Search This Blog

Monday, November 26, 2012

Watanzania zaidi ya 120 watinga Kampala, waipa Stars ushindi


Na mwandishi wetu-Kampala
 Beki wa timu ya Kilimanjaro Stars, Kelvini Yondani (kushoto)
akizungumza na Shaban Nditi muda baada ya mazoezi waliyofanya katika
Uwanja wa Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda jana. Kilimanjaro
Stars kesho inacheza na timu ya Burundi katika mwendelezo wa michuano
ya Cecafa Challenge 2012. Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro
Premium Lager
 Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen (kushoto) akimwelekeza
jambo kipa  na Nahodha wa Kilimanjaro Stars, Juma Kaseja wakati wa
mazoezi yaliyofanyika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Makerere nchini
Uganda jana.Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium lager
Wachezaji wa Kilimanjaro wakitaniana baada ya kumalizika kwa mazoezi yaliyofanyika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda.Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager

Watanzania zaidi ya 120 ambao ni Mashabiki wa timu ya Tanzania bara,
Kilimanjaro Stars walijitokeza Jijini Kampala na kuishangilia timu yao
kwa staili ya aina yake na kuisababisha Stars kuibuka na ushindi
katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Sudan katika michuano ya CECAFA
Challenge 2012.
Watanzania hao walitokea Mkoa wa Kagera huku wakiongozwa na Mwenyekiti
wa Bukoba Veterans, Ernest Nyabo.
Mashabiki hao walileta hamasa ya aina yake kwa wachezaji wa Stars,
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, kwani wachezaji
walijituma na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
“Tuna mapenzi na timu yetu ndio maana tumeacha shughuli zetu na
kupanda mabasi kuja huku Kampala kuiona timu yetu ikicheza na kuja
kwetu kumezaa matunda kwani vijana wamecheza vizuri na kuibuka na
ushindi,” alisema Bw Nyabo.
“Tumependa sana ushirikiano uliopo kati ya Mrisho Ngassa na John Bocco
kwani imezaa matunda” alisema mwenyekiti huyo.
Walisema endapo Stars itasonga mbele zaidi mashabiki wengi zaidi
watafunga safari kuja Kampala ili kuipa timu nguvu. “Tunachoomba tu ni
wachezaji pia wawe karibu na sisi…wakifunga waje upande wetu
tushangilie pamoja,” alisema.

Naye Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, inayodhamini
Kilimanjaro Stars, George Kavishe, aliipongeza timu hiyo kwa kuanza
vizuri na kuwaomba wachezaji wasibweteke kwani wazidi kutia bidii ili
washinde mechi zote zilizobaki na kutinga fainali.
 "Tuna imani nao na tunasubiri walilete nyumbani ili tusherekee pamoja,
tutazidi kuwapa sapoti kama wadhamini wao watupe ushindi tu," alisema.
 Baadhi ya mashabiki waliokuwa wakifuatilia mchezo hup kupitia Super
Sport walisema walifurahishwa na kiwango kilichooneshwa na Stars na
wako tayari pia kufunga safari kutoka Dar es Salaam na mikoa mingine
ili kuishangilia timu yao.
Baada ya ushindi huu Tanzania iko katika nafasi ya pili katika kundi B
ikiwa na pointi 3 huku Burundi ikiongoza kwa wingi wa mabao kwani
iliifunga Somalia mabao 5-1. Sudan inashika mkia ikiwa bila pointi
wala bao.
Stars inakabiliwa na kibarua kigumu Jumatano kuikabili Burundi na
baadaye Somalia Disemba 1ikiwa ni mechi ya mwisho katika hatua ya
makundi.
Kocha wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen amesema ana imani na wachezaji
wake kwani wengi ni vijana na tayari wameonesha kuwa wana ari ya
kushinda.
Alisema anasikitika kuwakosa washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas
Ulimwengu kwani wangeongeza nguvu kwenye kikosi chake.
“Nasikitika kuwakosa lakini kama kocha nitawatumia wachezaji waliopo
ila nina uhakika TFF wanalifuatilia suala hili ili wachezaji hawa
waungane nasi,” alisema.
Stars iliendelea na mazoezi katika viwanja vya Chuo Kikuu Makerere
huku Nahodha wake Juma Kaseja akiwaomba watanzania kuwapa moyo
wachezaji kwani mashindano ni magumu lakini watapambana ili waweze
kutwaa ubingwa.
“Siku za nyuma wachezaji wa timu ya Taifa wamekuwa wakizomewa sana
nawaomba watanzania wawape wachezaji moyo ili tuweze kushinda,”
alisema

No comments:

Post a Comment