Timu
ya Taifa (Taifa Stars) inatarajia kuingia kambini baada ya kumalizika
michuano ya Kombe la Chalenji inayofanyika Uwanja wa Taifa wa Mandela
ulioko Namboole jijini Kampala, Uganda. Michuano hiyo iliyoanza Novemba
24 mwaka huu itamalizika Desemba 8 mwaka huu.
Kwa
mujibu wa Kocha Mkuu wa timu hiyo Kim Poulsen, Stars itaingia kambini
kujiandaa kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya mabingwa
wa Afrika, Zambia (Chipolopolo) itakayochezwa Desemba 23 mwaka huu
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Baada
ya pambano dhidi ya Chipolopolo, wachezaji watapata mapumziko ya wiki
mbili kabla ya kuingia tena kambini Januari 6 hadi 20 mwakani kwa ajili
ya mechi nyingine za kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya
mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco.
Kim
anatarajia kuongeza kipa mmoja kwenye kikosi chake ili kuwasaidia
nahodha Juma Kaseja na Deogratias Munishi pamoja na chipukizi kadhaa
kutoka timu za Taifa za vijana za Ngorongoro Heroes na Serengeti Boys.
Vilevile
Kim anafuatilia wachezaji wengine kwenye timu ya Zanzibar (Zanzibar
Heroes) ambayo pia inashiriki michuano ya Kombe la Chalenji ikiwa katika
kundi C pamoja na timu za Eritrea, Malawi na Rwanda.
No comments:
Post a Comment