matokeo yake sasa amerudi tena London safari hii akiwa na mabingwa wa ulaya huku akiwa analipwa kiasi kisichopungua £75k kwa wiki, akiwa amezungukwa wachezaji wakubwa wenye vipaji vikubwa. Maisha yanataka nini tena kwa Demba Ba. Lakini vipi kuhusu Newcastle? Hawawezi kuumia sana, kama ambvyo nilisema huko mwanzoni Toon walifaidika na Ba ambaye walimpata bure. Kumsajili mchezaji ambaye ameshathibitisha ubora wake katika kucheka na nyavu kwenye ligi ya England tena akiwa na miaka 26 ilikuwa biashara nzuri kwao, hata kama kulikuwepo na wasiwasi kuhusu afya yake na kuondoka kwa Ba kuliwaumiza sana West Ham na mashabiki wao. Newcastle walifurahia wastani mzuri wa Ba wa kufunga goli katika kila mechi 2.
Tukichimbua ndani zaidi na tetesi zinasema kwamba Ba ametengeneza fedha nzuri kutoka kwenye fedha ambazo Newcastle wamelipwa. Mmoja wa wamiliki wa West Ham David Sullivan alisema: "Nimeambiwa amepata fedha kutoka kwenye zile £7m ambazo ziliwekwa kwenye kipengele cha kumuuuza ikiwa timu itakuja kumtaka.. Alikubaliana na Newcastle atapata nusu ya fedha zile. Hivyo kwenye Ba amechukua kwenye usajili wake wa kwenda Chelsea. Kulipwa £3m sio kitu kibaya, lakini kwa mchezaji wa kiwango chake sio kubwa sana. Na Newcastle walimlipa wakala wake £2m ili aweze kumshawishi kumtoa hapa (Wes Ham). Newcastle wameendelea kukataa lakini ndio ukweli." - Kama jambo hili ni kweli inabidi tuwapongeze Ba na wakala wake kwa kuwa wafanyabiashara wazuri.
Siku hizi mapenzi ya wachezaji na uaminifu kwa vilabu sio kitu ambacho kinatokea mara kwa mara kutokana na mishahara mikubwa ya kutisha inayotolewa. Lakini kitu kimoja inabidi tuelewe ni kwamba maisha yao ya kisoka yanaweza yakawa mafupi kutokana na majeruhi. Kwa kuliangalia hili la kucheza kwa muda mfupi nimemuelewa kabisa Ba na waka wake kibiashara zaidi.
Majeruhi ya goti ambayo yalizifanya klabu mbili (Stuttgart & Stoke) kukatisha suala la kumsajili, kwa hakika kitu hiki kilifanya maisha ya soka ya mchezaji yawe katika wasiwasi mkubwa. Je nani angemtaka ukiangalia reodi yake ya majeruhi? Je nafasi ngapi angezipata na hatua gani ya soka angekuwa anacheza? Ikiwa madai ya David Sullivan ni ya ukweli then Ba amejitengenezea maisha kiuhakika huko mbele na kufurahia matunda ya soka lake. Kuondoka kwenye klabu zake mbili hakuchagua maneno mazuri ya kusema. "Chelsea ipo kwenye levo nyingine, sio West Ham au Newcastle." Kwa kauli hii unaona kwamba Demba Ba sio mwenye uaminifu bali mtu mwenye tamaa ya kufanikiwa. Ndivyo inaonekana.

Kwa upande mwingine naamini hivi vipengele kama alivyoweka Demba Ba katika mikataba yake huko nyuma ni vizuri kwa wachezaji kwa kuwa vina faida kwao ikiwa wana imani na uwezo wao na wanataka kuendelea mbele zaidi katika soka la kizazi cha sasa. Tengeneza jina lako na klabu kubwa zitakuja tu kutaka kutengua vipengele vya mkataba wako na kukusajili. Rudia tena staili hiyo hiyo mpaka utakapofika juu kabisa.
Ingawa Chelsea sio klabu kubwa zaidi duniani lakini kwa hakika ni mojawapo ya klabu kubwa nchini England, ligi ambayo ni tajiri. Kwa umri wa Ba na leve aliyoifikia tutaona kama kweli ni mroho wa mafanikio zaidi kadri anavyozidi kukua kisoka au tutaona kama ni mroho wa fedha ambaye sasa anadhani ameshafika na kufanikiwa.
MUDA UTAONGEA ZAIDI
No comments:
Post a Comment