ASHLEY COLE ametania kwamba anahitaji pasipoti ya kihispania ili aweze kutajwa katika kikosi cha wachezaji bora wa dunia.
Beki huyo wa kushoto wa England, 32, amekosa nafasi katika kikosi cha FIFA/FIFPro World XI
kilichotangazwa jana usiku huku mbrazil Marcelo anayechezea Real Madrid akichaguliwa kwenye nafasi ya beki wa kushoto.
Cole alifunga penati katika ushindi wa Chelsea kwenye Champions League na akaenda nyumbani na medali ya saba ya kombe la FA Cup.s
Lakini hiyo haikutosha kumfanya achaguliwe kwenye kikosi cha wachezaji bora wa FIFA.
Cole alikuwa kwenye kikosi cha England kilichoshiriki Euro 2012 na kufika kwenye hatua ya robo fainali huko nchini Ukraine na Poland.
Akijibu moja ya hoja zilizotolewa na mashabiki wake Ashley Cole alisema - amezoea kukosa mapenzi mapenzi kutoka watu, na hana tatizo na hilo huku akiweka hashtag akisema #iwantspanishpassport”
No comments:
Post a Comment