Search This Blog

Wednesday, December 5, 2012

AZAM YATHIBITISHA KUMUUZA MRISHO NGASSA KWA $75,000 EL MERREIKH YA SUDAN

Azam FC leo imemuuza mchezaji wake Mrisho Halfan Ngasa kwa klabu ya El Mereikh katika majadiliano yaliyochukua takriban saa moja kwenye makao makuu ya klabu ya Azam FC na kuhudhuriwa na viongozi wa pande zote mbili.
El-Mereik wameshazungumza na mchezaji na kukubaliana maslahi yake binafsi ambapo Mrisho Ngasa atalazimika kusafiri hadi mjini Khartoom Sudan mara baada ya kuisha mashindano ya CECAFA Challenge Cup ili kuona mazingira ya klabu, kufanya vipimo vya Afya na kuangalia makazi yake binafsi.
Kuuzwa kwa Mrisho Ngasa nchini Sudan kunaifanya klabu ya Azam FC kupata kiasi cha zaidi ya Dola 50,000 pesa ambayo Azam FC waliiweka kama kima cha chini cha kumuuza Mrisho Ngasa.
Wakati Azam FC ikimtoa Ngasa iliweka kiasi hicho cha dola 50,000 kwa timu itakayomtaka lakini kutokana na kukosekana na mnunuzi huku Simba ikitoa ofa ya shilingi milioni 25, Azam FC iliamua kumpeleka Ngasa kwa mkopo ili akitokea mteja mwenye kufikia dau hilo waweze kumuuza.
Meng

i yalisemwa juu ya biashara ya mkopo kati ya Azam FC na Simba lakini msimamo wa Azam FC uliowekwa kwenye tovuti hii leo umethibitika baada ya El-Mereikh kufikia dau la kumnunua Mrisho Ngasa.
Mrisho Ngasa, mchezaji mwenye kipaji cha hali ya Juu cha kusakata kabumbu anakwenda nchini Sudan kwenye kikosi chenye mafanikio zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati baada ya TP Mazembe.
Azam FC inamuuza Mrisho Ngasa kwa kuzingatia umuhimu wa maendeleo ya mchezaji mwenyewe kimpira na kwa kipato, pia kwa kuzingatia kwamba Tanzania inahitaji wachezaji wengi wanaocheza nje kwenye vilabu vikubwa ili wanaporudi waweze kuisaidia timu ya Taifa.

7 comments:

  1. NGSA BORA UHAMIE SUDAN COZ WENGI TUNAJUA ULIKUA SIMBA KWA KULAZIMISHWA BUT HUKUWA NA MAPENZI PALE, KARIBU TENA NYUMBANI{YANGA} SASA ANAFUATA OKWI 5 LAZMA ZIRUDI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pole sana, kamwe zile tano hamta weza kuzirudisha kama ambavyo mmeshindwa kuzirudisha zile sita...nadhani una taarifa kuwa Okwi kashaongeza mkataba wa miaka miwili na tunaongeza majembe jiandaeni na tano zingine mafala nyie..

      Delete
  2. watu washaanza unazi mwacheni kijana awe huru acheze mpira majungu uwa ayasaidii kinachotakiwa simba sc kutafuta mchezaji mzuri zaidi

    ReplyDelete
  3. Hongera sana ngasa Mungu akuzidishie zaidi katika kikosi cha El Merheckh.

    ReplyDelete
  4. Hongera sana NGASA

    ReplyDelete
  5. thank u ngassa all da best uendako, tutakukumbuka jembe!

    ReplyDelete
  6. Kaendelee kukaza kijana mpaka mafanikio zaid yaje hiyo ndo njia panda ya ulaya, keep up bro.

    ReplyDelete