Search This Blog

Monday, November 26, 2012

YALIYOJILI KWENYE GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE KWENYE VIWANJA VYA LEADRES!

Pichani shoto ni  Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Stephen Gannon akionesha kipaji chake ikiwa ni sehemu ya kuwahamasisha vijana wakati wa kutafuta Vipaji katika shindano la Guinnes Football Challenge, Leaders Club Nov 24,2012
 Vijana mbalimbali waliojitokeza kwenye shindano hilo wakifuatilia michakato iliokuwa ikiendelea uwanjani hapo
Mmoja wa washiriki kutoka Kinondoni akijaribu bahati yake kwa kucheza mpira (ball Control) wakati wa Mchujo wa Guinness Football Challenge (GFC) uliofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.Aidha kwa mujibu wa waratibu wa shindano hilo wameeleza kuwa kutokana na vijana kujitokeza kwa wingi na timu kuwa nyingi wameongeza muda wa kuwataja washindi watakaopatikana. 
 Baadhi ya wadau mbalimbali waliojitokesha kushuhudia shindano hilo la Guinness Football Challenge (GFC),liliwavutia vijana wengi mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya vijana waliofika katika mchujo kutafuta timu 5 zitakazo liwakilisha taifa la Tanzania katika mashindano ya Guinness Football Challnge (GFC) nchini Afrika Kusini, ambapo vijana wawili wawili wanaonda timu moja na endapo kama timu hiyo itafanikiwa kushinda kule Afrika Kusini itajinyakulia kitita cha Shilingi Bilioni 1 na Milioni mia nne.

Washiriki wakijaribu bahati yao kwa kucheza mpira (ball Control) wakati wa Mchujo wa shindano la Guinness Football Challenge (GFC) uliofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya waratibu wa shindano la Guinness Football Challenge (GFC) wakiendelea kuratibu timu zilizokuwa zimeingia kwenye nafasi ya mchujo wa awamu ya pili.
Baadhi ya waratibu wa shindano la Guinness Football Challenge (GFC) wakijadiliana jambo huku mashindano ya mchujo yakiendelea,shindano hilo limefanyika mwishoni mwa wiki,viwanja vya Lidaz Club jijini dar na kuhuhuriwa na vijana wengi.

No comments:

Post a Comment