Kocha wa timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Kim
Poulsen ameomba ‘fair play’ kutoka kwa muamuzi wa mechi ya leo (kesho) dhidi ya
The Cranes ya Uganda katika nusu fainali ya mashindano ya Cecafa Challenge Cup
Jijini Kampala.
Kocha huyo aliyasema hayo mara baada ya Stars,
inayodhamniniwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kumaliza mazoezi katika Uwanja wa Chuo Kikuu Kyambogo.
“Vijana wamejiandaa vizuri kabisa na wote wako katika hali
nzuri ya kucheza ila tunachoomba ni fair play kutoka kwa muamuzi maana
tunacheza na wenyeji ambao wana watazamaji wengi,” alisema.
Alisema timu zote mbili ni nzuri na iwapo muamuzi
atachezesha vizuri basi utakuwa ni mchuano mkali. “Vijana wana ari na mchezo
huu na tukipewa fair play tutacheza vizuri kama tulivyofanya katika
michezo dhidi ya Rwanda,” alisema
Poulsen.
Muamuzi wa mechi ya Cranes na Stars ni Mohamed El Fadil
kutoka Sudan ambaye pia alichezesha mechi ya Stars dhidi ya Rwanda.
Alisema ana furaha kwa kuwa hakuna majeruhi hata mmoja na
pia aliwasifu wachezaji wake kwa kuonyesha umoja na nidahmmu ya hali ya juu. “Hawa
wanakaa kama familia si unawaona walivyo pamoja?” alisema Poulsen na kuongeza
kuwa hilo ni muhimu sana kwa mchezaji.
Naye kocha msaidizi, Sylvester Mash alisema Stars ina nafasi
kubwa sana ya kushinda mechi hii kwa sababu wenyeji wao, The Cranes watakuwa
wanacheza kwa wasiwasi kwa kuwa wako nyumbani .
“Timu yetu iko motivated kabisa na ukizingatia Uganda wako
nyumbani, wao ndio wana tension kubwa zaidi,” alisema na kuongeza kuwa mchezo
huu utakuwa wa kusisimua sana.
Akizungumza kutoka Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro
Premium Lager, George Kavishe alisema Stars ina kila sababu ya kutinga fainali
na kunyanyua kombe kwa mara ya nne.
“Sisi kama wadhamini tunasubiri ushindi maana tuna imani na
Stars na hatua waliyofikia ni nzuri nay a kutia moyo kwa hivyo watanzania
wajitokeze kwa wingi na kuufuatilia mchezo huu kesho,” alisema Kavishe.
Mchezo wa Stars na Cranes utatanguliwa na semi fainali ya
kwanza kati ya Zanzibar na Kenya ambao pia ni mchezo wa kusisimua kwani timu
zote mbili zimeshaonyesha uwezo mkubwa.
Kocha wa Zanzibar Salum Nassor ameshatangaza mara mbili
akiwa Zanzibar na hapa Kampala kuwa iwapo hataondoka na kombe basi atabwaga
manyanga.
Fainali na Cecafa Challenge zinatarajiwa kufanyika Jumamosi
Disemba 8 na mechi ya kumpata mshindi wa tatu na nne itachezwa siku hiyo hiyo
pia.
|
Ha ha Ngasa kabeba watu wawili... Kweli KIM kiboko.. Mazoezi mazuri
ReplyDeletehivi kweli editor maneno yooote na picha zooote hizi...umeshindwa kuandika mechi itaanza saa ngapi?????!!!!!????au kila mtu anajua mechi ni saa ngapi????
ReplyDelete