Wakati Jack Warner alipotoka kwenye mchezo wa soka mwaka 2011 aliacha wingu la hewa ya hasira nyuma yake toka kwa watu waliodai kuwa hakupambanishwa na tuhuma za rushwa dhidi yake kwenye uchaguzi wa FIFA.
Haikuwa kama Warner alikuwa kiongozi mdogo kwenye uongozi mzima wa FIFA . Amekuwa makamu wa Rais wa FIFA , Rais wa CONCACAF kwa
miaka 11, Rais wa Chama cha soka kwenye visiwa vya Carribean na
kiongozi wa soka la visiwa vya Trinidad and Tobago. Zaidi ya hayo
Warner alikuwa waziri kwenye serikali ya Trinidad and Tobago.
Hata hivyo ripoti zilizoibuka wikiendi hii zinaonyesha kuwa bado
watu wanazungumzia masuala mbalimbali yanayomhusu Warner . Kamati ya
hadhi ya serikali imeundwa maalum kwa ajili ya kuchunguza tuhuma za
masuala ya kibiashara ya Warner ambayo yana utata mwingi ndani yake
hususani ushiriki wa taifa la Trinidad and Tobago kwenye kombe la dunia
la mwaka 2006 huko nchini Ujerumani.
Nusu ya wachezaji wa timu ya taifa ya kipindi hicho wamekuwa
wakihangaika mahakamani kusaka malipo ya bonus za ushiriki wao kwenye
michuano hiyo huku lawama nyingi kwenye tuhuma hizo zikimwangukia Warner
pamoja na chama cha soka cha Trinidad and Tobago kama Taasisi.
Ndani ya FIFA Warner amekuwa mshirika mkubwa wa rais wa FIFA Sepp
Blatter . FIFA ilimruhusu Warner kufanya atakacho kwenye uongozi wa
CONCACAF huku akisaidiwa kiuchumi huku kazi kubwa ambayo Blatter
alimtaka aifanye ikiwa kumhakikishia kura 30 za ukanda wa CONCACAF kweye
chaguzi mbalimbali za FIFA.
Hata
hivyo haya yote yalianza kubadilika kwa ishara zilizoanza kuonekana
mwaka 2011 ambapo Warner alionekana anaanza kumuunga mkono Mohamed Bin
Hammam ambaye alijitokeza wazi na kutangaza kumpinga Blatter kwenye
uchaguzi wa Urais wa FIFA .Warner aliandaa mkutano kwa ajili ya Bin
Hammam huko Port Of Spain mji mkuu wa Trinidad and Tobago ambaye alikuwa
akiutumia kufanya kampeni .
Ni
mkutano huu ambapo wajumbe walipewa hongo za dola elfu 40 kwa kila
mmoja huku wakiagizwa kuwa fedha hizo ni gharama za kufika kwenye
mkutano huo. Kitendo hiki kiliifanya FIFA kufanya uchunguzi ambao
matokeo yake yalikuwa kuwasimamisha Bin Hammam na Warner kwa kile
kilichoitwa ukiukwaji wa maadili.
Warner
aliondoka FIFA akiwa hana doa kwa kuwa aliwahi kuondoka kabla mambo
hayajaharibika huku jamaa wake Bin Hammam akikutwa na hatia ambako
alifungiwa maisha kujihusisha na soka. Hata hivyo adhabu hiyo ya
kifungo cha maisha iliondolewa na mahakama maalum kwa rufaa za michezo
CAS ambako kwa sasa Bin Hamamm anakumbana na tuhuma za matumizi mabovu
ya fedha za Chama cha soka cha Asia .
No comments:
Post a Comment